Mkandara kila la kheri! Umefika wakati wa kutafsiri maneno kwa vitendo tangulia nasi twaja.. mie nasubiri Kitila akiwa Mwenyekiti tutakuwa wote.
Anyway back to the issue, ruzuku ni Saratani mbaya SANA inayomaliza vyama vya upinzani kidogo kidogo. CCM wanalijua hilo na wanalifanyia kazi kisawa sawa (rejea sakata la Mrema Vs Marando, Mrema Vs Lwekama, Mrema Vs Tado etc) na ukitafakari kwa undani utaona haya yaliyojadiliwa hapa Ujinga, upumbavu, ushamba, ujuha nk ni nadharia ambazo ukitaka kuziona kwa vitendo kinyang'anyiro cha ruzuku kitakupa jibu.
Mtego wenyewe upo pale kwenye sheria isiyo tambua muungano wa vyama, hivyo kama mtakubaliana kuungana ni kivyenu tume inatambua mgombea wa chama kimoja tu. Huko Chadema unakoenda waulize walipoiunga mkono CUF mwaka 2000 yaliwakuta yepi. Baya zaidi mbali na ruzuku kuna fitna ya viti maalum kwa kina mama, ambavyo navyo hugawiwa kulingana na viti vya kuchaguliwa ktk baraza la madiwani na Bunge. Kwa msingi huo kitendo cha kumuunga mkono mwenzio mbali na kumuongezea ruzuku bali pia kunamuongezea viti maalum.
Kwa msingi huo basi utaona suala zima la muungano limegubikwa na vipingamizi kadhaa wa kadhaa vya kisheria na vya kimaslahi, by the time wapinzani watakapogundua hili (walau kudai sheria ibadilike) CCM watakuwa washatawala kwa miongo kadhaa.