Tangazo la Wizara ya Nishati ni kichekesho

Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
413
Nimelisoma tangazo la Wizara ya Nishati na Madini kuhusu kile kilichodaiwa kwamba Ngeleja amemkana Jairo na kilichojitokeza pale kikanikumbusha ule usemi wa kimombo usemao kwamba a fool who is quiet is considered wise. Taarifa hiyo imejaribu kukanusha na kufafanua kukosekana kwa Ngeleja bungeni na kuonekana kwake katika mapokezi ya Katibu Mkuu aliyesimamishwa (David Jairo).

Tangazo limetetea kwamba Ngeleja alikuja Dar kuhudhuria mikutano ya masuala ya umeme na masuala ya mafuta. Hata hivyo hakuna maelezo ya kwa nini alihusika na mapokezi hayo na kwa nini ilikuwa lazima waandishi wachukue tukio hilo na kuacha yale ya msingi yaliyomleta ambayo hata hivyo hayakutangazwa wala kuonyeshwa.

Je, isingewezekana wakakutana ofisini kwa waziri kimya kimya kama wanavyofanya siku zote. Waandishi wale waliitwa na nani na walijuaje kwamba waziri alikuwa anasubiri ili awepo kwenye tukio hilo? Na vipi wale wafanyakazi walioacha kazi za ujenzi wa taifa na kujihusisha na kazi hiyo ambayo haina taji kwa taifa na mwajiri wao.

Kwa ujumla tangazo hilo limeacha maswali mengi kuliko majibu na unajiuliza iwapo ilikuwa ni lazima tangazo hilo litolewe. Kwangu mimi, hakuna ambacho tangazo hilo imefanikiwa kukipata zaidi ya kupoteza fedha za walipa kodi maskini wa nchi hii.

 
Usanii mtupu!!

Jamaa wamekumbatiana zero-distance ili wapigwe picha halafu wanazuga kuwa hakuja Dar kwa ajili ya Kumpokea J-Ro! Ila pia nahisi Vasco-da Gama ana mpango wa kumpa J-Ro ubalozi, Tusubiri tuone!!
 
Ngeleja usanii wake na uchakaramu wake utamponza anaonekana na anajifanya.....kuwa waziri mchangamfu anajiona kama ameshafuzu kuongoza wizara kumbe sio kweli anajifanya yeye ni mc wa kila jambo bungeni na nje ya bunge kwa wabunge wenzake!!!
 
ukidanganywa na ccm basi we shosti bwabwa
hahahahaaa!
Shosti halafu bwabwa! Yani hata ukibadili piston rings zote, sleeves, ukichonga block, ukibadili timing beld, ukiweka cranck shaft mpya, bado....bado kitu inalia Nock Nock....yani ccm is a rotten bedford!
 
Ningekuwa ngereja nisingekubli kuwa part of that mapokezi, that was simply crap
 
Mi nafkir Vasco daGama alichemka kumstop J-iro peke yke,alipaswa kuagiza wote waloshrk mapokez na kuacha majukumu ya msingi wawajibishwe mara moja,lakini pia hyo ngeleja anapaswa kutupwa nje ya ofc now as toka amekuwa wzr hana la kujivunia alilolifaoya zaid ya usanii mtupu.
 
Yani ndio viongozi wetu tuliowachagua watuwakilishe na kusimamia mambo mazito ya nchi yetu pamoja na asilimali zetu tulizojaliwa.
 
For Ngereja that was a wrong move, hata kama alijua kuwa J-RO alimfichia siri kuwa na yeye anajua kuhusu ule waraka alitakiwa kutojiusisha mpaka apate uhakika kuwa mkuu wa kaya aliruhusu hatua ya J-RO kurudishwa job.

Lakini pia JK amefanya wrong move, kama aliona umuhimu wa kumsimamisha tena then Ngereja na Luhanjo walitakiwa kumpa company mwenzao

Mr. President need to be serious with his assistants, wanamsubortage na yeye hajui.
 
Ngeleja alitamani sana kulisukuma gari la Jah-hero sema aliogopa macho ya watu!
Shame on you Nge.le.ja
 
hahahahaaa!
Shosti halafu bwabwa! Yani hata ukibadili piston rings zote, sleeves, ukichonga block, ukibadili timing beld, ukiweka cranck shaft mpya, bado....bado kitu inalia Nock Nock....yani ccm is a rotten bedford!
Bedford!!!!!!! Hahahahha hahahhahaa kweli ccm imekongolloka
 
Mkuu wote waziri na Rais pia walijua taarifa hiyo y Jairooo kurejea kazini.Sasa kilichotokea bungeni ndo kimeichanganya serikali na rais mwenyewe.Je ulize yote haya akuna mawasiliano ikulu na wizara zake?
 
Back
Top Bottom