Tanesco yatangaza mgawo; kuanza mara moja!

Mie nauliza, je, tunaweza kufanya mgomo baridi wa kuinyima TANESCO mapato, kwa kupunguza - kwa lazima - matumizi ya umeme, kwa sisi wateja wa LUKU? Kwa mfano, wanapoturejeshea umeme, tunaongeza 2 hours za mgomo, juu ya hizo 4 hours zao wanazosema, kwa hiyo jumla tunaongeza 4 hours, 2 hours asubuhi na 2 hours mchana, for a total of 12 hours kwa siku! Je, inawezekana? Tuone nini kitafanyika?

Mimi najua kwamba hii power crisis ni artificial, na hapa kuna njama za kutaka kununua hiyo mitambo ya umeme ili hao mafisadi wapate 20 percent zao! Sasa nini kifanyike tuwaoneshe kwamba tumechukizwa na ufisadi huo? Can we BOYCOTT TANESCO?

Did I get you right?
this could be Abunuwasi trick of new era
 
Mabya zaidi, inaelekea hajifunzi lolote katika huko kutalii kwake!

Presidaa yuko Comoro anafanya mpango tuungane nao kalakabagho akirudi magogoni hakuna mgao sisi wa yombo tunapigwa kabali na vibaka. Solution Buy used gen(dowans) hahaaaaa kweli njii hii imetawaliwa!!!
 
We are being blackmailed and it wont stop here. There is only one way to deal with a blackmailer...get rid of him!

DOWN WITH DOWANS! DOWN WITH TANESCO!
 
.....Hatuna serikali. Ni majambawazi tu yamekalia viti vya enzi yakitaka sifa yasizostahili.

...Imeandikwa...Mkiona chukizo la uharibifu limekalia patakatifu basi tambueni kuwa ule mwisho u karibu...
 
...Leo wanataka mnunue Dowans.. ili wawape umeme kesho watataka mfanye nini? !!

NO DOWANS, NOT BOWING DOWN!

Shehe Naambiwa mitambo imeshanunuliwa kitambo ila wanasaka njia ya kuhalalisha manunuzi.
wameshika pabaya sana this tyme
 
Matatizo yetu makubwa inaonekana kweli ni mentality ya kujinufaisha mmoja mmoja, come rain come sun. Mficha maradhi mauti humuumbua. Hili la Tanesco ni kama mchezo wa kuigiza.

1. Mwaka jana kuvunja mkataba na Dowans na CEO wa Tanesco kusema umeme wa Dowans hauhitajiki.

2. Baada ya miezi sita au saba baada ya kuvunja mkataba CEO yule yule wa Tanesco anarudi na kusema mgawo ni lazima tusiponunua mitambo ya Dowans

3. Kama wiki mbili baadaye waziri anakuja na anatangaza kuwa mjadala umefungwa na CEO wa Tanesco anaonya kuwa mgawo itakuwa lazima.

4. Kama wiki mbili baadaye, mgawo unaanza.

My pick:
Wakati mkataba wa Dowans unavunjwa hatukuwa na plan B. Maneno kuwa umeme unatosha ilikuwa uongo ili kuridhisha matakwa ya wakati ule. Tatizo la umeme Tanzania linajulikana hata Dowans ingeendelea, mgawo huwa ni suala la muda wowote kwa sababu hatuna mipango, na iliyopo ni ya kizushi.

Hili alilozungumzia Dr. Slaa la rais kuzungumzia mambo ambayo hayakuwa na kila mtu anaficha kichwa chake mchangani ni hali halisi ya nchi yetu. Viongozi wanapoongea hawajui kuwa maneno yao hayatakiwi kuwa ya kubabaisha. Kwani ni mara ya kwanza kutangaziwa mwisho wa mgao? Rais aliongea kuridhisha matakwa ya wakati ule tu.

Kwenye ishu yenyewe ya umeme kinachonikera ni hili suala la capacity charge. Capacity charge hulipwa ikiwa kampuni imezalisha au haijazalisha. Kusema ukweli unaweza kununua majenereta feki ukayaleta na siku zote yakawa mabovu, ukawa unakusanya hela za capacity bila mgogoro. Hivi hii huwa tunaigawa kwenye cost tunaposema umeme wa Songas kwa mfano tunalipa x per KwH?? Kwa sababu ikiwa hatujumlishi, tunajidanganya kuwa tunanunua umeme kwa hela kadhaa per unit, kumbe gharama halisi ni mara mbili.

Ikiwa Tanesco walishindwa kuzalisha umeme wao, tukasema solution ni kutumia independent power producer, na sasa inaonekana independent power producer si solution kwa sababu wana bei kubwa mno (capacity charge plus per unit tariff), sasa tutaponea wapi????

Ni ama tuache hawa IPP wafilisi, au tukose umeme kabisa na uchumi u colapse. kote hakuendeki.

BASI TUBINAFSISHE SERIKALI, TULETE RAIS NA MAWAZIRI KUTOKA NJE!!!
 
Indipendent power producer ni solution katika dunia ambayo haijatawaliwa na ufisadi. Sasa ufisadi umesababisha kununua umeme wa Independent Power Producers (IPP) kuwa kama wendawazimu. Nadhani hili hata WB na IMF hawakulifikiria.
 
...wizi mtupu
kama wamesema ni saa nne ktk siku ya mgao in real sense piga hesabu ya 4 x 4 - 24 utapata 8 ambapo mtakuwa mnapata umeme kwa saa 8 kwa siku.
Si mlikataa kuwa dowans isinunuliwe? safari hii mtaandamana kwa shinikizo kwamba inunuliwe.
Nchi hii kwa uzalendo wa kifisadi naivulia kofia.

Hii ndio Tanzania, mitambo imeharibika Ghafla!!
 
Ethiopia wanajenga Dam la USD 1.7 Billion by 2011 litakamilika na watazalisha over 2500 Megawats na ingine wataexport to Kenya! Wamekataa katakata kuwasikiliza WB na IMF inaonekana wamepata mkopo toka China!

Sudan nao pia wamefungua Bwawa kubwa sasa juzi kwa mkopo toka China!

Yet sisi bado tunazungumzia kununua Dowans ya Magawats sijui 50!!!!

Hivi Watanzania tutaamka lini???

Mradi Mkubwa wa Umeme utaanza lini?
 
Songas wamesema wana uwezo wa kununua mitambo mipya, si waombwe walete hiyo mitambo haraka? Umeme ni muhimu mno kwenye uzalishaji, kukatwa umeme masaa nane tena kwa Dar, nchi itapata hasara kiasi gani?
 
Songas wamesema wana uwezo wa kununua mitambo mipya, si waombwe walete hiyo mitambo haraka? Umeme ni muhimu mno kwenye uzalishaji, kukatwa umeme masaa nane tena kwa Dar, nchi itapata hasara kiasi gani?

hakuta kuwa na hasara yoyote ile, kwa Tanzania wanaotumia umeme nchi nzima ni aslimia 10 tu!!
 
Ethiopia wanajenga Dam la USD 1.7 Billion by 2011 litakamilika na watazalisha over 2500 Megawats na ingine wataexport to Kenya! Wamekataa katakata kuwasikiliza WB na IMF inaonekana wamepata mkopo toka China!

Sudan nao pia wamefungua Bwawa kubwa sasa juzi kwa mkopo toka China!

Yet sisi bado tunazungumzia kununua Dowans ya Magawats sijui 50!!!!

Hivi Watanzania tutaamka lini???

Mradi Mkubwa wa Umeme utaanza lini?

nshasema nimegoma kufikiri
unajuwa hawa watwana wanadhalilisha fikra zetu kwa vitu mkweche kama dowans ila hawana plans za kuiangalia kesho itakuwaje.
Tuna wanasiasa hatuna wataalam. Watu wanapiga siasa mpaka jikoni
 
Ethiopia wanajenga Dam la USD 1.7 Billion by 2011 litakamilika na watazalisha over 2500 Megawats na ingine wataexport to Kenya! Wamekataa katakata kuwasikiliza WB na IMF inaonekana wamepata mkopo toka China!

Sudan nao pia wamefungua Bwawa kubwa sasa juzi kwa mkopo toka China!

Yet sisi bado tunazungumzia kununua Dowans ya Magawats sijui 50!!!!

Hizi Watanzania tutaamka lini???

Mradi Mkubwa wa Umeme utaanza lini?

Mzalendohalisi,

Hiyo miradi mikubwa mikubwa ya Wachina iangalie sana mkuu, itakuja itokea Afrika puani. Hawa jamaa hii miradi mikubwa mikubwa hata kule kwao inawaletea matatzo sasa ndio iwe kwetu Afrika? Tuwe waangalifu sana.

Kama inawezekana tuwe na miradi midogo midogo ili hata kukiwa na matatizo sehemu moja basi effect yake haiwi kubwa sana.

Kwa nchi maskini kama za kwetu ni hatari sana kutegemea hii miradi mikubwa mikubwa. Kama ule mradi wa Singida utafanikiwa itakuwa nzuri, changanya na umeme wa maji, imarisha Kiwira na ule mgodi mwingine wa makaa ya mawe, ongezea technology ya solar kwenye miji midogo midogo, nafikiri ndio strategy nzuri.

BTW: Nilikuwa najua IMF wanatuonea Afrika, nimeona walivyowabana Ukraine, Slovakia na Iceland, kumbe Mwarobaini ni ule ule.
 
Back
Top Bottom