tANROADS MORO MNAMHUJUMU MKULO AU kILOSA?

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,083
5,066
Tangu mvua za masika zianze kumekuwa na usumbufu usio wa lazima kwa watu wanaosafiri kwenda Kilosa.Inabidi ukitokea Moro upitie Dumila safari ambayo huongeza zaidi ya Kilometa 50.
Tatizo lipo Mkata,Manzese na Chanzuru.
Mkata barabara ilikatika na vikawekwa vifusi bila kusindilia na matokeo yake magari yamekuwa yakikwama mno.Chanzuru kuna Mkandarasi anafanya light grading na kuna sehemu ndogo ambapo magari yamekuwa yanakwama na kutengeneza shimo kubwa ambalo sasa ni wiki ya pili hakuna gari inayoweza kupita;hii ina maana ya kuwa hata mgonjwa anayetoka kituo cha afya Kimamba inabidi aende mpaka Rudewa almost 12 kilometres kabla ya kupata barabara ya kwenda kilosa.
Mazense kuna seasonal river ambayo inaleta mchanga mara kwa mara;sehemu hii imekatika kiasi ambacho magari makubwa yanapata taabu mno kuvuka.
Tanroads naamini sehemu korofi ni ndogo mno na hazihitaji gharama ila inaelekea hamtaki kutoa kipaumbeleMnamkomoa nani????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom