GHIBUU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 4,432
- 3,006
Kumekuwa na mijadala mingi juu ya katiba mpya tanzania pamoja na zanzibar,lakini mimi nitakosoa kidogo,kukiangalia hapa lazima kutakuwa na matatizo ya muungano,kwanini tanganyika wajadili katiba zanzbar wajadili muungano ? Hili suala nimekuwa nikijiuliza sana lakini jibu nimelipata na lipo wazi kabisa.
zanzibar pamoja na wazanzibari wenyewe wanajadili suala la muungano kutokana wao ndio unaowaumiza,tanganyika wao hawaumizi,kivipi ? tanganyika ndio hii inayojiita tanzania hata ukiangalia nembo inayotumika kwa jina la tanzania ni ile ile ya tanganyika,kwa hiyo ni zahiri kabisa kuwa ni tanganyika,ni sawa zaire kuita kongo.
kwa hiyo masuala mengi ambayo ya tanganyika yako katika muungano na wao,na mamlaka yote imebeba serikali ya muungano,ndio maana wazanzibari wao wanajadili muungano kutokana ndio ulobeba mamlaka ya ya zanzibar,kivipi,kiuchumi inawaathiri,na zanzibar inataka isimame kama ni dola kamili kimataifa,iweze kiunuka kiuchumi.
kwa mfano mambo ambayo yanawarudisha zanzibar nyuma,katika masuala ya muungano kukosa kiti chao katika umoja wa mataifa,wazanzbari wanataka wasimame kama ni nchi na utaifa wao.
Kiuchumi nayo inawaasiri,wanakosa misaada kutoka katika umoja wa mataifa na duniani kote,kiasi ambacho msaada wowote unaokuja tanzania ambao hasa wa zanzibar unapitia katika muungano na walengwa ambao wao hauwafiki,kielimu pia hawafaidiki hasa ya juu kunapotokea nafasi za nje,ki afya misaada kutoka njee,wawekezaji kutoka njee,hayo yote yanaishia katika serikali ya muungano,mikopo inaishia katika muungano,ndio maana wazanzbari wanataka muungano ujadiliwe upya.
Lakini nikifata history ya muungano huu una ulakini,nafikiri ipo haja ya kujadiliwa kwa pande zote mbili,lakini mjadala huu vipi utafanyika wakati tanganyika haipo ?
Pia wazanzbari wanadai yakuwa mkataba wa muungano haupo,na ndio maana wao wanataka kuujadili,tumeona kuwa chanzo kikubwa cha mgogoro wa katiba pale zanzbar walipobadilisha katiba yao kuipa hadhi nchi yao kutambulika kama ni nchi,chama cha chadema wakaleta mjadala kuwa zanzbar imevunja mkataba wa muungano,na watanganyika wote wakaliunga mkono kuvunjwa kwa muungano huo kwa kipengele kile kinacho sema kule zanzbar ni nchi na ina mipaka yake.
sasa mi nataka kuuliza jee hatukuona kuwa muungano ulishavunjika zamani pale sisi watanganyika tukaivunja tanganyika kuita tanzania jee wakati tulipo ivunja tuliwashirikisha wenzetu wazanzibari ? laaa hakuna,jee muungano upo hakuna ? hakuna ... kutokana mshiki wake ameshakufa,hili ndio tatizo kubwa lililoleta mjadala zanzbar kwa kunyang'anywa mamlaka yake,mamlaka ya tanganyika yameingizwa katika muungano na ndio ikawa inaiburuza zanzbar.
masuala yanayohusu tanganyika basi tunaya force yaende na zanzibar,mfano zahiri TRA, pia tulitaka tuwapelekee TBS,haya ndio makosa makubwa tunayofanya,pia tunawapa asilimia 4.6 ya misaada kutoka njee,hii haiwezekani,kwani wao ni taifa huru na ni nchi,huu sio makubaliano,lazima tugawane sawa sawa.
Ndio maana zanzibar wanadai mamlaka yao ambayo miaka 47 imewarudisha nyuma kiuchumi,hivi sasa waziri kutoka zanzibar akitaka kuenda nje kuomba msaada lazima aombe ruhusa kwa muungano kutokana yeye ndie anayeshughulika na masuala ya njee na hii sio haki,tumewanyang'anya mamlaka yote.
kwa hiyo sasa hivi tanzania nafikiri ni wakati wa kujadili suala la muungano,tina tuwashirikishe wananchi,sio chama wala raisi wala waziri,tena pande zote mbili zanzabar na tanganyika.
Pili upitiwe mkataba wa muungano uwangaliwe umepitwa na wakati au bado,tatu tunangalie yale masuala ya muungano,na yajadiliwe na pande mbili sio bunge bali wazanzibar na watanganyika,tena kisheria,ikiwa wanasheria wa tanganyika wako sita na zanzbar sita ndio inavyo takiwa.
WazanzIbari wanadai na wanajadili na wanataka kujadili muungano kwanza ndio ijadiliwe katiba.
Muungano umeelemea kwa upande mmoja tu unaonekana,ndio maana watanzania bara hawakutaja sula la muungano kutoka wao haliwaumi,ili tuweze kufika huko tunako kwenda lazima tujadili muungano ndio tujadili katiba.
Lazima kuwe na mfumo wa serikali tatu lazima lazima au muungano uvunjwe,sisi watanganyika tunataka tusimame kama watanganyika na wazanzibari nao wasimame kama wazanzibari.
Tuwe na muungano kama wa east africa mashariki sio muungano huu sikuwa na tija na wala fair kwa pande zote mbili.
Mimi kama mimi ningependelea kuwe na serikali tatu sijui wewe mtanzania mwenzangu ?