Tanil Somaiya kukutana na waandishi

Sophia Simba na mwenzie Mkuchika mbona sijawasikia wakimjibu RA?....Double standards au ndo mambo ya ukipofu.....?
Mawaziri wa JK wanahitaji msaada mkubwa... Aidha ni tatizo la kujiamini kupitiliza ama ukurupukaji. Game lilikuwa mwanzoni sana, wakatia pua... Hawatakiwi kunyamaza kwani wanaonyesha wapi wameegamia, walitakiwa wamkemee hata RA ambaye kaenda zaidi ya kutumia televisheni moja!

Kabla ya kudandia hizi treni kwa mbele mawaziri wetu wawe makini sana.
 
Lakini wanajf, je mnakumbuka kwamba Tanil Somaiya alikuwa mtu wa karibu sana na Mengi miaka ya mwanzoni mwa tisini.

Tanil alikuwa na kampuni moja iliyokuwa inaitwa Sonia Industries Ltd. Ilikuwa sole distributor wa bidhaa za IPP hasa sabuni ya unga aina ya Foma, sabuni za kuogea aina ya palmolive, nk, ilikuwa pale Pugu road karibu na Quality Group ya Manji.

Kilichotokea ambacho siamini kwamba ni natural calamity, maji yalifunguliwa/yaliingia kwenye magodown yaliyokuwa yamesheheni sabuni za unga na kudaiwa kuziharibu zote. Sonia Industries Ltd, ikaenda mahakamani na kisha ikatangazwa mufilisi na kukwepa deni/madeni kutoka mabenki na watu mabalimbali akiwemo Mengi. Tangu hapo Tanil akawa anamkwepa Mengi hata magari yote yaliyokuwa ya mkopo toka kwa Mengi, Tanil akayabadiilsha majina na kuwapa ndugu zake wanaofanya biashara maeneo ya Kitumbini/Indra Gadhi, kisha akakimbilia Bukavu DRC. Aliporudi akaja na nguvu mpya na Kampuni ya Shivacom ambayo ndiyo mbia mkubwa wa Vodacom huko DRC kama ilivyo hapa,akiwa pia anamiliki sehemu kubwa ya hisa huko.

Kwa maana hiyo basi, ufisadi anaousema Mengi anaujua vilivyo kuliko wengi wetu tunavyofikiri. Ni swala la muda tu tutajua mengi zaidi. Na tuvute subra!
 
hapa ndipo iliposemwa kuwa aliye na mwana aeleke jiwe.
Ngoma ni ngumu na kila mdomo utasema sasa. wacha waparurane ila tutawadai nafsi zetu mda si mrefu.
 
Kamwe hatutapata ukweli kutoka kwenye 'press conferences' ! Ukweli (au sehemu yake) utapatikana mahakamani huko ndioyo wanapaswa kwenda.
 
Kazi ipo wakuu sasa sisi wenye nchi wazalendoo.....tumebakia hatuna chetu wanatamba wao tu kazi kweli kweli....

Hapo awali niliandika na sasa narudia, dola ya Tanzania 'imetekwa' na mafisadi ndiyo maana wanaweza kufanya lolote na wasichukuliwe hatua. It is state capture in the contemporary political science literature.

Mafisadi wanachojaribu kufanya ni kuimarisha imaya yao, ili waisguswe na mtu yeyote kwa lolote wafanyalo. Tishio la Mengi limewagutua, na dola ikiwa ni mateka tayari, imeahidi na kuwahakikishia ulinzi na usalama wa mali zao. Haya ni maamuzi ya mkutano wa Kamati Kuu ya CCM uliomalizika jana. Watuhumiwa wote watahitisha press conference.

Anachokiita RA kuwa ni ushahidi dhidi ya Mengi na kwamba anaukabidhi katika vyombo vya sheria, ni nyaraka za uongo/kughushi zilizotengenezwa na mawakala wa genge la ufisadi Ikulu kwa lengo la kupata kianzio/kisingizio cha kuanza 'kumshughulikia' Mengi. Vinginevyo, RA hana intelligence machinery ya kukusanya huo 'ushahidi.'

