Tanganyika ilikufaje Z'bar ikasalimika?

10/10/1963 ndo tarehe, mwezi na mwaka wazanzibari walipotoka karika minyororo ya dhulma za wakoloni wa Uingereza(slave traders, colonialists,imperialists,neo colonialists etc)
Junius,
Thanks. Nilikuwa namsahihisha Mlenge aliyesema Zanzibar ilipata uhuru kabla ya Tanganyika.
 
Zanzibar: ilikuwa ni nchi kabla haijatawaliwa
Tanganyika: kwanza ilitengenezwa iwe inchi, ndipo ikatawaliwa.

Kwa hiyo: Zanzibar ilikuwapo kabla ya Tanganyika.

Najua sisi Watanzania (bara) tunapenda sana 'sifa' kwa nchi yetu, lakini penye ukweli lazima tuseme.

Ndio maana utakuta sikukuu ya "Uhuru wa Tanzania" inasherehekewa 9-Disemba, hata kama Tanzania haikupata kutawaliwa ukoloni mkongwe; au utasikia kwamba Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961, ilhali Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1962; mradi tu isionekane Nyerere na TANU walikubali kuunda serikali chini ya utawala wa Malkia / Mfalme wa Uingereza aliyekuwa mkuu wa nchi ya Tanganyika (kupitia Gavana) mpaka mwaka 1962. Tanzania inapata kigugumizi kusema wapi mji mkuu uliko, kwa vile inataka 'sifa' kwamba na sisi dodi 'tumehamisha mji wetu mkuu', doli-doli, doli samora! wakati de facto / de jure mji mkuu ni Dar es Salaam.

Lakini yote haya ni "Red herring" ya real issue: is there love lost between Tanganyika and Zanzibar? Why Tanzania rulers want and budget for Tanzania to be a province of EAC federal government ('serikali saba'), but frets when hearing suggestion of having Federal Government of Tanzania ('serikali tatu')? Why aren't the articles of union in the public? Why aren't people of Zanzibar and Tanganyika are not asked whether and how they want the Union be structured?

Mlenge
 
Zanzibar: ilikuwa ni nchi kabla haijatawaliwa
Tanganyika: kwanza ilitengenezwa iwe inchi, ndipo ikatawaliwa.

Una maana gani unaposema "Zanzibar ilikuwa ni nchi kabla haijatawaliwa"?

Ni tafsiri ipi ya dhana ya "nchi" unayotumia?
 
Zanzibar: ilikuwa ni nchi kabla haijatawaliwa
Tanganyika: kwanza ilitengenezwa iwe inchi, ndipo ikatawaliwa.

Kwa hiyo: Zanzibar ilikuwapo kabla ya Tanganyika.

Najua sisi Watanzania (bara) tunapenda sana 'sifa' kwa nchi yetu, lakini penye ukweli lazima tuseme.

Ndio maana utakuta sikukuu ya "Uhuru wa Tanzania" inasherehekewa 9-Disemba, hata kama Tanzania haikupata kutawaliwa ukoloni mkongwe; au utasikia kwamba Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961, ilhali Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1962; mradi tu isionekane Nyerere na TANU walikubali kuunda serikali chini ya utawala wa Malkia / Mfalme wa Uingereza aliyekuwa mkuu wa nchi ya Tanganyika (kupitia Gavana) mpaka mwaka 1962. Tanzania inapata kigugumizi kusema wapi mji mkuu uliko, kwa vile inataka 'sifa' kwamba na sisi dodi 'tumehamisha mji wetu mkuu', doli-doli, doli samora! wakati de facto / de jure mji mkuu ni Dar es Salaam.

Lakini yote haya ni "Red herring" ya real issue: is there love lost between Tanganyika and Zanzibar? Why Tanzania rulers want and budget for Tanzania to be a province of EAC federal government ('serikali saba'), but frets when hearing suggestion of having Federal Government of Tanzania ('serikali tatu')? Why aren't the articles of union in the public? Why aren't people of Zanzibar and Tanganyika are not asked whether and how they want the Union be structured?

Mlenge

Si kweli kwamba zanzibar ilikuwepo kabla ya mkoloni mwarabu. Nirekebishe kama nimekosea.

The word ZANZIBAR is of Persian or Arabic origin. The Persians derive the name from Zangh Bar, meaning "the Negro Coast." On the other hand the Arabs deduce the name from the Arabic Zayn Z'al Barr, meaning "Fair is this land", an epithet that aptly describes the striking beauty of the country
The name Zanzibar once applied to the whole of the East African coast with its adjacent islands, from Somalia to Mozambique, and far into the interior of Zaire.
 

MUUNGANO WETU: Tanganyika ilikufaje Z'bar ikasalimika? (2)

Joseph Mihangwa

KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya wiki iliyopita, tuliona chimbuko la migogoro na kero za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambazo hazijapata ufumbuzi makini hadi leo.

Nilisema kuwa kuahirishwa kwa muda usiojulikana kwa uteuzi wa Tume ya Kupendekeza Katiba, ili hatimaye kuweza kuitishwa kwa Bunge la Katiba ndani ya mwaka mmoja, ili kupitisha Katiba ya Jamhuri mpya ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kuliupokonya Muungano huo nafasi ya kujiongoza kwa dira iliyokusudiwa, na hivyo kuendeshwa kwa Amri za Rais (decrees) na hisia za ki-imla kwa matashi ya wanasiasa.

Tuliona jinsi kwa miaka 13, tangu Aprili 26, 1964 hadi mwaka 1977, Muungano huo ulivyoendeshwa na kuongozwa kwa Katiba (ya muda) ya kuazima kutoka Tanganyika, hadi ilipoundwa Tume ya TANU na ASP, kupendekeza kuunganishwa kwa vyama hivyo, ambayo baada ya kazi hiyo, ilijigeuza kuwa Tume ya Kupendekeza Katiba ya Jamhuri ya Muungano, kinyume na matakwa ya Mkataba wa Muungano (Articles of Union) na Sheria za Muungano (Acts of Union).

Mapendekezo ya Tume hiyo ndiyo yaliyozaa Katiba ya Jamhuri ya Muungano 1977 iliyopitishwa na Bunge la kawaida badala ya Bunge la Katiba.

Tulibainisha kwamba, mikanganyiko mingi iliyoletwa na Katiba ya 1977 ni ya kurithi kutoka Katiba ya muda ya 1965, ambayo sio tu ilikwenda kinyume kwa sehemu kubwa na matakwa ya Mkataba na Sheria za Muungano; bali pia iliingiza mambo ya vyama vya siasa ambayo hayakuwa sehemu au moja ya mambo ya Muungano.

Niendelee nilikoishia wiki iliyopita kwa kusema kwamba, Katiba ya muda ya 1965 iliandaliwa na Mwanasheria Mkuu (wa Tanganyika), ikapitishwa na Baraza la Mawaziri la Muungano, kisha Bunge la kawaida la Muungano, na kutiwa sahihi na Rais wa Muungano; yote hayo yakifanyika kinyume cha matakwa ya (Hati) Mkataba wa Muungano na Sheria za Muungano.

Haukupita muda, mara Serikali ya Muungano ikaanza kunyemelea mambo mengine yasiyo ya Muungano kwa kuongeza idadi ya mambo ya Muungano, na kwa kuyapunguza yasiyo ya Muungano, hadi Tanganyika ikajikuta imekuwa ndiyo Tanzania, kama tutakavyoona baadaye katika makala hii.

Ni hisia hizi za kisiasa zilizozaa Katiba inayohojika ya mwaka 1977, na ambayo imeshindwa kutatua kero za Muungano na mitafaruku ya kisiasa huko Zanzibar.

Katiba ya nchi haipashwi kutawaliwa au kuongozwa kwa hisia za kisiasa, kwa sababu si kila mwananchi ni mpenzi wa siasa. Katiba ya kweli lazima ilenge kukidhi matakwa ya kila raia, bila kujali itikadi ya mtu; wala mtu asiwekewe mipaka ya ushiriki wake katika mambo ya nchi na ya uongozi, kwa maana huo ni ubaguzi kinyume na haki za raia. Katiba yetu ya sasa imejikita katika hayo.

Lakini, kwa nini mapungufu haya yaliruhusiwa kuingia katika Katiba yetu? Au ni kwa sababu ya wanasiasa wasioambilika?

Mkataba wa Muungano na Sheria za Muungano ndizo misingi mikuu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, bila hivyo hakuna Katiba, hakuna Muungano wala Zanzibar. Aidha, Bunge la kawaida la Muungano halina mamlaka ya kurekebisha, kupunguza au kuongeza mambo ya Muungano yaliyofikiwa kwenye Mkataba wa Muungano ambao hadi sasa unasomeka kama ulivyotiwa sahihi na waasisi wake hapo Aprili 22, 1964.

Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, iliundwa mahsusi kushughulikia mambo 11 tu ya Muungano, na kuacha mambo mengine yashughulikiwe na serikali huru za Tanganyika na Zanzibar, kila moja kwa eneo lake.

Hivi leo, mambo ya Muungano yamefikia 23 kwa njia ya Amri za Rais (decrees). Je, Rais, kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, ana mamlaka ya kuongeza au kupunguza mambo ya Muungano? Jibu ni "hapana".

Hakuna ubishi kwamba, Mkataba wa Muungano (Articles of Union) wa 1964, na Katiba ya mpito (Interim Constitution) ya 1964, zilitambua tangu mwanzo uwapo wa Serikali tatu - Serikali ya Muungano, Serikali hai ya Tanganyika na Serikali hai ya Zanzibar; hizi mbili kila moja ikiwa na mamlaka kamili kwa mambo yasiyo ya Muungano. Na hilo ndilo lilikuwa kusudio la Muungano chini ya mfumo uliotakiwa.

Alipomwagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanganyika, Rawland Brown, aandae Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, kwa mfano wa uhusiano kati ya Serikali ya Uingereza na Jamhuri ya Ireland, Aprili 18, 1964, Mwalimu Julius K. Nyerere hakumaanisha au kukusudia mfumo wa Muungano tunaoendesha leo. Na ndivyo Brown alivyoelewa pia. Tatizo letu ni upotoshaji wa tafsiri kwa vitendo, lakini mkataba huo ni sahihi kabisa kama ulivyokusudiwa.

Mkataba huu unafanana na ule wa Muungano kati ya Ethiopia na Eritrea; lakini kwa sababu pia ya kupotoshwa kwa makusudi na Serikali ya Ethiopia, migogoro na vita kati ya nchi hizo mbili imeendelea kwa muda mrefu hadi sasa.

Tatizo lilianza na Katiba ya muda ya 1965 ambayo, chini ya ibara ya 12 (1), ilibainishwa kinyemela kwamba: "Mamlaka ya utendaji (the executive) kuhusu mambo yote ya Muungano katika, na kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na (pia) kwa Tanganyika, yatakuwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano".

Hii ni kusema kwamba, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius K. Nyerere, alifanywa kuwa Rais wa Serikali mbili - Serikali ya Muungano na Serikali ya Tanganyika. Lakini isingekuwa hivyo, kama Karume angekuwa Rais wa Kwanza wa Muungano; yeye angekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na hapo hapo Rais wa Zanzibar, na Nyerere kubakia Rais wa Tanganyika.

Tunaamini kwamba, huu ulikuwa ni mpangilio wa muda tu kusubiri Katiba ya Muungano; na pia kwamba Nyerere alikuwa hakwepeki kuhodhi madaraka hayo kwa sababu Katiba ya Tanganyika ndiyo iliyokuwa pia Katiba ya Muungano, wakati Muungano ukisubiri Katiba yake, kama nilivyoeleza mwanzo.

Lakini utata huo ulizidi kuota mizizi pale ibara ya 49 ya Katiba hiyo ilipotamka kuwa: "Mamlaka ya kutunga Sheria kuhusu mambo yote ya Muungano katika, na kwa ajili ya Muungano; na kwa mambo yote katika, na kwa ajili ya Tanganyika, ni ya Bunge la Muungano".

Hii ilimaanisha kwamba, Rais wa Muungano sasa ndiye aliyekuwa pia Rais wa Tanganyika; na Bunge la Muungano, ndilo lililokuwa Bunge la Tanganyika, na kinyume chake.

Kwa jinsi hii, Tanganyika, kwa ukarimu usio kifani, ilikuwa imetoa kila kitu kilichokuwa chake juu na zaidi ya hisa ilizopashwa kuchangia katika Muungano, tofauti na Zanzibar iliyotoa hisa 11 tu, na kubakiza mengine yote ndani ya mipaka yake; lakini ikaruhusiwa kutumbua vinono vyote vya Tanganyika kwa mtaji mdogo wa hisa hizo 11.

Lakini kwa ukarimu huo, Tanganyika ilikiuka masharti ya Mkataba wa Muungano ambao uliitaka itoe/ichangie mambo 11 tu katika kapu la Muungano, ili kutoifanya Zanzibar ijione kama mshiriki duni asiye na sauti katika Muungano; au kama mgeni aliyekaribishwa tu kutumbua vinono vingi vya mwenyeji wake. Hilo ndilo Wazanzibari wanalalamikia kwa madai ya "kumezwa" na Tanganyika.

Lakini tofauti na Tanganyika, ambayo mamlaka yake yaligeuka kuwa ya Kimuungano, mamlaka ya utendaji kwa Serikali ya Zanzibar yalibakia kwa Rais wa Zanzibar, na yale ya kutunga Sheria kwa mambo yasiyo ya Muungano, yalibakia kwa Baraza la Wawakilishi.

Kana kwamba jina la Tanganyika lilikuwa limeota ukoma, juhudi zilifanyika kwa nguvu, lakini kwa shida sana, kulifuta kabisa katika historia ya Muungano kwa ubatizo wa nguvu kuitwa "Tanzania", kama tulivyokwishaeleza hapo mwanzo.

Tanzania ni jina lililosajiliwa kuwakilisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini jina halisia chini ya Mkataba na Sheria ya Muungano linabakia kuwa "Muungano wa Tanganyika na Zanzibar", bila kubadilika.

Ndiyo kusema kwamba, Tanzania ni kifupisho tu cha "Tanganyika na Zanzibar", kama vile Mwalimu Nyerere alivyowafundisha Watanzania kulitamka kama "Tan-Zan-ia", ili kutopoteza uwapo na hadhi ya kila nchi hizo katika Muungano.

Lakini kwa nini jina "Tanganyika" lilipotea miaka mitatu baada ya Muungano, wakati haikuwa hivyo tangu Muungano? Kwa nini haikuwa dhambi kuwapo kwa Tanganyika, ila baada ya miaka mitatu baadaye?

Tutatoa mfano: Katiba ya muda ya 1965 (ibara ya 2), ilitambua kwamba, "Eneo la Tanzania linajumuisha Tanganyika na Zanzibar".

Na kuhusu majimbo ya uchaguzi, ibara ya 25 ya Katiba hiyo ilitamka wazi kuwa, "Tanganyika itagawanywa katika majimbo mengi kwa kuzingatia idadi ya wakazi wapiga kura, na kila jimbo litakuwa na mbunge mmoja".

Kuhusu wajumbe wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, ibara ya 24 (1) (c), ilitambua kuwamo kwa "Wakuu wa Mikoa 17 wa kuteuliwa kwa Mikoa 17 (wakati huo) ya Tanganyika, na watatu wa Mikoa ya Zanzibar", kuonyesha kwamba Tanganyika na Zanzibar zilikuwa na mfumo wake wa utawala kwa mambo yasiyo ya Muungano.

Kama Katiba hiyo ilitambua kuwapo kwa Tanganyika hadi miaka mitatu baada ya Muungano, nchi hiyo iliyeyukia wapi, lini na kwa nini? Kwa nini kuyeyuka kwa Tanganyika kusitafsiriwe kumaanisha mmoja wa Wabia wa Muungano, Zanzibar, kukosa mshirika katika Muungano kufuatia hatua hiyo? Je, Zanzibar imeungana na Tanganyika au "Tanzania" ambayo haimo katika Mkataba wa Muungano?

Kwa nini hatua hiyo isitafsiriwe kuwa ni kitendo cha kukatisha tamaa (frustrate) au kuvuruga Muungano? Ni nani chanzo cha vurugu hii?

Msumari wa chuma ulipigiliwa kwenye kichwa cha Tanganyika kufuatia kutungwa kwa Sheria Namba 27 ya 1967 na Bunge la kawaida, iliyompa Rais uwezo wa kuweka neno "Tanzania" badala ya "Tanganyika" katika Sheria zote, na mahali popote "Tanganyika" lilipoonekana, lakini bila kugusa wala kubadili jina hilo katika Hati ya Mkataba wa Muungano na Sheria ya Muungano, ambazo hata hivyo, Rais hakuwa na mamlaka ya kuzibadili.

Hii ni kwa sababu, kwanza, Mkataba wa Muungano una hadhi ya kimataifa isiyoweza kuguswa na sheria za nchi; na pili, Sheria ya Muungano ni tunda la Mkataba huo wa Kimataifa ambapo kazi pekee ya mabunge ya nchi hizo mbili huru, ilikuwa ni kuridhia tu yaliyomo katika mkataba ili yapate nguvu ya kisheria kwa utekelezaji wa mambo yale 11 ya Muungano; na yasiyo ya Muungano yaendelee kushughulikiwa na Serikali za nchi husika.

Mabadiliko yote haya, kuanzia na Rais kuahirisha kuteua Tume ya kupendekeza Katiba na kutoitisha Bunge la kupitisha Katiba ifikapo Machi 26, 1965; kutungwa kwa Katiba ya muda ya 1965, na Sheria Na 24 ya 1967 iliyofuta kwa nguvu jina la Tanganyika; ndiyo yaliyoridhiwa na kurithishwa bila utafiti makini wa kisheria, kwa kuingizwa katika Katiba ya kudumu ya Jamhuri ya Muungano ya 1977; ambayo nayo hata hivyo, misingi na uhalali wa kutungwa kwake umezua utata miongoni mwa wanasheria wa mambo ya Katiba.

Katiba hiyo ilikwenda mbali zaidi kwa kutoa "ubatizo" kwa Tanganyika na kupewa jina la "Tanzania Bara", wakati huo huo mambo yake yasiyo ya Muungano yakahamishiwa kwenye Muungano, kama tulivyokwishaeleza.

Ukweli ni kwamba, kuanzia hapo, Tanganyika ilifanywa kuwa ndiyo Tanzania, na Tanzania kuwa ndiyo Tanganyika kwa jina jipya la "Tanzania Bara".

Mkanganyiko huu unathibitishwa pia na Sheria ya Tafsiri ya Sheria na vifungu Vikuu (Interpretation of Laws and General Clauses Act) Namba 30 ya 1972, kifungu cha 3 ambapo neno "Jamhuri" limetafsiriwa kumaanisha "Jamhuri ya Tanganyika na inajumuisha Jamhuri ya Muungano".

Tafsiri hii sio tu kwamba inaifanya Tanganyika kuwa ndiyo "Jamhuri ya Tanzania", bali pia inafifisha jina la Tanganyika kwa upendeleo wa jina kubwa la "Tanzania".

Ni kwa sababu hii sasa hakuna "Watanganyika" ila kuna "Wazanzibari"; na kuna Watanzania kwa maana ya wakazi wa Bara, lakini si kwa Wazanzibari ambao wamebakia kama Wazanzibari.

Ndiyo maana sasa inavumilika kuona Zanzibar ina Rais wake Mtendaji, bendera na wimbo wa Taifa, ngao ya Taifa na Jeshi (JKU) ndani ya Muungano; lakini Tanganyika haiwezi kuwa na hivyo vyote, ila kwa jina la Tanzania kwa sababu imekuwa ndiyo

"Tan-Zan-ia".

Hili ndilo wanalolalamikia Wazanzibari, kwamba kitendo cha Tanganyika kuingiza mambo yake yote yasiyo ya Muungano kuwa mambo ya Muungano, ni cha ukiukaji wa Mkataba wa Muungano; na hivyo kilio chao cha kwamba Zanzibar inamezwa na Tanganyika kinasikika na kupata nguvu.

Kwa wasioyafahamu yaliyomo katika Mkataba wa Muungano, wanaweza kushangaa kuona viongozi wa Zanzibar wakijichukulia maamuzi mengi bila hofu ya kuwajibishwa, tofauti ilivyokuwa huko nyuma. Maamuzi kama vile Zanzibar kuwa na imbo na bendera ya Taifa; suala la mafuta au Rais wa Zanzibar kubeza baadhi ya maamuzi ya Halmashauri Kuu ya CCM, ni mambo yasiyokiuka Muungano, tofauti na tulivyoaminishwa siku za nyuma.

Wanafanya hivyo kwa sababu wana uhakika kwamba hawavunji wala kukiuka matakwa asilia ya Mkataba na Sheria ya Muungano kwa yale yaliyoingizwa kwa ubabe. Na kweli, kama hatutapata akili na busara, tukakubali kuupitia upya msingi na matakwa ya Muungano, Zanzibar itaendelea "kusumbua" Muungano, kero hazitakwisha hadi mwisho wa dahari.

Ni bahati mbaya kwamba viongozi wa nchi wamekuwa wazito na waoga kuelezea historia na matakwa sahihi ya Muungano; pengine kwa hofu ya kumwamsha aliyelala wasije wakalala wao.

Lakini ni bora na rahisi zaidi kuongoza au kutawala watu wenye uelewa kuliko "waliolala"; kwani hao waliolala wakiamka, wakafahamu kwamba wamedanganywa, wamehadaiwa au kupumbazwa kwa hila, wanaweza kujeruhi na amani itatoweka!

 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom