Tangazo Maalum: Mradi wa Kazi Majuu!

Status
Not open for further replies.
Wakuu kule Nigeria kuna kitu kinaitwa section 419..sijui kama mmeshawahi kukisikia?


Wakuu kautafiti kidogo tu google kananiletea info hizi, jana niliwaambia kuhusu section 419 kule Nigeria na hapanarudia tena.

Nilicgofanya ni kukopy sehemu ya info alotoa mkulu FMES hapo juu, actually paragraph ya kwanza tu, na jibu la kwanza google ndo hiyo website http://419.bittenus.com/eageap/


Applicants will have their entry visas processed in their country of choice for employment and housing resettlement program. All entry for VISAS will be applied through the respective government right channels for the visa depending on the system of government been operated by the country an applicant is applying to relocate.


sasa ukichunguza kwa makini hiyo website ina mapungufu mengi ambayo kwa credible organisation isingekuwa nayo.

website jina lake yenyewe utata,

Angalia picha za wenyewe zilivo kisha right click uangalie properties baadhi yake zina majina tofauti na jina la kwenye picha!

Angalia emails..za yahoo na gmail!

address za hongkong, na namba za simu walizotoa ukichunguza country code ni sawa ila zinazofuata ni fake,

Sijui tunaelekea wapi lakini sikutemea kama hili lingeweza kuletwa hapa JF, au kwa vile sasa hivi kuna wanachama zaidi ya 12,000 ukiacha wapiga chabo?
 
mimi kwanza nilistushwa neno lilotumika kwenye post "(MRADI) wa kazi majuu" na sio "nafasi za kazi majuu".kwahio neno (MRADI) inafanya hili swala biashara sio msaada wa kupunguza ajira kwenye nchi maskini.sema ndio hivyo huwezi kujua kitu bila kujaribu kama mtu unaweza kurisk $300 sio mbaya kwani kuna kukosa na kupata na nivizuri mtu ukajaribu labda wewe ndio utakuwa mfano kwamba hii system inafanya kazi. good luck everybody .
 
- Kwa wale wote niliowatumia info, mkipitia kwa makini web ya hawa jamaa utaona kuna mahali wamesema wazi kwamba kama una maswali kabla ya anything, tumia e-mail wameiweka chini kati ya hizo mbili moja ni web yao na nyingine ni e-mail tu zao, au tumia fax waliyoiweka hapo, kuwatumia maswali yako.

- Kabla hujafanya anything, please tumia huo wasaa kuwajua vizuri, na kwa wale watakaofikia kutaka ku-move forward tafadhali mnifahamishe ili mnipe info za kuweza kumpatia huyu sister aweze kufuatilia fomu zenu kwa karibu, maelezo yote yako wazi na very clear, kama huyaelewi please uliza anayeweza kukusaidia, huko kuna masharti ya kutimizwa kwanza, hakikisha unayatimiza kama maelezo yanavyosema.

- Hizi kelele za mlango za mwenye shibe, anayejibadili badili na ID zake lukuki humu ndani zisiwasumbue sisi kabla ya kwenda kupanda meli enzi zetu tulikutana sana na watu kama huyu, wanaolimbuka na shibe kidogo tu, wakijifanya bongo ni baabu kubwa sana mnakimbilia nini huko Ulaya!, siku hizi yote yako juu ya mawe, lakini tuliweka pamba kwenye masikio, hii sio process ndogo na rahisi rahisi, iwapo utayasoma vizuri maelezo yao utaelewa ninachosema, watu wenye record mbaya hasa criminal walikotoka hawatakiwi, meaning kwamba kuna sometype ya venting process through ubalozi wao bongo,

- Naomba sieme wazi kwamba, ninaamini kati ya watu 10 wa kwanza watakaojaribu, angalau watatu au wanne wata go through ninaamini that kwa 100%, watatu watashindwa kuelewa maelezo na kuishia kujiharibia wenyewe, na wengine waliobaki hawatakuwa na hela zinazotakiwa, ndio maana seriously nimeamua kuanza na watu wangu wa karibu sana watatu, ambao nitawasimamia mwenyewe, ndugu mmoja na washikaji wawili.

Respect and Later!

FMEs!
 
du wajinga ndo waliwao!hahaha FM Mwambie huyo mzungu hawezi kuiiba faranga kirahisi namna hiyo.
 
Nadhani ni utapeli wa kiusomi,

hapa ni kuwa hata wewe Fm unaweza kutapeliwa kwa kudanganywa ili usadie kutapeli wengine.

kazi ya kwanza kutoa fedha inatia mashaka,haifai
 
Nadhani ni utapeli wa kiusomi,

hapa ni kuwa hata wewe Fm unaweza kutapeliwa kwa kudanganywa ili usadie kutapeli wengine.

kazi ya kwanza kutoa fedha inatia mashaka,haifai

- Mkulu Rutunga unapoteza muda bure ndugu yangu, hapa in me una-deal na baharia, tena longtime baharia kabla sijapanda meli nimekutana na watu kama wewe wengi sana, ambao ningewasikiliza nisingepanda meli na kuwa na maisha niliyonayo leo, walisema unaenda Europe kwa nani? Hivi hizo meli wao wazungu hawazitaki ila zimekusubiri wewe tu utoke Africa? Utakaa kwa nani wakati unatafuta hiyo meli? Hivi unakujua Europe wewe au unakusikia? uliza mtoto wa flani alivyosota mpaka akarudi mwenyewe! Yule mwingine wametupa kwenye bahari! na blah! blah! blah! kama hizi zako,

- Omba barua ya information nikupatie, inakupeleka kwenye web yao na ifno zao zote ziko wazi, mpaka address ya HQ yao, cha kufanya ni kutuma mtu unayemjua aliye karibu na hupo mji, au kufuatilia mwenyewe kama kweli wapo hapo, wamesema wazi kwamba kabla hata hujajiingiza nao watuime ujumbe wa E-mail kuwajuza uwajue vizuri, siamini kwamba unaweza kufanya this thing in one weeek au one day, hebu soma maelezo niliyoweka pale nyuma, kuna a lot of paper work need to be done,

- Kwamba aliyeni-introduce in this thing ana nia mbaya, hapana labda wewe ndiye mwenye nia mbaya, kwa sababu mwenye nia njema angepitia the whole thing kwanza na kupitia all the facts, kabla ya kutoa conclusion kama zako, mimi sioni ajabu kuwepo kwa kitu kama hiki kwa sababu siku zote wafilipino hingia melini kwa njia hii, wao huletwa na mashirika mbali mbali ya dunia ya aina hii ambayo serikali yao huwa ina-deal nayo one on one, infact mpaka huko International Community, kuna vitu kama hivi ambavyo wananchi wa mataifa mbali mbali huwa wanaruhusiwa kuhamia US, UK, na Canada throuh wao yaani kama UN, UNESCO N.K kwa kushirkiana na serikali mbali mbali, lakini siis bongo kwa sababu ya roho mbaya zetu huwa hatuzikisikii wala hata kujua kuwa zipo, ingawa kuna wachache wanaojua na huwa wanapitisha ndugu zao tu tena kwa siri sana,

- Again ninasema hivi kwa kuanza nitaanza na ndugu yangu mmoja na washikaji wangu wawili mabaharia ambao wako juu ya mawe, otherwise mkuu kama unataka kushiriki naomba uufuatilie, itakapofikia malipo mimi nitakutolea, unajua kutoa sio utajiri kama unavyofikiri, kuhusu hii deal ninasema kwamba ninaamini kwa 100% kwamba ipo, lakini kuingia sio rahisi kama inavyoonekana, na ni kwa mara ya kwanza nimegundua kwamba ni njia hii ndiyo imempeleka mshikaji wangu mmoja majuu, maana aliwahi kuishi majuu akarudi bongo, akachacha sana lakini akaenda na kujikita kwenye kambi ya refugee Ngara, in one month akahamia majuu yeye na watoto wake, akapewa nyumba na kazi, kila nilipojaribu kumdadisi amerudije majuu, anakwepa kuniambia na kunipa haidthi ambazo hazijai kwenye mkono, jana nimemtwangia na kumpa wazi kwamba finally nimegundua alirudije majuu, ameishia kucheka sana,

Rutunga, ninamuaminia kwa 100% huyu sister wa kizungu aliyenipa hizi info, sina sababu hata moja ya ku-question nia yake, kwa sababu hana sababu hata moja ya kunidanganya, angekua na njaaa ningeelewa, nisiyemuamini hapa ni mtu kama wewe ambaye nia yako sio siri kuwa ni mbaya tena sana, sasa nakupa offer jaza fomu, mimi nitakulipia hizo hela unazolilia sana, na kwa taarifa yako ni kwamba nimekuwa nikiwasidia wananchi wengi sana humu nje ya forums na sijawadai senti hata moja maana wizi, utapeli, na tamaa tamaa ni tabia ya kuzaliwa nazo, mimi sina hizo mkuu.

- Kwa wakulu wengine nimeupata ujumbe huku pm na e-mail na soon nitawatumia hizi info na details zake.

REspect.

FMEs!
 

"The international ........ and other charity organizations arrange transportation to US, UK.and Canada on loan basis for us on behalf of the applicants or the group’s trip. Refugees and successful applicants are expected to repay the cost of their transportation after they settled down in their new resident countries."

- Maneno kama haya yananifanya niamini kwamba this thing is for real!

Respect.

FMEs!
 
hata nami naungana na Yo Yo, niorodheshe ... watanikata hizo $ 300 kwenye mshahara wangu

Naomba kuunga mkono hoja; wakukate hapa hapa; ukitoa dola 300 then usipate hata hiyo kazi nani atairudisha; tusije tukaanza ujanja ujanja hapa; nakumbuka nilishaona watu fulani ambao kazi yao ni kufuatilia agency zinazotoa scholarshipa na info za kazi hizo ndizo zimekuwa k=zikileta shida; badala ya ktu kupewa haki yake bila kujali ana dola mia tatu au la sasa watu wanalipia inof ambayo kimsingi ni haki yake kupata habari hiyo;

Nataka nipate link mkuu ya hao matajiri sio kupitia gateway yenye kiwango kama hicho mkuu
 
- Mkulu Masa ukishaibiwa hiyo hela yako nitafute mimi FMES, nitakurudishia mkono uliokupa wewe ndio huo huo uliowanyima ninaojaribu kuwasaidia, huna facst zaidi ya filimbi, vipi kule kwa George Mwakalinga yamekushinda?

- Unaukumbuka wimbo wa Remmy kwamba "....usicheke cheke kwa sababu leo umeshiba kumbuka kesho matumbo yatawasha......",

Waache wenye shida wajaribu kuliko kuingilia njia ya msaada wa Mungu kwa watu wake, utaumia mkuu vipi kwenu hakuna mifano ya waliomkufuru Mungu kwa kucheka msaada wa Mungu kwa masikini kama unavyofanya hapo juu?

Respect.

FMEs!

Tumekwisha! Sasa kama na mzee FMES unaamini kwenye hivi vitu, sijui nani atabaki nji hii. Sitaki kuamini kwamba kuna watu huku watatuma kweli hizo $300 zao. Na ninakataa kabisa akili yangu kuamini kwamba hizo messages zinatoka kwa FMES. Maani nikikubali kuamini kwamba haya yanatokea, naweza kuanguka kwa kihoro.

Yaani hapa nasikia kucheka huku nasikia kulia.

Chonde chonde FMES. Futa tu angalau hiyo guarantee yako ya kuwarudishia watu pesa zao. Chonde chonde. Inaweza kuku-cost kaka. Hayo maneno unayosema yanakufanya uamini wameyaweka hapo makusudi, wanajua kuna watu kama wewe watayahitaji ili waamini.

Inanikumbusha profesa mmoja UDSM alipoingizwa mjini baada ya kupewa dili ya kuuza sea shells nje. Kuja kustuka ashapoteza mamilioni ya pesa, madeni kibao, huku wife akiwa lupango kwa sababu "alikopa" pesa za mishahara ya watu akijua ataweza kuzirudisha dili likikamilika. Prof wa watu ashatuma kontena la sea shells, badala ya kupokea fedha, eti yeye ndio anazituma sasa. Yaani wewe ndio unauza mali alafu ndiye unayetuma pesa. Hiyo hata abunuasi hakuwahi kuweza kuifanya. Ni kama sinema hivi. Na hata akiambiwa haelewi kabisa na majibu aliyokuwa akitoa akiulizwa hayana tofauti sana na anayotoa muheshimiwa hapa. Yaani hawa matapeli sijui wanawavutisha nini victims wao.

Some Links:
http://www.fraudwatchers.org/forums/archive/index.php/t-5335.html
http://www.fraudwatchers.org/forums/archive/index.php/t-3374.html
 
Hawa wanahitaji msaada maana walitoa thanks kwenye post ya namna hii ......Mungu baba awaepushe na balaa hili, FMES please stop this messy!

Mzee Masa

Mzee Masa na wengine walio pessimistic na hii kitu,...

NADHANI kuna kitu kimoja unabidi muwe waangalifu kidogo. Inawezekana kweli hili deal likawa fake. Inawezekana FMES na yeye akawa amedanganywa......Lakini umeshajihangaisha kuutafuta ukweli zaidi ya hizi stereotypes tulizozizoea? za wanaijeria? Ofcourse deal kama hizi ni vyema mtu uwe makini lakini nadhani hatuna budi vile vile kuwa inquisitive. Mpaka sasa naamini Mzee FMES hana njaa ya kumuibia kapuku kama Masanja $$300. Harafu this guy is real kwa sababu anakwambia umuandikie akupe maelekezo..sasa nadhani mtu yeyote mwenye NIA YA KUUJUA UKWELI ingebidi ayapate hayo maelekezo..aulize maswali..ndo aje hapa kwenye thread atoe ushauri kwamba watu watoe hiyo pesa au wasitoe kutokana na maelezo aliyopewa na bwan FMES... Labda uniambie kama umewasiliana na huyu jamaa FMES ukatafuta sources zako..ukaona ni utapeli.

Othwerwise, waacheni wanaohangaika wahangaike..huwezi jua..maana unaweza mkatisha tamaa mtu kwa kitu ambacho ni cha kweli. Mimi naamini wote humu ni watu wazima..tunajua namna ya kuhangaika..unafikiri hata aliyepeleka hela DECI hakujua? kama alivyosema SHAPU kuna waliofaidi DECI mpaka leo huwezi kumwambia ubaya wa DECI....

Mi nadhani ni kuwekana sawa tuu kwa vitu kama hivi..its all about kusaidiana. Do your research and then come here and tell us your kapriensi..

Ni hayo tuu,

Masanja,
 
Hawa wanahitaji msaada maana walitoa thanks kwenye post ya namna hii ......Mungu baba awaepushe na balaa hili, FMES please stop this messy!

Mzee Masa

Mkuu uliangalia tu thanks au pia michango ya waliotoa thanks, LOL! Angalia what I have been saying onthis thread kisha u relate thanks na hiyo shida ya kazi. Unajua posts kama hizi wakatio mwingine zinaelimisha hata wale ambao walikuwa hawajui uwepo wa hawa wahuni wa 419.
 
Inawezekana habari hizi zinaweza kuwa na ukweli wake ingawa unakuwa na wasiwasi maana kuna watu kibao huko Magharibi hawana kazi kwa nini watafute kutoka Afrika? Lakini kwa upande mwingine wanaweza kuwa wanaangalia cheap labour.
Kuhusu kufanya na Immigration, nakumbuka kipindi fulani Congress ya Marekani waliweka Brakes kwenye H1B visa kutokana na mtikisiko wa uchumi. Sasa sijui kama brake zilishaondolewa au la.

Hata hivyo siamini kama Mkuu FMEs anaweza kuacha mtanzania mwenzake anatapeliwa huku akijua ukweli........
 
FMEs
Natambua na kuheshimu sana mchango wako kwa watanzania kupitia michango yako katika JF, lakini kwa hili naomba ukubali kuwa ni utapeli. Yawezekana dhamira yako binafsi ni nzuri lakini matapeli wanataka kupitia mgongoni mwako au mgongoni mwa huyo unayesema ni rafiki yako. Pengine wa -nigeria wame-hijack email yake(huyo dada rafiki yako) na kuanza kuitumia kwa faida yao. Nashauri watanzania wenzangu msiichangamkie hili deal na kama nchi husika mnaijua tafadhalini sana ulizieni ukweli wa taarifa zake kupitia ubalozi wa tanzania katika nchi hiyo au iliyo karibu na nchi husika. FMEs kubali kwamba hata wewe unaweza kutapeliwa na sikia ushauri wa wengi-sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Ukiendelea kung'ang'ania hii deal unaweza kufikirika kuwa nawe ni sehemu yake. Sipendi nishawishike hivyo. Kwa common sense ya kawaida, hii deal imekaa kitapeli.
 
FMEs
Natambua na kuheshimu sana mchango wako kwa watanzania kupitia michango yako katika JF, lakini kwa hili naomba ukubali kuwa ni utapeli. Yawezekana dhamira yako binafsi ni nzuri lakini matapeli wanataka kupitia mgongoni mwako au mgongoni mwa huyo unayesema ni rafiki yako. Pengine wa -nigeria wame-hijack email yake(huyo dada rafiki yako) na kuanza kuitumia kwa faida yao. Nashauri watanzania wenzangu msiichangamkie hili deal na kama nchi husika mnaijua tafadhalini sana ulizieni ukweli wa taarifa zake kupitia ubalozi wa tanzania katika nchi hiyo au iliyo karibu na nchi husika. FMEs kubali kwamba hata wewe unaweza kutapeliwa na sikia ushauri wa wengi-sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Ukiendelea kung'ang'ania hii deal unaweza kufikirika kuwa nawe ni sehemu yake. Sipendi nishawishike hivyo. Kwa common sense ya kawaida, hii deal imekaa kitapeli.


Muungwana Reasoning, hivi kweli umereason? MAANA ni maneno kama haya uliyoandika ambayo ni dangerous. Yaani hapa umeandika hisia tuu.

Mkuu, hiki kitu kiko wazi..umemwandikia FMES na kumuuliza? People get real jamani! Its only through this guy you can verify the information given. Maana yeye ndo kaileta hii habari.

Ushauri: Kila binadamu ana hangaika kivyake na ana bahati yake. pata information ichambue then fanya maamuzi.

Ukweli na uongo utajulikana. Kwa nini useme kwamba kitu ni uongo wakati hujaongea na prime mover? muhusika mwenyewe?

Masanja
 
internet is fairly new in Tanzania and it is our responsibility to educate and protect the vulnerable part from failing into it's shortcomings.
my only Inquiry is make it public for the Mass to see.if it is genuine no one will argue against that.and if it's fake then someone knowledgeable will let others know.
keeping it in PM's Loops only increase the chances of backstabbing to those vulnerable ones.

transparency,that's all that is needed.
 
craigs_list_foundation.jpg
 
- Hao juu ndio wahusika wa hii charity/organization, sasa shika picha zao kabisa wakileta za kuleta angalau una pa kuanzia. Kwamba eti mimi sijui utapeli, think again nilipozaliwa na kukulia na watu niliokua nao, au kama hujui uliza kabla hujasema sema.

- Kwa wale mnaonitafuta na maneno mengi sana, samahani sasa sina huo muda wa kulumbana, ninawasiliana na wananchi wengi sana waliojitokeza toka bongo, yaani wenye shida kweli, kesho usiku nitaruka kwenda kujionea mwenyewe the whole story,

- ila one thing maelezo zaidi sina tena, nimemaliza na kama nilivyosema, nimeamua kuanza na kumsaidia ndugu yangu mwenyewe ambaye nitamlipia, na washikaji wawili wengine.

Respect and See yah!

FMEs!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom