Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Nimelitafakari sana hili, na nimegundua kwamba tangu kuapishwa kwa JK mwezi uliyopita, Watz wamekuwa wanaonja machungu tu: Mgao wa umeme na maji, habari za kupanda bei za umeme, ongezeko la bei ya mafuta, ongezeko la bei ya bidhaa mbali mbali, wanafunzi wa vyuo kuandamana kudai haki/posho zao, uharamia katika chaguzi za mameya wa halmashauri .
Listi ni ndefu mno, na mwanzo ndiyo huonyesha ishara ya tunakokwenda. Ni bora wananchi wakasahau kabisa uwezekano wa hata kutimiza asilimia 0.000001 ya ahadi lukuki alizotoa JK wakati wa kampeni iwapo mwanzo ni wa namna hii.
Nasikia yeye yuko majuu kwenye matanuzi.