Tangazo hili la maralia

Gamaha

JF-Expert Member
Jul 17, 2008
3,815
4,861
kuna tangazo la maralia linarushwa na vituo mbalimbali vya TV, lengo ni kuhamasisha watanzania kutumia vyandarua. lakini kwa nini wameweka hili tangazo kwa kingereza kwa nini wasitumie kiswahili ili lieleweke vizuri na watu wote na si wasomi tu wanaojua kingereza.

Au kwa sababu pesa za kutoa tangazo zimetoka kwa wafadhili wameshinikiza watumie lugha yao, mi naona ni upuuzi bora wasingetoa hilo tangazo kwa sababu watu wengi wasio na elimu ndio hawajui umuhimu wa kutumia vyandarua, na ndio hao hawaelewi pia hili tangazo. Tanzania yangu inanikela saa nyingine jamani
 
Wazungu wanaanza kukutawala tena kupitia utandawazi,si unasikia kibwagizo cha Tangazo hili ni "kwa hisani ya watu wa marekani" ,Miafrika ndivyo tulivyo
 
Wafadhili hao hawana muda kusikia hayo matangazo hawajui hata local TV zetu, shida ni watz kujipendekeza kwa wazungu- rejea matukio kibao - hapohapo mzungu anaongea kiswahili viongozi wetu wanatumia kiingereza.

Hivi kwanini wafadhili hawa; mfano kuna nchi moja inapenda sana kufadhili miradi ya kupanga uzazi wa mpango ( ki ukweli kupunguza watoto) na inasisitiza sana matumizi ya kondomu sio kuzuia ukimwi ila kupanga uzazi lakini ni nchi hiyo hiyo iko mstari wa mbele kufadhili vyandarua watanzania wasife na ugonjwa wa malaria ambao unaweza kuwa unaongoza kwa vifo vingi. Sasa najiuliza si ingeacha kufadhili vyandarua ili watu wengi wafe kwa malaria na hivyo wapungue kabisa.

Baadaye nikasema labda wanatufunika blanketi tuaamini kuwa vyandarua vinasaidia kupunguza malaria wakati ukweli vifo viko pale pale, kutokana na ufadhili wa vyandarua ambao ni mkubwa sana macho yetu yamefungwa kabisa kuaangalia njia nyingine za kutokomeza malaria. Kila siku ni vyandarua vyandarua tu-huku watu wakiendelea kufa na kuugua malaria sugu na hatimaye kuwafanya baadhi ya watanzania akili zao kuwa na mushkeli.
 
Si wafadhili, ni ujinga wetu. Wafadhili wengine wanajua kwa sehemu kiingereza.
Uliwahi kujiuliza ni kwa nini ukiondoa ccm na chadema vyama vingi vilivyo na usajili wa kudumu majina yake ni ya kiingereza? Unajua kirefu cha NCCR? na hapo tuwalaumu wafadhili?
 
Hii yote inatokana na ujinga wetu wa kuwanyenyekea wageni na lugha zao!
 
Back
Top Bottom