Kama mengi angekuwa amefanya jambo lolote kinume cha sheria, serikali ya Mkapa ingekuwa imemshughulikia siku nyingi. Matamshi ya Mkapa mara baada ya kutinga ikulu mwaka 1996 kuwa alitaka kumfilisi Mengi ndiyo yaliyozaa ugomvi baina ya Jenerali Ulimwengu/HCL na Mengi. hatimaye mpango huo ulikufa mara baada ya kuingiliwa na Mzee Mwinyi, marehemu Ali Juma (RIP), Malecela na Msuya. Mkapa alishinikizwa kuacha mpango huo, na baadaye Mengi kulipa deni 'halali' lililokuwa linadaiwa na NBC. Huo ndio ukweli wa mambo na bila ushabiki nani zaidi kati ya papa na nyangumi.

Serikali (mateka wa mafisadi) itamfungilia Mengi mashitaka 'kifani' mahakamani, lakini yenye lengo la kuhadaa umma kuwa Mengi ndiye mkosaji ili kumwadabisha, kumfilisi na hatimaye kutoa ujumbe kwa watu wengine (umma) wenye nia ya kupambana na ufisadi, kuwa wasithubutu tena kuwagusa mafisadi walioteuliwa na dola. Na hapo ndio utakaokuwan mwisho wa mjadala na harakati zote za kupambana na ufisadi.

Vinginevyo, tusubiri kuona yatakayojiri, muda si mrefu kuanzia sasa.

Njia pekee ya kuendeleza moto wa vita dhidi ya ufisadi na hatimaye kuinusuru Tanzania ni watanzania wote kwa sasa kujitokeza kwa wingi, na kupitia njia mbali mbali, kuungana na harakati za Mengi kupambana na ufisadi. Si Tanzania wala watanzania, isipokuwa mafisadi, watakaopoteza kitu iwapo tutashiriki wote kikamilifu katika vita hii takatifu ya kuikomboa nchi yetu!
 
Invisible,

Sasa kweli tumechoka na hizi press conference, hawa jamaa wanajua weaknesses za Mengi ndio maana wanaongozana kwa press conferences. Mbona hawakufanya hivyo Dr. Slaa alipowataja?

Mengi amewapa hawa jamaa njia ya kutokea nje.
 
Duh! press com kibao!, haya sasa waandishi wachumia tumbo, hiki ndio kipindi cha mavuno na kitadumu mpaka October, 2010.
 
nashindwa kucheka wala kulia, nabaki nagugumia tu.
kama serikali imesita kukemea kauli za RA za kukimbilia kichaka chza ubaguzi wa rangi basi mjue TUMEKWISHA.

siamini kama Bunge letu linasubiri kufundishwa kazi, i mean hichi ndicho kipindi cha kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali..... hakuna kipindi kingine zaidi ya hiki cha kurudisha heshima ya nchi (golden chance), ambapo wanaibuka mawaziri wanaongea kama wamelevywa na mvinyo mpya hata wanachosema hakieleweki

kila mtu kwa imani yake AOMBE kunusuru maisha ya kina mama na watoto watakaotaabika moto ukiwaka.
 
Na kwakuongezea kidogo, Mengi alimpa Tanil gari moja kali sana aina ya Mercedez Benzi ambalo lilikuwa linafanana kabisa na alilokuwa anatumia Mengi. Kipindi hicho ofisi za Tanil zilikuwa mtaa wa mosque karibu na iliko Diamond Bank sasa. Mengi alikuwa akienda mara kwa mara kwa Tanil na alikuwa anakunywa hata chai ama kahawa hapo ofisini. Ni kutokana na yaliyotokea huko Sonia Industries Ltd, Benzi nalo liliuzwa. Tanil kabla ya kutoraka akawa anajificha kwenye duka la ndugu yao mmoja aliyekuwa anauza baiskeli hapo Indra gadhi huku mara zote akitumia ama taxi au mojawapo ya magari ya ndugu yake huyo aina ya min pajero au Toyota Canter lililobadilishwa rangi na umililiki kutoka kwake kwenda kwa kampuni ya ndugu yake huyo ili kuweza kuwakwepa akina Mengi na wengineo waliokuwa mamemkopesha mamilioni ya shilingi.
 
Serikali mpaka ifuate urasimu kuwatia hatiani mfisadi papa ila walala hoi ni jela tu na faini fort night.
 
anaesema mengi si fisadi ana ushahidi wa kutosha. anaesema rostamu ni fisadi pia ana ushahidi wa kutosha. mimi nasema hv hawa wawili WOTE NI WEZI tofauti ni staili wanazotumia kuiba,mlioko nyumbani kataeni kugeuzwa kama chapati kwenye kikaango.
 
sidhani kama alifikiria, maana kesho yake live on TBC, aliyatamka tena maneno yale yale kwa lugha ya 'kishankupe' huku akiyatilia msisitizo wa kidole juu, mdomo akiubinjuwa. hapo kuna kufikiria kweli?.

Hivi huyo kiranja wa kitchen party naye anawasumbua vichwa, kinacho nisikitisha ni kwamba serikali yetu ni mufilisi kiasi cha kukosa watu makini wa kuwa mawaziri, hadi na huyu ss eti ni full minister? Yeye wange muacha huko kuwa MC wa Hadija Kopa na Kitchen party zote, make anafaa sana huko!
 
Tanil Somaiya ni mtu muhimu sana katika kitendawili cha tuhuma za rushwa wa Radar. Kwa wale wataokwenda kumsikiliza wasisahau kummuliza aliko rafiki yake toka utotoni na partner wake katika biashara Gaileshi ambaye alikimbia nchi na anatafutwa na SFO na Interpol. Somaiya atakuwa amefanya kitendo cha kizalendo akitupa fununu huyu mwenzake yuko wapi. Nina uhakika kama kuna mtu anajua Gaileshi aliko ni Somaiya.
Walifanya mengi pamoja katika deal za magari ya kijeshi na ndege ya rais.

Swali la pili ambalo ningefurahi akiuulizwa ni kwa nia gani ( mea culpa) hasa hasa alifadhili uchaguzi UV-CCM uliofanyika hivi karibuni? Ni kwa vile anaipenda CCM sana kuliko raia wa kawaida masikini ( angeanzisha SACCOS ya machinga) au alikuwa anawekeza kiaina katika chama kongwe hapa nchini. Aambiwe kwamba " he can fool some people sometimes but not all the people all the time". Aambiwe vile vile kwamba " No situation is permanent except change". Indeed "change" is coming.
 
.... mwaka uliopita tulikuwa tunaongelea neno FISADI... mwaka huu mambo yameongezeka zaidi, lazima ufafanue... FISADI gani? PAPA au NYANGUMI... nakumbuka Mzee Lipumba naye alikuwa ana wale wa kwake anawaita FISADI DAGAAA... Kiswahili kinaendelea kukua.
 
.... mwaka uliopita tulikuwa tunaongelea nene FISADI... mwaka huu mambo yameongezeka zaidi, lazima ufafanue... FISADI gani? PAPA au NYANGUMI... nakumbuka Mzee Lipumba naye alikuwa ana wale wa kwake anawaita FISADI DAGAAA... Kiswahili kinaendelea kukua.

Ni kweli, na lina noga hasa linapotumika kwa muhusika zaidi, aka Fisadi papa ROSTAMU AZIZI! kiranja wa mfisadi Tanzania (CCM)
 
anaesema mengi si fisadi ana ushahidi wa kutosha. anaesema rostamu ni fisadi pia ana ushahidi wa kutosha. mimi nasema hv hawa wawili WOTE NI WEZI tofauti ni staili wanazotumia kuiba,mlioko nyumbani kataeni kugeuzwa kama chapati kwenye kikaango.

Edson u have raised a very good point lakini jinsi ulivyomalizia- yaan wakatae kugeuzwa kama chapati?yaani unamaanisha kwa sasa wanageuzwa? lugha hii tamu kwel kweli
 
Duh! press com kibao!, haya sasa waandishi wachumia tumbo, hiki ndio kipindi cha mavuno na kitadumu mpaka October, 2010.
How true.I was just thinking the same when I landed on this page.Its like we were there at the same time.
 
Hizi Press Conferences zimekuwa sasa kama ndio platforms za kuanikana, kurushiana vijembe na kuumbuana.

Lakini ni afadhali sasa mambo yamekuwa mazuri kwa waandishi wa habari wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom