Tangazo la msiba wa wilbert matoka

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,568
2,910
Ninasikitika kuwatangazia ndugu jamaa na marafiki kuwa kaka yetu mpendwa Wibert Matoka hatuko naye tena Duniani. Amefariki leo hii 31/08/2008 Dar es salaam katika Hospital ya regent. Alikuwa anasumbuliwa na kutokwa damu puani bila kukoma.
Brother Wilbert Matoka mpaka mauti yalipomkuta alikuwa ni lecturer kule Iringa chuo kikuu cha Mkwawa. MUCHE.
Wilbert alisoma shule za ryamisanga na Masurura Musoma kabla ya kujiunga na masomo ya sekondari Nsumba Mwanza 1972-1975. Baadaye alijiunga na cHuo cha Ualimu cha Taofa Butimba. alihitimu kama mwalimu mwaka 1977 na kupangiwa kwenda Mtwara wilayani Newala. Alifundisha huko miaka kadhaa kabla hajarejea tena butimba na Chang'ombe kusomea Diploma ya Ualimu. Baada ya kuhitimu alifundisha kwa muda chuo cha UALIMU Chang'ombe kabla ya kujiunga na Chuo kikuu cha Dar es salaam kusomea BED in Physical education. Alipohitimu 2000 alendelea ma MA IN education hapohapo mlimani. na alipohitimu alijiriwa kama mhadhiri chuo kikuu cha MUCHE.

Mwalimu kama alivyojulikana sana alikuwa ni mwana michezo hodari. alimudu kucheza na kuwa coach wa michezo kadhaa. wnamichezo wengi wanamjua kuanzia kule umisavuta n.k

Wibert ameacha Mjane Sofia. Vijana wawili Chacha Matoka anayesoma pale kijitinyama ustawi wa jamii(HRM) Warioba Matoka LLB Mlimani na Wegesa Matoka A level sangu secondary school.

Mwili wa marahemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda kijijini Masurura Musoma kwa mazishi.
View attachment 2197
 

Attachments

  • mwalimu 2.jpg
    mwalimu 2.jpg
    58 KB · Views: 135
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape faraja ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu katika kipindi hiki kigumu kwao cha kuondokewa na kipenzi chao~AMEN.
 
Mungu amlaze malaha pema. Pole ziwaendee wanafamilia, ndugu na jamaa wa Karibu na Mungu awape uvumilivu kwenye wakati huu mgumu.
 
Raha ya milele umpe ee Bwana na Mwanga wa milele umwangazie, Apumzike kwa Amani AMEN.
Poleni ndugu,jamaa,marafiki na wote mliofikwa na msiba huu.
 
Bwana ametoa. Bwana amechukua. Aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi na awafariji aliowaacha.
 
Tupo wote katika kipindi hiki kigumu, Mungu awajaze faraja na muwe na subiri. 'Amen'
 
May the Almighty God rest his soul in eternal peace. Amen
praise be to God. Halleluyah!!!
 
Poleni kwa msiba, Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
 
Sometimes you see a face you say hello and go your way. Sometimes you discuss politics with this face in a group and not even ask about their name. You do not give it a thought.
Poleni sana wafiwa. May God grant you strength and wisdom during these trying times. I never knew the story behind this face but now I understand for one he worked hard to improve life for him and his family. Aisee, Poleni sana. God be with you all in these trying times. Poleni sana
 
Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi ambaye alimuumba Wibert Matoka, hatimaye imempendeza amemrudisha kwake.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe (Ayubu 1:21). Amen
Poleni sana kwa msiba huu ndugu wote wahusika.
Mungu Mwenyezi, Muumba wa Mbingu na Nchi awape uvumilivu na kutukumbusha wote kuwa hapa duniani ni mahali pa kupita.
 
Poleni sana maana mwenyewezi mungu alisema kwamba mnakwenda kutembea na kurudi so tunamuombea ailaze roho yake mahali pema peponi
 
Mungu ailaze mahali pema peponi Roho ya Marehemu. Pole sana kwa wanafamilia. Hii ni njia yetu sote na tukae tukijua kuwa kila mtu ana siku yake ila hatujui siku wala saa bali tujiandae kwa kuwa waadilifu na kuishi kwa utakatifu siku zote. Amen
 
Poleni wote mliofikwa na kuguswa na msiba huu, Mungu awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom