Tanesco yazidi kubanwa; Waziri Muhongo asema kesi Tanesco ni ‘ulaji’ tu; lina Kesi 200 zisizoisha

Kwa Prof. Muhongo hatimaye naona mwanga angavu kabisa wa matumaini. Huyu bwana siyo mwanasiasa. Ni mtendaji. Hataki utani wala ubabaishaji. Anachotaka ni outcome siyo output. Siyo akina nchimbi.
 
..inabidi tuwe macho kidogo hapa.

..waziri amesema kuna mikataba 26 na baadhi yake ni mibovu. halafu anawataka wajumbe wa bodi waipitie.

..sasa what happens kama wajumbe wa bodi watatofautiana na mtizamo wa waziri na kumrudishia majibu kwamba mikataba yote ni mizuri??

..kama waziri tayari ameona kuna mikataba mibovu, kwanini asitoe amri mara moja kwamba irekebishwe??

..tusiwe na haraka ya kushangilia ushindi. tusubiri miezi mitatu tuone kama kuna mikataba itarekebishwa, na zaidi ni mikataba mingapi.

Am interested to know hii board mpya. Gen(Retired) Mboma yumo ndani au this time kaachwa pembeni?
 
nguvu ya soda hiyo. Ngoja manji amuwekee 2bn mezani kwake tuone kama atakuwa tofauti na ngeleja.

wewe ni msaliti mkubwa! Mnakatisha tamaa watu wazalendo wa kweli, huyo manji kama anakudanganya siku zake zimekwisha zakutufanya sisi wajinga watu wenye bongo kama wewe ndiyo manasababisha nchi hii kuwa masikini kwa mawazo yenu ya kibinafsi.
 

Pole sana ndugu, usipoteze sana na muda na watu kama hawa, kwa kifupi ni kwamba kuna baadhi ya watu wamezi-set akili zao kwamba maadamu kitu fulani hakijafanywa au kusemwa na CHADEMA basi ni takataka, na wewe ukisema kitu chochote kukosoa CHADEMA hata kama mwisho wa siku una nia ya dhati kabisa ya kusaidia kuijenga CHADEMA bado utaambulia matusi tu na mimi nasema hawa ndio watu ambao wataiangusha CHADEMA hiyo hiyo wanayopiga kelele humu kila siku kwamba wanaipenda, sote tunapenda mabadiliko nchini mwetu na haijalishi nani anayaleta! Mh. Waziri ameongea vizuri sana na tunapata matuamaini kwamba atajaribu!

Aisee umenifurahisha sana mawazo yako hayo huo ni ukweli kabisa wote tunataka mabadiliko na in fact mtu yeyote mzalendo tumuunge mkono nchi kwanza mambo ya vyama tuachane nayo bwana! Mimi naipenda chadema sababu ya kuona huenda wakatusadia lakini wasiwasi wangu ikiwa watu ni kupinga hata kama kuna mtu anaonesha uzalendo hapo mimi ndiyo sielewi kama kweli lengo letu ni moja kukomboa nchi au kushabikia vyama!
 
Andiko moja kwenye Biblia Linaesema tusiwe na haraka ya kuweka mikono ya baraka kwenye kichwa cha mtu, Binafsi nachelea kusema nimapema sana kuamini na kutekeleza ayasemayo pamoja na nia nzuru aliyonayo haijui rangi halisi ya chama chake cha CCM.
 
Nguvu ya soda hiyo. Ngoja manji amuwekee 2bn mezani kwake tuone kama atakuwa tofauti na Ngeleja.

Look this shuleless opening ur mouth empty minded....
U know nothing & u won't know anything in ur entire life....
how u come with such F****ing words.... Sie tunamjua huyu Prof. Muhongo, si jana, au leo..... shut..up... go to ur haemophrodite manji....
 
Andiko moja kwenye Biblia Linaesema tusiwe na haraka ya kuweka mikono ya baraka kwenye kichwa cha mtu, Binafsi nachelea kusema nimapema sana kuamini na kutekeleza ayasemayo pamoja na nia nzuru aliyonayo haijui rangi halisi ya chama chake cha CCM.

Si mwanachama wa CCM, wala CDM, hana chama, hakuchaguliwa, hakuomba.. AMETEULIWA...ni mt
very open & serious on issues, na tunamjua Prof.. ni Nyerere's siblings in terms of UTAIFA..
 
Look this shuleless opening ur mouth empty minded....
U know nothing & u won't know anything in ur entire life....
how u come with such F****ing words.... Sie tunamjua huyu Prof. Muhongo, si jana, au leo..... shut..up... go to ur haemophrodite manji....
Acha kufuka mapovu kama kifutu. Mwaga mapoint tuyaone. vinginevyo tusubiri, muda ndio utaamua.
 
Mwanzo mzuri kikubwa ni apate ushirikiano....hakika nchi inaliwa hii kama ndo iko hivyo.

Hongera Waziri Muhongo....Mungu akulinde na kukubariki.




JUMAPILI, SEPTEMBA 16, 2012 08:22 NA ARODIA METER DAR ES SALAAM

*Waziri Muhongo asema kesi Tanesco ni ‘ulaji’ tu
*Asema shirika hilo hivi sasa lina kesi 200 zisizoisha.
*Aitaka TPDC kupitia upya mikataba 26 ya gesi
*Akataa fedha ya mafuta na gesi kuingizwa Hazina
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kesi mbalimbali zinazokabili mashirika yaliyo chini ya wizara yake likiwamo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni kichaka cha ‘ulaji’ wa watu.

Profesa Muhongo pia ameonya kuwa mtumishi atakayeingia mkataba mbovu na kampuni yoyote ya kigeni au ya ndani atafukuzwa kazi na kushtakiwa.

Aliyasema hayo wakati wa akizindua bodi mpya ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), katika Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency Dar es Salaam jana.

Fedha nyingi katika Tanzania zinapotea kwa njia ya mikataba mibovu na kesi nyingi zisizoisha mahakamani.

Alisema kwa mfano Tanesco peke yake kuna kesi zaidi ya 200 ambazo nyingi ni miradi ya watu wachache.

Waziri alisema baadhi ya watumishi wanashirikiana na makampuni ya sheria kuyaibia mashirika kwa kujipatia zaidi ya Sh milioni 200 kwa mwaka.

“Fedha nyingi katika nchi yetu zinapotea kwa kesi zisizoisha na mikataba mibovu… kesi hizo zinaifikisha bili zaidi ya Sh milioni 200 kwa mwaka na kusababisha taifa kubaki katika ufukara.

“Nimekwisha kusema ni marufuku kampuni moja kurundikiwa kesi nyingine na kampuni itakayopewa kazi hiyo lazima ishinde kesi nane kati ya 10, tofauti na hayo inyang’anywe mara moja… na tabia hii ife,” alisema Profesa Muhongo.

Kuhusu Bodi ya TPDC

Akizindua boda ya TPDC, Profesa Muhongo aliwasimamisha wajumbe wapya wa bodi kila mmoja kwa dakika mbili akiwataka waeleze uzoefu wako na jinsi watakavyosaidia kuliinua shirika hilo.

Baada ya kujielekeza waziri aliwakabidhi wajumbe hao mkoba wenye mikataba 26 ya TPDC ili waipitie na kutoa mapendekezo yao ndani ya miezi mitatu.

Alisema Novemba 30 mwaka huu atakaa pamoja nao kujadili mkataba moja baada ya mwingine.

“Hapa tuna mikataba 26 baadhi yake ni mibovu, kazi yenu ni kuipitia upya ni lazima kila mkataba ufanyiwe auditing (ukaguzi).

“Nimeambiwa kisima kimoja kinalindwa kwa thamani ya Dola za Marekani milioni 100 mpaka 150, kwa hiyo lazima bodi ipitie kwa makini suala hili ikiwezekana ulinzi huo ufanywe na jeshi letu ili fedha zibaki nchini.

“Tusije tukafanya tena mkosa kama tulivyofanya kwenye sekta ya Madani. Kampuni nyingi ni wajanja msiwaamini hata kidogo, haiwezekani mtu anachimba kwa miaka 10 bila kulipa kwa kisingizio cha fedha alizotumia.

Azuia mikataba mipya

Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo amepiga marufuku mikataba mipya hadi ya sasa itakapopitiwa upya na kujiridhisha kwamba ipo kwa manufaa ya Watanzania.

“Kuanzia sasa sitasaini mkataba wowote hadi hii iliyopo tutakapojiridhisha kuwa iko salama kwa manufaa ya watanzania.” Alisema.

Fedha za gesi na mafuta kutoingizwa Hazina

Profesa Muhongo vilevile alisema fedha zote zitakazotokana na gesi na mafuta hazitaingizwa Hazina.

Alisema hatua hiyo itaepusha fedha hizo kuchangwa na nyingine na baadaye kuchakachuliwa na hivyo kushindwa kuonekana zimefanya jambo gani.

Waziri alisema fedha hizo zinapaswa kuonekana zimefanya kitu ambacho Watanzania watajivunia kuwapo kwa raslimali hiyo.

“Fedha za gesi na mafuta hazitakwenda Hazina kwa sababu huko kuna matobo mengi. Sitaki zikachanganywe na nyingine ambazo zikienda kwenye halmashauri mwishowe tutasikia dawati moja limenunuliwa kwa Sh milioni 10,” alisema.

Azungumzia malipo ya huduma (capacity charge)

Waziri Muhongo pia amepiga marufuku mashirika yote yaliyo chini ya Tanesco kuingia mkataba na kampuni unaotaka malipo ya huma (capacity charge).

Alisema malipo hayo ni bandia na wizi wa wazi, na mtumishi yeyote atakayeingia mkataba wa aina hiyo atafukuzwa kazi na baadaye kushtakiwa.

“Ni marufuku kwa kampuni inayotaka kufanya biashara na sisi kuweka kipengele cha capacity charge, kampuni itakayotaka capacity charge ni ya kipuuzi.

“Katika sekta ya umeme kuna kampuni zinazolipwa hadi Sh bilioni mbili hadi saba kwa mwezi kutokana na malipo ya capacity charge.

“Yeyote atakayeingia na kusaini mkataba wa aina hiyo akaufute mara moja kabla haujanifikia, tutamfukuza kazi na atashtakiwa kwa sababu ni mwizi,” alisema.

Sera ya gesi na mafuta

Waziri alisema ili sera ya gesi na mafuta iweze kuandaliwa wananchi wanaoishi mikoa inayotoa raslimali hiyo wajulishwe waweze kutoa maoni yao nini kiingizwe kwenye sera hiyo.

“Tena nyinyi wataalam msiende na kuwabwagia tu hiyo draft na kuondoka, muipeleke wiki mbili kabla na baadaye mkutane nao ili waseme ni kitu gani wanataka kiingizwe kwenye sera hiyo,” alisema.

Mchango katika bajeti ya serikali

Waziri Muhongo aliyaagiza mashirika yote yaliyo chini ya wizara yake kujiandaa kuchangia bajeti ya serikali mwakani.

Alisema serikali kama mbia mkuu wa mashirika hayo lazima apatiwe gawio lake kila mwaka.

“Hata wale wanaopata hasara lazima waonyeshe kwamba katika kipindi fulani watakuwa wanatengeneza faida kwa hiyo gawio lake lazima lionekane, hatuwezi kuendelea kukusanya kodi katika viberti, bia, soda huku nyinyi mkiendelea kupokea fedha za serikali bila kurejesha gawio,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Michael Mwanda alisema pamoja na mambo mengine wanatambua umuhimu wa kukamilika kwa Sera ya Gesi Asili na umuhimu wa kuifanyia marekebisho sheria ya utafutaji na uzalishaji mafuta ya mwaka 1980 kuondoa upungufu uliopo

 
wewe ni msaliti mkubwa! Mnakatisha tamaa watu wazalendo wa kweli, huyo manji kama anakudanganya siku zake zimekwisha zakutufanya sisi wajinga watu wenye bongo kama wewe ndiyo manasababisha nchi hii kuwa masikini kwa mawazo yenu ya kibinafsi.
Many thanks. But time will tell who is right-between me and you stupid self.
 
lazma tubadilike na kumpongeza mtu anapofanya vizuri sio kila kitu ubishi usio na maana,kwa hili unaonesha jinsi ulivyo maskini wa fikra!
kaza buti muhongo!
A Conclusion based on a few data is as invalid as the person making such conclusion
 
Katiba mpya inakuja, mawaziri watoje nje ya bunge (wasiwe wabunge) au wajumbe wa kamati za vyama vya siasa i.e NEC or CC. Anaweza kuwa mwanachama lakini asiwe mbunge or m-NEC. Pia kama wanasema wamesoma lazima kuwa na evidence ya elimu yao from a credible institution. Huu muda uliobakia hadi 2015 uwe ni ndio mwisho wa kuwa na cabinet ya magumashi.

Umesema kitu cha maana sana. Wasomi wanatukanwa bila kujua kweli kuna watu wanajitambulisha kama wasomi kumbe wamefanya udanganyifu mkubwa katika kufikia level hizo walizonazo. Hata utaratibu wakuwapandisha ma-professor umegubikwa na mengi ila tu kwasababu vetting institutions zetu sijui zinafanya kazi gani (Mfano utakuta mtu kawa full profesor kwa proceedings tu!? japo TCU sasa imerekebisha sana)..Kuna wengine wamesoma kweli kwenye credible institutions lakini wanapofika nchini wanakuwa inconsistent katika profession zao na kuingilia profession zenye kulipa zaidi ambako competence yao siyo kubwa ; kwakua tu wana qualify kama PhD holders basi wanapewa majukumu ambayo ni nje ya center of their excellence matokeo yake wanavurunda..Mtu yeyote akipewa asignment nje ya taaluma yake huyo ni lay kwenye hiyo taaluma hata kama ana PhD credible kwenye field nyingine.

Ni muhimu pia kuangalia human resource management yetu maana watu wengi wamesoma michanganyiko mpaka wanakosa area of specialization..At manegerial post i.e politcal position hawa ni wazuri lakini siyo katika ku-solve field specific problems!
 
Binafsi prof.Muhongo namkubali sana kwani hua anamaanisha kile anachokisema,wasiwasi wangu ni kua anapambana na viongozi wenzake wakubwa katika nchi hii wenye uroho wa kula mali ya uma bila ya kuwafikiria watanzania wa kawaida walala hoi,hivyo naona kama ana hatari kubwa sana katiaka utekelezaji wa kazi zake,wasipomtia Gonjwa la ajabu basi hata kuuondoa uhai wake wanaweza,mafisadi wana nguvu kubwa sana kupigana na mafisadi yeye peke yake ni hatari kubwa sana kwake,hata hivyo namuombea kwa Mungu amlinda aweza kutekeleza ,malengo yake salama.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Andiko moja kwenye Biblia Linaesema tusiwe na haraka ya kuweka mikono ya baraka kwenye kichwa cha mtu, Binafsi nachelea kusema nimapema sana kuamini na kutekeleza ayasemayo pamoja na nia nzuru aliyonayo haijui rangi halisi ya chama chake cha CCM.

Lakini pia kuna lingine linasema neno ndilo liloumba vitu vyote..So kwa maneno yetu tunaumba tunachotaka kutoka kwa huyu prof Mhongo!
 
..inabidi tuwe macho kidogo hapa.

..waziri amesema kuna mikataba 26 na baadhi yake ni mibovu. halafu anawataka wajumbe wa bodi waipitie.

..sasa what happens kama wajumbe wa bodi watatofautiana na mtizamo wa waziri na kumrudishia majibu kwamba mikataba yote ni mizuri??

..kama waziri tayari ameona kuna mikataba mibovu, kwanini asitoe amri mara moja kwamba irekebishwe??

..tusiwe na haraka ya kushangilia ushindi. tusubiri miezi mitatu tuone kama kuna mikataba itarekebishwa, na zaidi ni mikataba mingapi.
jokaKuu,
Hapo mimi naona waziri amewatega wajumbe wa bodi. Kama watarudi waseme mikataba ni mizuri itabidi wamweleze ni mizuri kwa vipi. Kumbuka dakta Muhongo mwenyewe atakuwa ameshaipitia mikataba hiyo kama mwalimu wa darasani. Anataka kuwashirikisha wajumbe wa bodi katika uamuzi wa wizara yake, which is a good thing, na pia kupata fursa ya kuona role ya wajumbe wa bodi katika upitishwaji wa mikataba nchini. I think the professor is smart.
 
Back
Top Bottom