Tanzania awards $500 mln oil supply deal to Swiss firm Augusta; GVT hope will lower prices...

Mkuu, nimecheka sana hii hofu yako. Hizi ni fedha wanazotoa Oil Marketing companies kwa mahitaji yao ya muda huo, na wala si serikali. Ni kwamba, badala ya wao kununua mmoja mmoja, sasa wameform kampuni inayokusanya mahitaji yao na kutangaza zabuni kwa ajili ya kuwaletea. Nitakutafutia literature proper nikutumie, ilimradi usiwe mvivu wa kusoma. Nitapenda u argue ukiwa na full knowledge.
Mkuu Uchumi wa nchi hauandaliwi na mashirika bali serikali na ndjio maana tuna Rais. Kama ingekwua hivyo kuna sababu gani ya kuwa na rais ikiwa mashirika yenyewe yanaweza kufanya hivyo!. Bado nakueleza kwamba hakuna biashara yoyote ya kiuchumi inayoweza kufanyika pasipo kupangwa mabadilishano, lazima serikali ijali sana negative balance of trade.Tunanunua mafuta toka kampuni ya Swiss sisi tunauza nini?..Bado huelewi mkuu wangu..

Nchi inaweza tu kuendelea ikiwa nayo unauza mali zake nje, na sio kuwa at users end..hii ndio maana ya Ubepari kibiashara. Serikali inaanda mazingira bora ya biashara baina ya watu wake (mashirika) kuuza nje na pia washirika ya nje kuuza ndani kwa kuweka mkazo wa mabadilishano..Huwezi kuacha milango wazi kila mtu aingie maadam kashinda Tender ati tunapeleka mazao yetu soko huria tu watakao taka kununua wanunue - Hapana, tunalazimishana kununua mali zetu ndio Ubepari wenyewe na ndio maana unawaona kina Obama wako Japan na China. Nunua changu hiki nami nitanunua chako kile hutaki nitakwenda nchi wanayotaka kununua mali zangu..
 
Nijuavyo mimi siku zote biashara kubwa za kimataifa kama hii hufanywa kutokana na makubaliano ya kibiashara baina ya serikali yetu (rais) na nchi inayotoa mafuta (rais wao). Kwa mfano tutanunua mafuta Saudia kwa kiasi kadhaa wakati huo huo nao wakinunua mali zetu ktk mabadilishano ya bidhaa na siii mikataba kama hii ya kuzawadia mashirika binafsi. Kazi hiyo itafanywa na Saudia ili kurahisisha na kufuatilia kodi za export ya mafuta yao..

Nakumbuka vizuri sana wakati wa Nyerere tulikuwa hatuzawadii mashirika binafsi bali ni mikataba baina ya nchi mbili na hii ndio kazi ya IKULU kutafuta uwezekanao wa free trade baina ya nchi mbili.. Haya nayoyaona Bongo ni ya kipekee.. ONLY IN TANZANIA..

Hawa jamaa wameleta petrol inayoaminika iko chini ya kiwango cha ubora wa petrol kwa matumizi ya Tanzania. Kila mtu naona yuko kimya! What the hell is going on???
 
Badala yake wamezawadiwa mkataba mwingine...kweli wajinga ndio wali wao.
 
Hawa jamaa wameleta petrol inayoaminika iko chini ya kiwango cha ubora wa petrol kwa matumizi ya Tanzania. Kila mtu naona yuko kimya! What the hell is going on???
UTAPELI mkuu wangu, utapeli bado unaendelea halafu watu kama Mbalamwezi wanashangilia!... jamani jamani hivi mtaamka lini nyie Wadanganyika..Bofya
Labda nimuulize hili.. Marekani na EU wamepiga marufuku kununua mafuta ya Iran, nao China na India wamesema wao wataendelea kununua mafuta ya Iran.. how come?.. Je sisi tunaponunua mafuta kutoka shirika hili tunajua mafuta yao wanayatoa wapi?
 
Sometimes napata shida na utafuta majibu lakini naishia kujijibu na hakuna wa kumjmuliza.Mpango huu wa kuagiza ni Bulk ulifumuka na kubuni wa Masebu na team yake ya EWURA baada ya crisis ya mafuta Tanzania.Kipindi kila walionekana kwenye Televison wakijitetea kuwa ujio wa style hiyo ungepunguza vitendo vya muagizaji mmoja mmoja kuja na visingizio vya bei ya soko na hivyo kuleta usawa na idadi ya kiwango sahihi cha maitaji yetu ungefanyika.Yani kwa lugha nyingine alimaanisha kuwa kwa style hii ya BULK tungefaidika na mambo mawili kwa mpigo moja ni bei kutoku kubadilika badilika na mbili wingi wa mafuta utaondoa upungufu [shortage] ya mafuta hapa nyumbani kwa visingizio vya usafirishaji.

Lakini napata shida na kwa swala hili naungana na Mkandara hivi hii balance of Trade kwetu inafanyaje kazi jamani?
Tulibinafisisha kila kitu hatimae kila kitu tumekuwa wachuuzi,matokeo yake Rais wetu akiluka na ndege kwenda nje anakwenda kwenye vikao vya kisiasa na mialiko ya dhifa za kipriotocal za serikali na si kutengeneza mikataba ya kibiashara itakayo ifaidisha Tanzania na maskini walio Arumeru.

Hivi kwani tuliuza na kubinafisisha migodi,tungekuwa tunamlki baadhi ya migodi yetu chukulia mfano wa migodi ya vito vya thamani Alimas na Tanzanite leo hii Rais badala ya kutoka hapa akaenda Saudia Arabia akaongea na Serikali ya huko akiwa na Economic delegate ya waataalamu wa BOT kuwa nina so and so carat of Dimonds from Tanzania I need this much Tons of fuel is there a deal Gentleman.

Hakika uchumi huu wa kichuuzi unaotumaliza matokeo yake Serikali inaingia deal na kofia ya mashrika ambayo kwao wao PROFIT MAXIMIZATION ni kanuni,wala sio swala la majadiliano.Lakin viongozi wanavyokuwa wabishi watatetea kuwa Makampuni kama hayo hayako kwa ajili ya Profit.

Hivi ni kwanini Serikali ilibinafisiha mgodi wa Mwadui [Diamonds] hivi ni kwani Serikali iliweka wawekezaji kwenye migodi ya Tanzanite Merelani tumekosa nini? Hivi Serikali imekosa heavy intellectual brains ziambiwe fulani na fulani kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano nakupa mgodi huu uzalishe kwa faida ya Watanzania nje ya hapo utalijibu Taifa even if is to put you in Lock up kwa kushidwa kuperform tutafanya kwako na kwa mkeo sema unaitaji nini upewe kutimiza ahadi hii.Na kweli kama hawa tunaoita jicho la nchi usalama wa Taifa wakaamishia nguvu zao huko kulinda na kutetea rasilimali hiyo muhimu ya uchumi, ndani na nje kwenye centre selling organisation kokote duniani wangefanya na kuachana na lawama za kufukuzana na wana si asa wa kibongo.

Ni lini tutathamini mother nature nasi tukawa strongly proud kulinda TUNACHO CHETU NA HATUMPI MTU OTHERWISE NA YEYE ATUPATIE TUNACHOITAJI TOKA KWAKE [Barter system].

Hakika Mungu anifanya Rais kabla mwenyewe ajaludi ofisini kwa saa moja cha kwanza kuitaifisha ni migodi ya vito vya thamani na kuandika maisha yangu yote Mzungu,Mhindi,Mchina,wala Mzambalauu hatii mguu kwenye biashara hiyo inabaki ni Government deal on behalf of the people of united Republic of Tanzania, Rais akiludi migodi yote ya vitoa anakuta under seal.

Hivi ni nchi gani duniani isiyotaka Tanzanite au Diamonds,hasa izo zilizoendelea wanazitaka sana wako tayari kukupa chochote wapate hizo diamonds.Ndio kuna wacheza faul,kwa hili kazi ya usalama wa Taifa ndio ingekuwa sehemu muhimu kwao wao nao kuonyesha kuwa mafunzo waliyopata ni kwa ajili ya kutetea Taifa lao na kulinda mali zake ziuzike na kubadilisha popote pale duniani iwe ni kwa kubadilishana na mafuta, kupeleka watu shule, au chochote muhimi yakiwemo madawa ya binadamu.

Kaa nchi kadogo kwa aina hiyo ya ufahamu na mbwembwe za duniani uenda kangepata heshima yake na wakubwa wakakaheshimu kuwa na udogo wake kana watu ambao ni makinia na hatari kwa kulinda mali zao na wanajua wanachofanya.Mungu Taifa langu tumekosea wapi?
 
Wizi mtupu, "contract to supply oil for the first two months of 2012" Kesho kutwa tunaanza mwezi wa nne, sijui niseme nini hapa, kwamba Jamaa wameishamaliza kusupply mafuta tayari au ni nini? mambo ya kijinga jinga kama haya ndio huwa yanakuja kutucost issues zinapolazimika kuwa settled kwenye courts of law.
 
DSN,
Kwa mwaka tuna import mafuta tu zaidi ya billioni 2.5 Usd, hii tunaitupa tu kwa shrika la uchuuzi bila Swiss kununua chochote kwetu! Wao uchumi unazidi kukua na shirika share zake kupanda sisi tunatoka kapa. Halafu sisi na hiyo Mwadui diamonds na Tanzanite kwa nini nao wasiwe DSE na mchuuzi wetu wenyewe..ooh! Hatuna uwezo na longolongo.Lakini kwa ujinga wetu tunapeleka sigara na bia zinazouzwa ktk local market at ndi soko huria.. Aaaah linchi hili bana..
 
Sangara, hiyo article isikuchanganye ni ya Nov 2011. Mkandara, si kwamba nashabikia, bali najadili mfumo ulivyo na unavyofanya kazi. Wengi wetu tuna tabia ya kuzungumzia mambo bila facts. Nimekuwa nikifuatilia tatizo la mafuta na solutions zake kitambo. Imetokea tu kuwa nimechangia kwa kuonyesha namna unavyofanya kazi hasa kwa kuzingatia michango ya wenzangu.
 
Huu ni utapeli oil iko kwenye soko la dunia na kufanya Bulk imports haitapunguza bei!!!. Tanzania ina magari yasio zidi million 1 sasa Bulk imports ni kiasi gani?. Vilevile kwasababu soko ni la dunia nzima ni kwanini wauzaji watoe unafuu wakati India, China, USA, Brazil wananunua oil 1000% zaidi ya sisi? kwanini wasiwape discount hao!!. Kitu kingine kwasababu serikali inafanya Bulk imports inasababisha oligopy kwa hiyo kampuni kwasababu haina ushindani? sasa bei itashuka vipi wakati mwingizaji ni mmoja anaweza kutafuta sababu yeyote ya kupandisha bei. Hizi kama tulivyosema mwanzo ni 10% za watu wa serikali tu. Biashara zote za oil na kampuni zipo hapa Houston, TX kwa wasiojua hapa ndiyo Head Qtr ya oil business in the World!!. Huu ni upuuzi tu

Kwanini wewe usi bid? ilitangazwa.
 
Wizi mtupu, "contract to supply oil for the first two months of 2012" Kesho kutwa tunaanza mwezi wa nne, sijui niseme nini hapa, kwamba Jamaa wameishamaliza kusupply mafuta tayari au ni nini? mambo ya kijinga jinga kama haya ndio huwa yanakuja kutucost issues zinapolazimika kuwa settled kwenye courts of law.

Soma article ni ya lini na nyuzi ilianzishwa lini kabla hujaanzisha maandamano!
 
DSN, tuwe fair. mfumo unaouongelea ulianza kubuniwa 2008. Kwa hiyo, utakuwa husemi ukweli kuuhusisha na mgomo wa juzi. Research kwanza before you speak.

Mkuu Mkandara,

naona unachanganya vitu vingi sana kwenye hii topic.

1. Tunajadili ufanisi wa Bulk Procurement.
2. Unalaumu serikali kununua mafuta nje ya nchi.
3. Unalaumu kwa nini serikali inanunua mafuta kwa kisai chote hicho cha fedha huku ikiwa haiuzi kitu nje.
4. Umependekeza Rais angeingia mkataba na nchi zenye mafuta.
5. Unaongelea Hisa...
Mwingine anaongelea madini

Nadhani tungerejea kwenye point kwamba, uendeshaji wa uchumi hutegemea mafuta. Kwa muda mrefu sana, (toka 1999 soko huria la mafuta lilipoanza rasmi) wauza mafuta wamekuwa wakinunua kwa mfumo ambao baadaye wachumi wameona ni inefficient.

Ninakubaliana nawe kuwa we import too much. Toka ndege hadi toothpick. lakini je, wewe unashtuka ku import mafuta leo? tumekuwa tunaagiza mafuta toka nchi hii ipate uhuru. So, kwa kuanzia, kuagiza mafuta ni jambo ambalo kwa sasa hatuwezi kulibishania, maana inabidi iwe hivyo hadi tutakapothibitisha yapo ardhini na tunaweza kuyachimba.

la muhimu, ni kuongeza export kwa, pamoja na mambo mengine, kuprocess mazao ya biashara yatukomboe, hasa kwa kuwa watu wengi wanategemea kilimo na hii inaweza kusaidia kuupunguza umasikini. Mikataba mizuri ya madini ni lazima ili tunufaike pakubwa.

Lingine, ni kuongeza uzalishaji wa gesi asilia tufulie umeme ili tuweze ku export kujaribu kupunguza trade deficit.

Kuuliza kwa nini tunaendelea kununua mafuta (eti kwa kuwa tu Marekani kapiga marufuku kununua mafuta ya Iran) ni nje ya topic na pia ni utumwa wa kifikra.
 
Betweeen July 2011 and January 2012, Price of oil rose by 39.6 percent to an average of USD 973.4 per ton, while the volume of oil imports rose by more than 67 percent to 2.3 million tons…

On the other hand, traditional exports declined by 18.1 percent to USD 282.6 million, largely due to a fall in production of coffee, cotton, tobacco and cashew nuts following unfavorable...

Source: BoT Mid Year Economic Review
 
DSN, tuwe fair. mfumo unaouongelea ulianza kubuniwa 2008. Kwa hiyo, utakuwa husemi ukweli kuuhusisha na mgomo wa juzi. Research kwanza before you speak.

Mkuu Mkandara,

naona unachanganya vitu vingi sana kwenye hii topic.

1. Tunajadili ufanisi wa Bulk Procurement.
2. Unalaumu serikali kununua mafuta nje ya nchi.
3. Unalaumu kwa nini serikali inanunua mafuta kwa kisai chote hicho cha fedha huku ikiwa haiuzi kitu nje.
4. Umependekeza Rais angeingia mkataba na nchi zenye mafuta.
5. Unaongelea Hisa...
Mwingine anaongelea madini

Nadhani tungerejea kwenye point kwamba, uendeshaji wa uchumi hutegemea mafuta. Kwa muda mrefu sana, (toka 1999 soko huria la mafuta lilipoanza rasmi) wauza mafuta wamekuwa wakinunua kwa mfumo ambao baadaye wachumi wameona ni inefficient.

Ninakubaliana nawe kuwa we import too much. Toka ndege hadi toothpick. lakini je, wewe unashtuka ku import mafuta leo? tumekuwa tunaagiza mafuta toka nchi hii ipate uhuru. So, kwa kuanzia, kuagiza mafuta ni jambo ambalo kwa sasa hatuwezi kulibishania, maana inabidi iwe hivyo hadi tutakapothibitisha yapo ardhini na tunaweza kuyachimba.

la muhimu, ni kuongeza export kwa, pamoja na mambo mengine, kuprocess mazao ya biashara yatukomboe, hasa kwa kuwa watu wengi wanategemea kilimo na hii inaweza kusaidia kuupunguza umasikini. Mikataba mizuri ya madini ni lazima ili tunufaike pakubwa.

Lingine, ni kuongeza uzalishaji wa gesi asilia tufulie umeme ili tuweze ku export kujaribu kupunguza trade deficit.

Kuuliza kwa nini tunaendelea kununua mafuta (eti kwa kuwa tu Marekani kapiga marufuku kununua mafuta ya Iran) ni nje ya topic na pia ni utumwa wa kifikra.

Kama bulk procument ina manufaa mbona January tulinunua mafuta kwa bei kubwa kuliko iliyokuwa sokoni?? Hivi nani ni a? Yule jamaa ex addax na muitaliano au kuna wana siasa ndani? Tunaotetea kwamba kila kitu kiko sawa, kwanini juzi ile kampuni ya uagizaji inayojiita PIC waliumana meno katika ya mwenyekiti wa bodi na viongozi wa makampuni matatu makubwa yenye veto kwenye hiyo kampuni? Tanzania tukiendelea kuiendesha hivi sijui tutaenda na kufika wapi!!!
 
Kama bulk procument ina manufaa mbona January tulinunua mafuta kwa bei kubwa kuliko iliyokuwa sokoni?? Hivi nani ni a? Yule jamaa ex addax na muitaliano au kuna wana siasa ndani?

Mkuu Ndahani,

hebu tusaidiane hapa, bila ushabiki. Bei ya mafuta ilikuwa juu kwa kiasi gani kuliko ya wapi?
na je, Addax alifanya nini na wapi? kwa mujibu wa taarifa za PIC kwenye kamati ya bunge ya nishati, na ambayo hata TAOMAC wenyewe hawakuipinga, na hata jamaa wa Addax, ni kuwa waliokosa zabuni walianzisha fitna kwenye magazeti. Kampuni zetu za local na za nje zilishindwa kufuata masharti ya tenda kizembe kizembe tu...Unaelezwa kufunga nyaraka kwenye bahasha moja, wewe unafunga kwenye bahasha tatu tofauti? Unaelezwa kuambatanisha original unaweka copy? wakawa disqualified, wakagombana, baadaye wakakaa kimya. wangekuwa na haki, ungewaona wameenda FCT kuappeal.

Ki ukweli kama ni uhuni labda wanafanyiana wao kwa wao kwenye kuibiana nyaraka za zabuni, maana wote wanashiriki kuunda bodi ya kuendesha hiyo PIC Ltd. Na kama siasa, wabunge wengine katika kamati pia ni wafanya biashara za mafuta hayo hayo...Azimio la Arusha?
 
Sometimes napata shida na utafuta majibu...Lakini napata shida na kwa swala hili naungana na Mkandara hivi hii balance of Trade kwetu inafanyaje kazi jamani? Tulibinafisisha kila kitu hatimae kila kitu ...

DSN, hilo ndo jibu sahihi. Tulikosea sana kufanya ubinafsishaji kwa fujo. Wakati IMF walipotushauri kuvunja TIPPER refinery, hatukujiuliza mara mbili. Wenzetu Kenya na Zambia walikataa na wanapeta hadi leo.

na kuhusu urari wa biashara (trade deficit) hautakwisha ikiwa tutaendelea kuagiza hata toothpick na kuacha kukzaia uzalishai wa bidhaa zilzo ndani ya uwezo wetu.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Isaiah 54 na Malamwezi,

Mimi sikubaliani kabisa na huu mfumo na si kweli kwamba huu mfumo unapunguza bei ya mafuta!!!. Cha kujiuliza ni kwa nini bei ya hizo kampuni inatofautiana sana wakati bei ya kitaifa ni moja? Nitajaribu kuwaelimisha lakini nanyi mnatakiwa kufanya research na kuelewa siko la dunia kwani ukiangalia Tanzania pekee huwezi kujua kama unaibiwa au la. Nimewapa data za fact za 2010 lakini cha maana hata kama Tanzania imeongeza uingizaji zaidi ya mara mbili itakuwa 76,000 bbl/day ambayo ni ndogo sana kitaifa!!.

Biashara ya Tanzania inavyofanyika:
Hizo kampuni zinazo bid kwenye tender ya kufanya supply za mafuta wanafanya hivi: Kwenye oil trade kuna watu wanaotabiri bei ya mafuta itakuwaje kwa siku zijazo labla miezi sita (6), mitatu (3) au hata mwaka. Hivyo kinachofanyika ni kwamba kampuni zinanunua mafuta kwa wingi labla kwa mfano leo wamenunua mafuta kwa $100 na wataalamu wao wamewaambia mafuta mwezi wa saba yatauzwa $120 lakini hawana uhakika yanaweza yakawa zaidi au yakawa pungufu. hizo kampuni zinaenda kwenye tender kama za Tanzania na kuwaambia tutakuuzia mafuta kwa $115 bbl mwezi wa saba na wenyewe wamenunua leo $100 bbl hivyo watatengeneza $15 bbl. kama bei itakuwa chini mfano $90 bbl Tanzania bado itanunua mafuta kwa $115 kwasababu hiyo ndiyo Tender na kama bei ikipanda kuwa $120 bbl Tanzania itanunua kwa bei ileile ya makubaliano ya $115 bbl. Hii system inaitwa ku Hedge! mara nyingi wanaoumia ni wanunuzi si wauzaji!!!.
Kwanini Tanzania inatumia hii system:

1. Watu wengi wanaweza kula rushwa kwenye hii system maana hwanunui moja kwa moja kwenye soko la dunia hivyo unaweza kuweka 10% yako kwenye kampuni hizi.
2. Malipo yanaweza kuchelewa kitu ambacho huwezi kufanya kwenye soko la dunia kama Chicago commodity market hivyo unaweza kuanza kuwazungusha zungusha kidogo kama kwenye kampuni za ujenzi na umeme wanavyofanya. Njia hii inatumika kwa viongozi ili waanze kuombwa ombwa kila siku na kuongeza power yao.
3. Ni rahisi kuelezea kwenye budget kwasababu unaweza kuwaambia bunge bei ni $115 hivyo ukapata budget na inaonekana kama ni uwazi!.

Kampuni za huku kubwa haziwezi kufanya bishara hizi kwasababu fine za rushwa ni kubwa sana Chevron mfano imelipa $300m fine kwa serikali kwa kufanya biashara kama hizi huko Nigeria na Guine.

Ni lazima tuelewe BP nayo imejitoa Tanzania na nchi nyingi za Africa kwasababu ya kuhofia rushwa kubwa ambayo inaweza kuweka kampuni yao hatarini wakati faida si kubwa hivyo. Nafahamu watu waliofanya uamuzi wa kuuza assets za BP Africa kwa Apache!.

Hizi biashara zimebaki kwa Hedge Fund na kampuni ndogo ambazo haziangaliwi vizuri lakini hii system unaenda kulipa zaidi kuliko Tanzania kununua mafuta yenyewe kwenye soko la dunia. Tender system ni rushwa kubwa!.

Kama hapa hamjaelewa basi ndugu siku nyingine!!!
\

DSN, tuwe fair. mfumo unaouongelea ulianza kubuniwa 2008. Kwa hiyo, utakuwa husemi ukweli kuuhusisha na mgomo wa juzi. Research kwanza before you speak.

Mkuu Mkandara,

naona unachanganya vitu vingi sana kwenye hii topic.

1. Tunajadili ufanisi wa Bulk Procurement.
2. Unalaumu serikali kununua mafuta nje ya nchi.
3. Unalaumu kwa nini serikali inanunua mafuta kwa kisai chote hicho cha fedha huku ikiwa haiuzi kitu nje.
4. Umependekeza Rais angeingia mkataba na nchi zenye mafuta.
5. Unaongelea Hisa...
Mwingine anaongelea madini

Nadhani tungerejea kwenye point kwamba, uendeshaji wa uchumi hutegemea mafuta. Kwa muda mrefu sana, (toka 1999 soko huria la mafuta lilipoanza rasmi) wauza mafuta wamekuwa wakinunua kwa mfumo ambao baadaye wachumi wameona ni inefficient.

Ninakubaliana nawe kuwa we import too much. Toka ndege hadi toothpick. lakini je, wewe unashtuka ku import mafuta leo? tumekuwa tunaagiza mafuta toka nchi hii ipate uhuru. So, kwa kuanzia, kuagiza mafuta ni jambo ambalo kwa sasa hatuwezi kulibishania, maana inabidi iwe hivyo hadi tutakapothibitisha yapo ardhini na tunaweza kuyachimba.

la muhimu, ni kuongeza export kwa, pamoja na mambo mengine, kuprocess mazao ya biashara yatukomboe, hasa kwa kuwa watu wengi wanategemea kilimo na hii inaweza kusaidia kuupunguza umasikini. Mikataba mizuri ya madini ni lazima ili tunufaike pakubwa.

Lingine, ni kuongeza uzalishaji wa gesi asilia tufulie umeme ili tuweze ku export kujaribu kupunguza trade deficit.

Kuuliza kwa nini tunaendelea kununua mafuta (eti kwa kuwa tu Marekani kapiga marufuku kununua mafuta ya Iran) ni nje ya topic na pia ni utumwa wa kifikra.
 
Kamundu, nakuelewa sana mkuu, ila nasikitika kwa kuwa nahisi ninachokiandika mimi wewe husomi ukaelewa au husomi kabisa.

1. Ninafahamu sana namna hedging inavyofanya kazi, lakini kwa mfumo huu inakuwaje hedging wakati haihusishi bei ya mafuta? Gharama zinazotajwa kwenye mfumo huu ni Freight na Insurance, halafu bei itakuwa inatumika ya sokoni wakati huo. Hujaelewa wapi hapa?

2. Kwa mfumo ulivyo operators wa Petroleum Importation Coordinator Ltd (PIC) ni mkusanyiko wa wakurugenzi wa kampuni za mafuta Tanzania. Wao wanagombea biashara hiyo hiyo kwa mfumo wa tenda. Sasa ukisema rushwa, wanampa nani ili kiwe nini? Au una assume rushwa wapeane wao kwa wao ili wamwachie mmoja wao ashinde zabuni?

Ni vema ukajikita zaidi kuelewa kwanza namna imports zinavyofanya kazi bada ya assumptions za hedging za USA na Canada peke yake. Ninakubaliana na wewe kuukosoa mfumo huu, lakini huwezi kuukosoa kabla kuelewa unafanyaje kazi.
 
Mkuu Ndahani,

hebu tusaidiane hapa, bila ushabiki. Bei ya mafuta ilikuwa juu kwa kiasi gani kuliko ya wapi?
na je, Addax alifanya nini na wapi? kwa mujibu wa taarifa za PIC kwenye kamati ya bunge ya nishati, na ambayo hata TAOMAC wenyewe hawakuipinga, na hata jamaa wa Addax, ni kuwa waliokosa zabuni walianzisha fitna kwenye magazeti. Kampuni zetu za local na za nje zilishindwa kufuata masharti ya tenda kizembe kizembe tu...Unaelezwa kufunga nyaraka kwenye bahasha moja, wewe unafunga kwenye bahasha tatu tofauti? Unaelezwa kuambatanisha original unaweka copy? wakawa disqualified, wakagombana, baadaye wakakaa kimya. wangekuwa na haki, ungewaona wameenda FCT kuappeal.

Ki ukweli kama ni uhuni labda wanafanyiana wao kwa wao kwenye kuibiana nyaraka za zabuni, maana wote wanashiriki kuunda bodi ya kuendesha hiyo PIC Ltd. Na kama siasa, wabunge wengine katika kamati pia ni wafanya biashara za mafuta hayo hayo...Azimio la Arusha?

Nipe muda ntakupa actual prices...mid of next week. Ila, Kwani Augusta alinunua wapi mafuta yale ya January? Halafu si kweli kwamba Addax ilununua magazeti. Kwani nani asiyejua jinsi tunavyoyapeleka mambo TZ. Anayesema ukweli ndo anaambiwa mzushi na muongo ili mradi watu walinde maslahi yao!
Na kaka naamini sote tuna nia njema na Tanzania. Augusta kwani ni ya nani? Sio yule muitaliano aliyekuwa AGIP au Tiper hapa hapa Tanzania anayewakilishwa na ex Addax(Mgoa)?
Halafu standard zetu za kukataa tender ni namna ya kufunga tender document kwenye bahasha???? Well, time will prove us right or wrong. What I suspect ni kuwa hatujui tunachofanya. Tuendelee kushupaa na kujenga haya makampuni makubwa ya nje. Tutakaojililia ni sisi maana hela za kwetu na uwezo wa kujenga kampuni zikawa kubwa pia tunao.Tunaposhindwa ni tamaa zetu na njaa ndogo ndogo tu, however clean we try to convince people that we are.
 
Augusta Energy Wins $750 Million Tanzania Tender to Supply Oil

By David Malingha Doya - Mar 29, 2012 12:49 PM GMT+0

Augusta Energy SA, a Geneva-based oil trader, has for the third time won a tender to supply petroleum products to Tanzania, under the East African country’s bulk-procurement system.
“The tender is estimated to be worth $750 million at today’s price,” Shanif Mansoor, chairman of Tanzania’s Petroleum Importation Coordinator Ltd., said today in a phone interview from Dar es Salaam, the commercial capital. PIC, as the company which groups oil-marketing companies in Tanzania is known, issues a tender to import fuel every two months.
Augusta Energy will supply 640,000 metric-tons of oil products for delivery in May and June, Mansoor said. The next tender will be issued in two months for consumption in July and August, he said.
Tanzania consumes 1.54 million cubic meters (407 million gallons) of petroleum annually, according to information on the website of the Energy and Water Utilities Regulatory Authority. The country is also a transit hub for oil products that are shipped to nations in the region including the Democratic Republic of Congo, Rwanda, Burundi and Zambia.
To contact the reporter on this story: David Malingha Doya in Dar es Salaam atdmalingha@bloomberg.net
 
DSN, hilo ndo jibu sahihi. Tulikosea sana kufanya ubinafsishaji kwa fujo. Wakati IMF walipotushauri kuvunja TIPPER refinery, hatukujiuliza mara mbili. Wenzetu Kenya na Zambia walikataa na wanapeta hadi leo.

na kuhusu urari wa biashara (trade deficit) hautakwisha ikiwa tutaendelea kuagiza hata toothpick na kuacha kukzaia uzalishai wa bidhaa zilzo ndani ya uwezo wetu.

Hakuna shirika la umma lililokuwa na faida, watu wanaiba hazina inalipa mpaka mishahara. Mitanzania ililemaa kwa neno "umma", ikiwa mali ni ya umma, kwanini kila mmoja asichukuwe chake mapema na kujineemesha? huo ndio ujinga wetu.

Haohao walioziuwa mali za umma leo ndio haohao wanaolalamikia mfumo wa kibepari!

Mfumo tulionao sasa, ni wengi wawafanyie kazi wachache, tukipenda tusipende ndio upo.

Zambia na Kenya ni nchi za kibepari tokea mwanzo na huna cha kuwaambia, kule hata mfanyakazi anakuwa na discipline ya hali ya juu kwani hakuna cha umma. Kwetu watu hata kwenye kampuni za watu binafsi bado wanafikiri ni za umma.
 
Back
Top Bottom