Tangazo: Bash la Balozi NYC Haya Tukutane Wakuu!

- Anyways, matayarisho ya sherehe yanaendelea, tena kwa kasi ya ajabu sana naona tutakutana tu huko, ila tu msisahau kuleta watoto, si unajua ndio taifa la kesho.

Ahsanteni.

William.
 
Just look for the dude with the politically incorrectly dressed chick in the Balenciaga, making all washua go "hmmmmmmh"?
 
heshima mbele wakuu.mimi napenda sana kuona watu wakikutana pamoja kwenye nchi za watu kama hizi party zinavyofanywa na huwa ni nyingi mno.sasa kwa vile ni nchi za nje na wengi wenu mnajiweza kidogo mara nyingi nimeona party nyingi zinaishia kukutana na kula ,,kucheza, kunywa na kujuana tumemaliza.mimi ushauri wangu mdogo tu,kwanini mnapokutana kwenye hizi party msipitishe kimchango flani yani sio lazima kwa wale walikuwa nacho chochote wachangie na huo mchango mue mnasaidia labda kwenye mahospitali nyumbani,au mashule ambayo hayana madawati na kadhalika.nadhani kama mkijaribu kufanya hivi mtakuta kwamba hizi party zina umuhimu mkubwa kuliko watu wanavyofikiria kwani mtakuwa wakati huo huo mnasaidia jamii nyumbani.ni wazo tu wakuu na nawatakia party njema.
 
heshima mbele wakuu.mimi napenda sana kuona watu wakikutana pamoja kwenye nchi za watu kama hizi party zinavyofanywa na huwa ni nyingi mno.sasa kwa vile ni nchi za nje na wengi wenu mnajiweza kidogo mara nyingi nimeona party nyingi zinaishia kukutana na kula ,,kucheza, kunywa na kujuana tumemaliza.
- Si kweli kwa sababu kuna ma-single kukutana kufahamiana mpaka kuishia kwenye ndoa, mifano ipo, kuna kusaidiana shule huenda shule yangu sio nzuri au malipo ni makubwa kuliko ya mwananchi mwenzangu hapa ninapata nafasi ya kubadilisha shule, mifano ipo, huenda kazi ninayofanya hailipi kama ya mwananchi mwenzangu ninahama kazi na kwenda kwenye malipo zaidi na mifano ipo, huenda sisi ni ndugu tumepoteana siku nyingi tunakutana na kuendeleza undugu na mifano ipo, huenda ninapoishi kuna wa-Tanzania wenzangu lakini sijui kama wapo tunakuatana kwenye hizi party na kufahamiana na majirani na mifano ipo, watoto wadogo kukutana na kufahamiana na mifano ipo.

- Halafu kumbuka kwamba huwa pia tunakutana wakati wa shida, sio sherehe tu kwa hiyo again mkuu bado unajaribu kulazimisha hoja, lakini uko out of the line na the spirit ya hizi sherehe.

mimi ushauri wangu mdogo tu,kwanini mnapokutana kwenye hizi party msipitishe kimchango flani yani sio lazima kwa wale walikuwa nacho chochote wachangie na huo mchango mue mnasaidia labda kwenye mahospitali nyumbani,au mashule ambayo hayana madawati na kadhalika.nadhani kama mkijaribu kufanya hivi mtakuta kwamba hizi party zina umuhimu mkubwa kuliko watu wanavyofikiria kwani mtakuwa wakati huo huo mnasaidia jamii nyumbani.ni wazo tu wakuu na nawatakia party njema.
- Mkuu wananchi wanapotaka kuchanga kusaidia jamii popote pale, inatakiwa iandaliwe kama Fund Raiser, lakini huwezi wananchi wanajaribu kustarehe kwa kutumia michango yao, ukaanza kupitisha bakuli eti kwa ajili ya shule za bongo, mkuu hapo kwenye party kuna watu kutoka sehemu ngapi za bongo?

- Je tutaanza kusaidia shule ya mwananchi gani na tutaacha ya mwananchi yupi? Kama wewe una shida ya kusaidia shule kwa njia ya party, basi tangaza party ya Fund Raiser useme na shule unayotaka kuisaidia, wananchi waje kwenye hiyo party wakijua wazi kwamba wanakuja kuchangia shule,

- Rais Mkapa, alipokuja kutuaga wananchi wa NYC kabla ya kuvua madaraka ya urais, alikuja na Rais wa sasa ambaye wakati huo alikuwa waziri wa nje na Rais mtarajiwa, katika ule mkutano pale Hermsely Hotel, akatokea bwana mmoja akamuuuliza Rais Mkapa, swali kama hili lako kwamba serikali ianzishe tabia ya kupokea michango toka kwa wananchi wa nje ili kusaidia kujenga bara bara ba kuweka umeme, lahaula la kwata Rais Kikwete akaomba kulijibu lile swali, nafikiri waliokuwepo wote wanakumbuka jinsi alivyotaka kushusha mbingu na majibu yake,

- Kwa kufupi tu alisema hivi, kama kweli mnazo hizo hela basi pelekeni msaidie vijijini kwenu na familia zenu kwa sababu serikali haihitaji hiyo michango ambayo haiwezi kumudu gharama za hata mti mmoja wa umeme, sasa mkuu mimi nikupe dola zangu mbili zikajengee shule kwenu, vipi kwetu? Kila kitu na wakati wake, kuna wakati wa kupanda na kuvuna, kuna wakati wa mvua na kiangazi, na pia kuna wakati wa sherehe na wakati wa Fund Raising, hatuwezi kuchanganya mambo,

- Point yako ni valid, lakini kama vile huko mwanzoni iko kwenye the wrong place, hapa sio mahali pake, anzisha mfuko maalum wa kusaidia shule Tanzania, na uweke ratiba za kuchangia uweke shule zote za Tanzania ambazo zitawakilisha wachangiaji wote, ninaomba uziache sherehe au party ziwe kama zilivyo yaani party za kusherehekea maisha ya wananchi kwa jasho lao. Hizi sherehe ni utamaduni ambao umekuwepo kwa miaka mingi sana, kila inapofika wakati wa Summer na mwisho wa mwaka na pia upo utamaduni wa kuchangiana wakati wa shida, au kusaidia jamii ndio maana meli ya MV. Bukoba ilipozama, tulikutana na kuchangia wananchi waliopona na tumewahi kufanya Fund Raising nyingi sana huko nyuma za namna hii na pia harusi za wananchi wenzetu, hizi tunafanya kila wakati sijasikia ukilalamika kama unavyolalamikia hii party, vipi kuna tatizo unashindwa kulisema wazi nini? maana haiwezekani ukawa hutaki tu kukubali mkuu sema tatizo lako badala ya kuendelea kuzunguka mbuyu, wote hapa ni watu wazima na tunajua namna ya kuchambua ishus betweeen the lines,

- Unaonekana una tatizo bigger than hii party kwa nini usiliseme tu mkuu, ukapatiwa majibu? Ila tu so far so good matayarisho yamepamba moto na wallahi hii party itakuwa ni kwa mtindo wa mdundo kama ule ambao ungetumika kwenye safari ya Tour ya mwisho ya MJ, yaani "This is it", kwa hiyo just see yah there!

Ahsante.

William.
 
Wananchi wote mnaoishi USA mnaalikwa nyama choma Nyumbani kwa Balozi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa anaefanya kazi na kuishi NY, USA, tarehe 15/08/ 2009. Kwa maelzo zaidi nenda Michuzi blog.
 
Last edited:
SMOKING BBQ
SAT AUG 15TH
30 Overhiil rd, Mt.Vernon NY10552
From 2pm
COME ONE COME ALL
[FONT=Courier New, courier, monaco, monospace, sans-serif] AFTER PARTY

MAO PRODUCTIONS & CLUB SERENGETI
[FONT=Courier New, courier, monaco, monospace, sans-serif] Spinning the best from Africa [/FONT]
[FONT=courier new, courier, mono][FONT=Comic Sans MS, sans-serif] @ THE ALAMO[/FONT][/FONT]
166 GRAMATAN AVENUE
MT. VERNON,NY 10550
ADMISSION : FREE
DIRECTIONS AND INFO (917)709 6889

[/FONT]
 
Ni balozi wa Tanzania UN. Kuna tofauti kubwa kati ya balozi wetu USA na balozi wetu UN. Rudi kwa Michuzi ukalisome tangazo tena, au vipi wasiliana na Kamanda William Malecela, bila shaka atakupa maelezo yote.
 
Nipo hapa sasa hivi. Nyama ya kuku ni tamu sana, mbuzi, na nk. Ni raha tupu.
 
- Si kweli kwa sababu kuna ma-single kukutana kufahamiana mpaka kuishia kwenye ndoa, mifano ipo, kuna kusaidiana shule huenda shule yangu sio nzuri au malipo ni makubwa kuliko ya mwananchi mwenzangu hapa ninapata nafasi ya kubadilisha shule, mifano ipo, huenda kazi ninayofanya hailipi kama ya mwananchi mwenzangu ninahama kazi na kwenda kwenye malipo zaidi na mifano ipo, huenda sisi ni ndugu tumepoteana siku nyingi tunakutana na kuendeleza undugu na mifano ipo, huenda ninapoishi kuna wa-Tanzania wenzangu lakini sijui kama wapo tunakuatana kwenye hizi party na kufahamiana na majirani na mifano ipo, watoto wadogo kukutana na kufahamiana na mifano ipo.

- Halafu kumbuka kwamba huwa pia tunakutana wakati wa shida, sio sherehe tu kwa hiyo again mkuu bado unajaribu kulazimisha hoja, lakini uko out of the line na the spirit ya hizi sherehe.

- Mkuu wananchi wanapotaka kuchanga kusaidia jamii popote pale, inatakiwa iandaliwe kama Fund Raiser, lakini huwezi wananchi wanajaribu kustarehe kwa kutumia michango yao, ukaanza kupitisha bakuli eti kwa ajili ya shule za bongo, mkuu hapo kwenye party kuna watu kutoka sehemu ngapi za bongo?

- Je tutaanza kusaidia shule ya mwananchi gani na tutaacha ya mwananchi yupi? Kama wewe una shida ya kusaidia shule kwa njia ya party, basi tangaza party ya Fund Raiser useme na shule unayotaka kuisaidia, wananchi waje kwenye hiyo party wakijua wazi kwamba wanakuja kuchangia shule,

- Rais Mkapa, alipokuja kutuaga wananchi wa NYC kabla ya kuvua madaraka ya urais, alikuja na Rais wa sasa ambaye wakati huo alikuwa waziri wa nje na Rais mtarajiwa, katika ule mkutano pale Hermsely Hotel, akatokea bwana mmoja akamuuuliza Rais Mkapa, swali kama hili lako kwamba serikali ianzishe tabia ya kupokea michango toka kwa wananchi wa nje ili kusaidia kujenga bara bara ba kuweka umeme, lahaula la kwata Rais Kikwete akaomba kulijibu lile swali, nafikiri waliokuwepo wote wanakumbuka jinsi alivyotaka kushusha mbingu na majibu yake,

- Kwa kufupi tu alisema hivi, kama kweli mnazo hizo hela basi pelekeni msaidie vijijini kwenu na familia zenu kwa sababu serikali haihitaji hiyo michango ambayo haiwezi kumudu gharama za hata mti mmoja wa umeme, sasa mkuu mimi nikupe dola zangu mbili zikajengee shule kwenu, vipi kwetu? Kila kitu na wakati wake, kuna wakati wa kupanda na kuvuna, kuna wakati wa mvua na kiangazi, na pia kuna wakati wa sherehe na wakati wa Fund Raising, hatuwezi kuchanganya mambo,

- Point yako ni valid, lakini kama vile huko mwanzoni iko kwenye the wrong place, hapa sio mahali pake, anzisha mfuko maalum wa kusaidia shule Tanzania, na uweke ratiba za kuchangia uweke shule zote za Tanzania ambazo zitawakilisha wachangiaji wote, ninaomba uziache sherehe au party ziwe kama zilivyo yaani party za kusherehekea maisha ya wananchi kwa jasho lao. Hizi sherehe ni utamaduni ambao umekuwepo kwa miaka mingi sana, kila inapofika wakati wa Summer na mwisho wa mwaka na pia upo utamaduni wa kuchangiana wakati wa shida, au kusaidia jamii ndio maana meli ya MV. Bukoba ilipozama, tulikutana na kuchangia wananchi waliopona na tumewahi kufanya Fund Raising nyingi sana huko nyuma za namna hii na pia harusi za wananchi wenzetu, hizi tunafanya kila wakati sijasikia ukilalamika kama unavyolalamikia hii party, vipi kuna tatizo unashindwa kulisema wazi nini? maana haiwezekani ukawa hutaki tu kukubali mkuu sema tatizo lako badala ya kuendelea kuzunguka mbuyu, wote hapa ni watu wazima na tunajua namna ya kuchambua ishus betweeen the lines,

- Unaonekana una tatizo bigger than hii party kwa nini usiliseme tu mkuu, ukapatiwa majibu? Ila tu so far so good matayarisho yamepamba moto na wallahi hii party itakuwa ni kwa mtindo wa mdundo kama ule ambao ungetumika kwenye safari ya Tour ya mwisho ya MJ, yaani "This is it", kwa hiyo just see yah there!

Ahsante.

William.
mkuu heshima mbele na sina tatizo lolote zaidi ya hapo na ndio maana nikatumia neno "WAZO" kama unajua linamaanisha nini na nikaendelea kusema kwamba mie pia napenda pati na yote uliotaja juu hapo ndio niliosema na nimeongezea tu hilo "WAZO" amabalo naona limekuhudhi kidogo.Sasa nashangaa umechukulia personal japokuwa kwamba sikulenga party hii tu nimezungumzia nchi zote za nje lakini nimekuelewa majibu yako na nashukuru kufahamu kwamba wazo langu alistahili kuwa hapa kama ulivyosema na nimekuelewa.samahani sana mkuu kama kawazo kangu kamekugusa kiasi hiko.huyo RAISI kikwete unayesema alitakakushusha mbingu na majibu yake wakati aliulizwa swali mbona anashindwa kuwashusha "MAFISADI" na anacheo zaidi sasa hivi kuliko wakati huo aliotaka kushusha mbingu? anyway umefanya tutoke nje ya topic kidogo lakini kama nilivyokwambia lilikuwa wazo mkuu.
 
Last edited:
Taarifa ya The Bash:-

Asalaam Waleikhum Ndugu Zangu,

Wakuu naomba kutoa heshima za juu kwa wananchi wote mliohudhuria hili Bash, kwa kifupi ni kwamba:-

1. Bash lilifanyika kama lilivyopangwa, yaani kuanzia Saa Nane Mchana na lilisha saa Sita za Usiku yaani saa ambayo mimi nilikuwa mtu wa mwisho kuondoka uwanjani, ambapo kwa pamoja wananchi karibu wote kutoka pale tulihamia Alamo Club, kujumuika na Ma-DJ Mao & Freddy, mpaka muda mchache sana uliopita, yaani majogoo ya asubuhi.

- Naomba samahani kwa wapenzi wengi mliokuwa mmekuja kushuhudia pambano la mavazi na minenguo ya Ndombolo na Taarabu, na wale wote mliojiandikisha kushikiri kwamba hatukuweza kufanya hivyo kutokana na wingi wa wananchi ndani ya Club, haikuwezekana kabisa kusimamisha muziki jinsi wananchi walivyokuwa wanayaruka majoka. Lakini ninaahidi kwamba next time tutayarisha siku maalum kwa ajili hiyo tu!

- Kwenye hili Bash, tuli-serve Nyama za kuchoma, kuanzia za mbuzi, ngo'mbe na kuku. Vinywaji baridi na vikali, na pia kulikuwa na matunda na maji kwa wingi sana si unajua mambo ya afya!

2. The Bash, ilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dr. Asha-Rose Migiro, Balozi wetu Umoja wa Mataifa, Dr. Augustine Mahiga, (ambaye pia Bash lilifanyikia nyumbani kwake), Maofisa wa Ubalozi wetu kwenye Umoja wa Mataifa na familia zao, Mkurugenzi Mteule wa NIMR Tanzania Dr. Mwele Malecela, Wa-Tanzania walioko Umoja wa Mataifa, na pia sisi wananchi walalahoi ambao ndio tuliokuwa wengi zaidi na familia zetu.

3. Wakizungumza kwa nyakati mbali mbali, viongozi Dr. Migiro na Dr. Mahiga, walionyesha kufurahishwa sana na the turnout ya wananchi na pia kuwakumbusha wananchi wote kwamba sisi wote ni ndugu wamoja, tuendelee kudumisha amani na mshikamano wetu, na pia kujumuika kila inapobidi either wakati wa shida (kama tulivyojumika last week kwa mwananchi mwenzetu aliyefiwa na mzazi wake) au wakati wa raha pia kama kwenye hili Bash na kwamba siku zote ni muhimu kuwepo na balance.

4. Sasa as the Organizer/Cordinator wa hili Bash ambalo nilishirikiana na watayarishaji yaani kamati ya sherehe ya Ofisi ya Ubalozi wetu NY, naomba kusema hivi from the bottom of my soul, natoa heshima kwa wananchi walalhoi wenzangu wote karibu 200 mliohudhuria, kwa kuitikia wito huu ambao sio siri kwamba kulikuwa na time limitation yaani siku nne tu za kuitangaza, hii ni kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika, ndio maana ninaelewa kwamba kwa nini wananchi wengi hawakufika.

- Walikuwepo wananchi toka Boston, Springfield MA, Lansik Michigan, Las Vegas, Poconos, Arizona, New Jersey, Connecticut, DC, Philly na Wakulu wa NYC na vitongoji vyake kama kawa, yaani The Bronx, Brooklyn, Queens, Manhattan, Staten Island, Long Island na pia The Crew wakulu wa Mount Vernon, na ma-JF kama Mkulu Maxshimba na Sahiba, I am humbled na presence yenu, wananchi wengi sana walijitambulisha kwangu kama ni Ma-JF respect kwenu wote ambao msingependa niwataje kwa majina yenu ya hapa! I was shocked na jinsi wakinamama wengi waliojitokeza kujitambulisha kwangu kuwa ni members hapa, that was wasup!

- Pia Owner wa Blog maarufu sana sasa hivi New York, ya fundiwakombo.blogspot alikuwepo, Mkuu respect zaidi. Maharusi wetu Mr. & Mrs. Binamungu waliofunga ndoa tuliyohudhuria last week kule New Jersey walikuwepo, naomba kuwapa hongera tena na karibuni to the Club ya maisha ya ndoa. Pia Mkulu Maftah, supplier wa mbuzi tuliowatumia kwenye hili Bash, alikuwepo, ukimuhitaji in the future ni-PM tu hakuna tatizo. Afisa Utawala wa Ubalozi wetu NYC naye alikuwepo.

- The bash limefanyika na kuisha kwa amani na upendo, mimi na kamati ya matayarisho ndio tuiliokuwa watu wa mwisho kuondoka pale uwanjani yaani Saa Sita kamili usiku, hakukuwa na anything unusual, kwa hili ninawapa heshima tena wananchi wote kwa ustaarabu wenu wa hali ya juu sana mlio uonyesha, I am proud na kila mwananchi aliyehudhuria for that, na ninasema kwamba Mungu wa Mbinguni awajalie na kuwaongezea amani zaidi katika maisha yenu.

- Kamati nzima ya matayarisho kutoka Ubalozi wetu NYC, ninawaambia kwamba I am humbled na your trust in me na poleni sana na uchovu wa shughuli, na pia naomba niwe mkweli kwa wananchi wote mliohudhuria kwamba kama kuna any negativity au mapungufu katika This Bash, basi ni mimi ndiye ninayebeba msalaba huu, yaani the buck stops here kwangu kwa 100%, lakini I gave it all.

Mungu wa Mbinguni Awazidishieni Wote na Hasa JF inayotukutanisha Ibarikiwe ili Idumu Zaidi, na Pia Ndugu zangu Issa Michuzi na Mkulu Wa Springfield Masss, mbarikiwe sana kwa all your support!

Ahsanteni Wote na samahani kwa maelezo marefu lakini ni vyema kuwa na picha kamili ya yaliyojiri.

William.

NB: I am looking forward ku-organize one more Bash, Mungu akipenda kabla ya mwisho wa Summer, stay tuned!
 
Asante Mkulu. It was nice once again kukutana nawe na Mkuu wetu balozi na Mama Migiro.

Mungu awabariki na kuwazidishia pale mlipo pungukiwa.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom