TANGANYIKA INDEPENDENT 1961 (video)

Mazee shukurani sana.

Watu walifurahi sana siku hiyo ya December 9 1961. Lakini furaha na ndoto hii imebadilikwa kuwa jinamizi.
 
Shukrani sana Babylon - nimeku-SENK ki-jF

Lakini ni kweli NDOTO za hawa wa-Tanzania zimetimia? Je tumekuwa HURU? Je tumeona MATUNDA ya Uhuru? Je Tuna-KULA MATUNDA ya Uhuru?

Ipo siku!
 
Miaka ya kumalizikia muongo wa 1970, nilipata bahati ya kuzungumza na Mzee Asanterabi Nsilo Swai (sasa marehemu) hapa kwenye Umoja wa Mataifa, New York, kuhusu suala la "modality of decolonization and independence for Tanganyika."

Mzee Swai alikuwa ni mmojawapo wa wajumbe wazalendo wa mazungumzo ya "Lanacaster House Constitutional Conference" kuhusu uhuru wa Tanganyika.

Mzee Asanterabi Nsilo Swai alisema kwamba tulipewa Serikali ya Madaraka Mei 1961, ambayo ilikuwa idumu kwa mwaka mmoja. Kwahiyo, kulingana na uamuzi huo, tulikuwa tujitawale Juni 1962. Lakini tulijitawala 9 Desemba, 1961.

Moja, kwa nini Tanganyika ilijitawala mwezi Desemba 1961 na sio mwezi Juni 1962?

Mbili, ni akina nani kwa upande wa wazalendo (TANU) walioamua siku hiyo ya uhuru?

Kwenye Mkutano wa Lancaster Conference wa mwisho, uliofanyika mjini Dar es Salaam, kulikuwepo na utata wa kuamua siku hiyo ya uhuru miongoni mwa wazalendo wawakilishi wa TANU.

Macleod-Turnbull-Brown (wakoloni) walitamka kuwa mwenye kuwakilisha "State" ya Uingereza siku ya uhuru mwezi Juni 1962 angekuwa Malkia Elizabeth II.

Walipendekeza kuwa haingewezekana kwa Malkia Elizabeth II kuja Tanganyika mwezi wa Juni kwa sababu ya shughuli za ki-itifaki zinazofanywa mwezi huo wakati wa kusheherekea Siku ya Kuzaliwa kwa Malkia.

Malkia Elizabeth II (Elizabeth Alexandra Mary) alizaliwa tarehe 21 April, 1926; sherehe za ki-serikali zinafanywa kila mwaka mwezi Juni.

Malumbano yalieendelea kwa muda mrefu. Wakoloni walipendekeza uhuru wa Tanganyika uwe mwezi Desemba 1962. Wazalendo walikataa kata siku ya kuzaliwa kwa Malkia wa Uingereza kuchelewesha uhuru wa Tanganyika!

Hatimaye, Mwenyekiti wa mkutano huo, Bwana Ian Macleod, alishauri akutane na baadhi tu ya wajumbe wazalendo. Akashauri akutane na wajumbe watatu ili wamalize upesi malumbano yaliyokuwa yanajitokeza.

Je, Nyerere aliwachagua akina nani?

Aliwachagua Oscar Salathiel Kambona na Asanterabi Nsilo Swai.

Baadhi ya "vigogo" wa ujumbe wa wazalendo hawakupendezwa na uteuzi huo!

Kwenye mkutano wa kikundi hicho kidogo, ilibidi Waziri wa Makoloni Ian Macleod aukunje mkia na kuwaisha siku ya uhuru wa Tanganyika kwa miezi sita --- 9 Desemba, 1961.

Julius Nyerere alitangaza kwa wananchi mjini Dar es Salaam kuwa Tanganyika itajitawala tarehe 9 Desemba 1961. Alibebwa juu juu mabegani huku akishikilia kibango kilichoandikwa "Complete Independence 1961."
 
Miaka ya kumalizikia muongo wa 1970, nilipata bahati ya kuzungumza na Mzee Asanterabi Nsilo Swai (sasa marehemu) hapa kwenye Umoja wa Mataifa, New York, kuhusu suala la “modality of decolonization and independence for Tanganyika.”

Mzee Swai alikuwa ni mmojawapo wa wajumbe wazalendo wa mazungumzo ya “Lanacaster House Constitutional Conference” kuhusu uhuru wa Tanganyika.

Mzee Asanterabi Nsilo Swai alisema kwamba tulipewa Serikali ya Madaraka Mei 1961, ambayo ilikuwa idumu kwa mwaka mmoja. Kwahiyo, kulingana na uamuzi huo, tulikuwa tujitawale Juni 1962. Lakini tulijitawala 9 Desemba, 1961.

Moja, kwa nini Tanganyika ilijitawala mwezi Desemba 1961 na sio mwezi Juni 1962?

Mbili, ni akina nani kwa upande wa wazalendo (TANU) walioamua siku hiyo ya uhuru?

Kwenye Mkutano wa Lancaster Conference wa mwisho, uliofanyika mjini Dar es Salaam, kulikuwepo na utata wa kuamua siku hiyo ya uhuru miongoni mwa wazalendo wawakilishi wa TANU.

Macleod-Turnbull-Brown (wakoloni) walitamka kuwa mwenye kuwakilisha “State” ya Uingereza siku ya uhuru mwezi Juni 1962 angekuwa Malkia Elizabeth II.

Walipendekeza kuwa haingewezekana kwa Malkia Elizabeth II kuja Tanganyika mwezi wa Juni kwa sababu ya shughuli za ki-itifaki zinazofanywa mwezi huo wakati wa kusheherekea Siku ya Kuzaliwa kwa Malkia.

Malkia Elizabeth II (Elizabeth Alexandra Mary) alizaliwa tarehe 21 April, 1926; sherehe za ki-serikali zinafanywa kila mwaka mwezi Juni.

Malumbano yalieendelea kwa muda mrefu. Wakoloni walipendekeza uhuru wa Tanganyika uwe mwezi Desemba 1962. Wazalendo walikataa kata siku ya kuzaliwa kwa Malkia wa Uingereza kuchelewesha uhuru wa Tanganyika!

Hatimaye, Mwenyekiti wa mkutano huo, Bwana Ian Macleod, alishauri akutane na baadhi tu ya wajumbe wazalendo. Akashauri akutane na wajumbe watatu ili wamalize upesi malumbano yaliyokuwa yanajitokeza.

Je, Nyerere aliwachagua akina nani?

Aliwachagua Oscar Salathiel Kambona na Asanterabi Nsilo Swai.

Baadhi ya “vigogo” wa ujumbe wa wazalendo hawakupendezwa na uteuzi huo!

Kwenye mkutano wa kikundi hicho kidogo, ilibidi Waziri wa Makoloni Ian Macleod aukunje mkia na kuwaisha siku ya uhuru wa Tanganyika kwa miezi sita --- 9 Desemba, 1961.

Julius Nyerere alitangaza kwa wananchi mjini Dar es Salaam kuwa Tanganyika itajitawala tarehe 9 Desemba 1961. Alibebwa juu juu mabegani huku akishikilia kibango kilichoandikwa “Complete Independence 1961.”

Tungekuwa na waandishi wa habari wanaoandika kama hivi ningefurahi sana.Just the facts, vikorombwezo na uzushi na nini sijui inakuwa vigumu sana kama unaheshimu facts kama huyu mwandishi.
 
...Safi sana....Inakumbusha mbali tulikotoka ingawa tunakokwenda ni giza zaidi......
 
Nilishawahi kuona mkanda video ya Uhuru wa Tanganyika. Nafikiri BBC wanazo zote na Waandishi wa Habari wa Tanzania kama Tido Mhando wanaweza kuziulizia na kuomba copy. Ninachikumbuka hadi leo ni taa ya diod iliyowashwa na kufanya sura ya NYERERE.

KWa wale vijana, kama mmeona kibao INDEPENDENCE EVENUE basi mfahamu kuwa hiyo ni SAMORA EVENUE.
Pia ukiangalia 2:37:35 utamuona Mtemi wa Wanyamwezi. Sijui kama huyu alikuwa ni Marehemu Abdallah Fundikira au baba yake. Nimemfahamu kwa sababu moja tu kuwa ile symbol aliyovaa kichwani na ile shuka/mgolole?? ni sawa na aliyovaa huyu jamaa ambaye sasa ni mtemi aitwaye Msagata Ngulati Fundikira.

7250d1261513961-tanganyika-independent-1961-video-msagata-ngulati-fundikira.jpg
 
Attachments

  • Msagata Ngulati Fundikira.jpg
    Msagata Ngulati Fundikira.jpg
    53.3 KB · Views: 106
Ingefaa sana tutafute movies alizocheza Rasid Mfaume Kawawa za Idara ya Maendeleo ya Jamii:

Muhogo Mchungu

Dawa ya Mapenzi

Charo Afika Dar es Salaam
 
Who was the head of state in Tanganyika on December 25 1961?

Who did the Prime Minister report to?

Who signed the laws?
 
Mlenge,

Head of State was Queen Elizabeth 11, who was represented by the Governor-General Richard Turnbull in Tanganyika.

Who did the Prime Minister report to?

Parlaiament.

Who signed the laws?

Governor-General Richard Turnbull on behalf of Queen Elizabeth 11.
 
Miaka ya kumalizikia muongo wa 1970, nilipata bahati ya kuzungumza na Mzee Asanterabi Nsilo Swai (sasa marehemu) hapa kwenye Umoja wa Mataifa, New York, kuhusu suala la "modality of decolonization and independence for Tanganyika."

Mzee Swai alikuwa ni mmojawapo wa wajumbe wazalendo wa mazungumzo ya "Lanacaster House Constitutional Conference" kuhusu uhuru wa Tanganyika.

Mzee Asanterabi Nsilo Swai alisema kwamba tulipewa Serikali ya Madaraka Mei 1961, ambayo ilikuwa idumu kwa mwaka mmoja. Kwahiyo, kulingana na uamuzi huo, tulikuwa tujitawale Juni 1962. Lakini tulijitawala 9 Desemba, 1961.

Moja, kwa nini Tanganyika ilijitawala mwezi Desemba 1961 na sio mwezi Juni 1962?

Mbili, ni akina nani kwa upande wa wazalendo (TANU) walioamua siku hiyo ya uhuru?

Kwenye Mkutano wa Lancaster Conference wa mwisho, uliofanyika mjini Dar es Salaam, kulikuwepo na utata wa kuamua siku hiyo ya uhuru miongoni mwa wazalendo wawakilishi wa TANU.

Macleod-Turnbull-Brown (wakoloni) walitamka kuwa mwenye kuwakilisha "State" ya Uingereza siku ya uhuru mwezi Juni 1962 angekuwa Malkia Elizabeth II.

Walipendekeza kuwa haingewezekana kwa Malkia Elizabeth II kuja Tanganyika mwezi wa Juni kwa sababu ya shughuli za ki-itifaki zinazofanywa mwezi huo wakati wa kusheherekea Siku ya Kuzaliwa kwa Malkia.

Malkia Elizabeth II (Elizabeth Alexandra Mary) alizaliwa tarehe 21 April, 1926; sherehe za ki-serikali zinafanywa kila mwaka mwezi Juni.

Malumbano yalieendelea kwa muda mrefu. Wakoloni walipendekeza uhuru wa Tanganyika uwe mwezi Desemba 1962. Wazalendo walikataa kata siku ya kuzaliwa kwa Malkia wa Uingereza kuchelewesha uhuru wa Tanganyika!

Hatimaye, Mwenyekiti wa mkutano huo, Bwana Ian Macleod, alishauri akutane na baadhi tu ya wajumbe wazalendo. Akashauri akutane na wajumbe watatu ili wamalize upesi malumbano yaliyokuwa yanajitokeza.

Je, Nyerere aliwachagua akina nani?

Aliwachagua Oscar Salathiel Kambona na Asanterabi Nsilo Swai.

Baadhi ya "vigogo" wa ujumbe wa wazalendo hawakupendezwa na uteuzi huo!

Kwenye mkutano wa kikundi hicho kidogo, ilibidi Waziri wa Makoloni Ian Macleod aukunje mkia na kuwaisha siku ya uhuru wa Tanganyika kwa miezi sita --- 9 Desemba, 1961.

Julius Nyerere alitangaza kwa wananchi mjini Dar es Salaam kuwa Tanganyika itajitawala tarehe 9 Desemba 1961. Alibebwa juu juu mabegani huku akishikilia kibango kilichoandikwa "Complete Independence 1961."

Mkuu, Asante kwa makala yako fupi na yenye kueleweka.... Nimekumbana na thread hii kwa msaada wa Google, Kuelekea miaka 50 ya Uhuru Tanganyika, siyo vibaya tukajikumbusha historia ya nchi yetu, maana wengine tuko nyuma kidogo...

Mkuu, Ningependa kufahamu juu ya Mzee Asanterabi Nsilo Swai angalau kwa uchache tu..
 
Thnx much. Inafurahisha. Mbona haya hayapo ktk historia yetu. Shulen hazfundshw.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom