Elections 2010 Tanroads ni EPA nyingine ya kutoa michoto kwa CCM

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Wadau: hii ni sehemu ya stori kuu katika Tanzania Daima ya leo. Nilipohighlight in red yaonyesha kwamba Tanroads katika uchaguzi huu ndiyo 'EPA' nyingine ya mchoto kwa ajili ya kampeni za CCM kujipatia ushindi. Sasa naamini kabisa kwamba ufisadi wa genge la JK ndiyo umewakimbiza makada mashuhuri ndani ya chama hicho kumfanyia kampeni, kwani kwa imani yao wanashindwa kabisa kumnadi mtu ambaye yumo katika dimbwi la ufisadi. sasa hivi ni familia yake tu na watu kama Makamba, Kinana na Bilal.





.....Akiwahutubia wananchi wa mji wa Mpanda katika mkutano mwingine, Dr Slaa alisema taifa limepoteza imani na Rais Jakaya Kikwete kwa sababu hana uchungu na nchi na amekuwa akishirikiana na mafisadi kutapanya rasilimali za nchi.

Dk. Slaa ambaye amekuwa akikumbushia jinsi alivyomtaja Kikwete miongoni mwa orodha ya mfisadi iliyotolewa Septemba 15, 2007, Mwembeyanga Dar es Salaam, alisema Kikwete anawalinda mafisadi, huku akijidai mbele ya umma kwamba anapigana na ufisadi.

Alimtaka Rais Kikwete atoe maelezo ya sh 29 bilioni, ambazo serikali ilipeleka TANROADS, ambayo imekuwa inatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma, ambazo nyingine zinasemekana kupelekwa kusaidia kampeni za CCM badala ya kujenga barabara zilizokusudiwa.

"Aseme hizi shilingi bilioni 29 zilizotolewa CRDB kwenda TANROADS zimejenga barabara gani? Tumepoteza imani na Rais. Anashindwa hata kusimamia barabara za nyumbani kwao, atawezaje kusimamia hizo anazoahidi kujenga kwingine?" alihoji.

Dk. alisema barabara ya Bagamoyo–Msata ambayo ilitengewa shilingi bilioni 12 kupitia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) miaka mitatu iliyopita, kwa mkataba wa awali, haijajengwa, lakini Kikwete anaahidi barabara mpya kwingine bila kufuatilia ujenzi wa barabara hiyo.

"Aseme, walipewa ngapi, zimetumika ngapi, kwa nini mkataba umevunjwa…kama za jimboni kwake zimeliwa anatangaza za majimbo mengine…kwa nini tusiseme kuna ulaji wake katika barabara hizo?" alihoji.

Dk. Slaa alisema katika kudhihirisha kwamba Kikwete hayuko makini, anafanya njama kumrejesha ofisini Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Ephraim Mrema, ambaye amekuwa akilalamikiwa kwa tuhuma mbalimbali zinazohusu ubadhirifu wa fedha za barabara, huku zikiwapo tetesi kwamba aliwekwa pale ili kufanikisha kukusanya pesa za uchaguzi kwa ajili ya CCM.

Alisema amepata taarifa kuwa katika siku za karibuni, Rais Kikwete amemtonya Mrema kuwa ameagiza nafasi hiyo itangazwe gazetini ili kuwazuga watu wanaolalamikia uteuzi na utendaji wake.

"Kikwete amemwambia Mrema wa TANROADS kuwa ‘nimeagiza nafasi yako itangazwe ili kina Dk. Slaa wasipate hoja ya kuongea', anamwambia chinichini…kumbe ndiyo maana Kikwete amekuwa akishindwa kuchukua hatua kila tulipomlalamikia bungeni kuhusu ufisadi TANROADS … sasa tunataka maelezo kutoka kwake," alisema.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wakazi wengi wa mji huo, Dk Slaa pia aliwaonya polisi kuwa makini katika kusimamia haki na amani katika uchaguzi huu.

"Nchi ikiingia katika machafuko CCM itapata laana, na polisi hamtabaki salama. Mwaka 2001, wananchi wa Zanzibar walipoteza maisha, wengine wakawa wakimbizi kutokana na kauli za viongozi wa CCM na polisi….CHADEMA tunataka uchaguzi wa amani na ulio huru. Amani ikivunjika historia itawahukumu," alisema.

Dk. Slaa alikuwa akizungumzia vikundi vya vijana wa CCM ambavyo vimekuwa vikifanya fujo kwenye mikutano ya CHADEMA, na taarifa kuwa wana usalama wa taifa wamesambazwa nchi nzima kusaidia uchakachuaji wa kura.

Alisisitiza kuwa, kazi ya usalama wa taifa ni kulinda usalama wa taifa, si usalama wa CCM au wa Kikwete.

Alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kuwa kisheria, wana usalama hawaruhusiwi kukanyaga kwenye mikutano ya siasa au kwenye vituo vya kupigia na kuhesabia kura.

"Mkiwaona, kama hamuwawezi, tupigieni simu tuwashughulikie," alisema.

Aliwaomba polisi na majeshi yote kujiepusha na siasa, na badala yake kufanya kazi yao kwa uadilifu usiopendelea upande wowote, kwa maana wanaweza kujikuta wanamtetea na kumlinda kiongozi ambaye hatashinda uchaguzi, jambo linaloweza kuwapatia msukosuko baada ya uchaguzi.
 
Asante Mkuu kutuwekea habari hii. Hata mimi naamini hivyo kwamba Tanroads ndiyo mchoto mkubwa wa wagombea wa CCM na habari nilizopata ni kwamba John Nchimbi aligawiwa mamilioni ya mapesa kutoka Tanroads. Bila shaka haya haya yote yatakuwa hadharani na kwa kiasi kikubwa yatatikisa huu uchaguzi. Subirini tu.
 
Bora hii kashfa iwe hadharani mapema kuliko ije mwaka baada ya uchaguzi.
 
bora hii kashfa iwe hadharani mapema kuliko ije mwaka baada ya uchaguzi.

je mifuko yetu ya pension ipo salama? Hasa ppf ambako dg aliongezewa mkataba bila interview wakati aliyemtangulia aliondolewa kwa kisingizio cha interview ili huyu wa sasa aingie. Aliye tangulia alikuwa mlokole hatoa kitu kwao.
 
Back
Top Bottom