TANESCO yasisitiza hakuna mgawo

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
Licha ya baadhi ya maeneo katika jiji la Dar es Salaam kukosa umeme hivi karibuni, lakini Shirika la Umeme nchini (Tanesco), limesisitiza kuwa hakuna mgawo wowote utaofanyika hivi sasa.

Akizungumza na NIPASHE Jumamosi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Felchesmi Mramba, alisema licha ya maeneo kadhaa kukosa umeme hivi karibuni, lakini tatizo hilo lilitokana na matatizo ya kiufundi ama matengenezo ya mitambo yake na siyo mgawo.

"Wananchi wasiwe na wasiwasi, kwani shirika linawatoa hofu tatizo la mgawo wa umeme hivi sasa hakuna, lakini iwapo sehemu umeme unakosekana hilo ni tatizo la kiufundi ama utengenezaji wa mitambo ama dharura yoyote imetokea," alisema Mramba.

Mramba alifafanua, mgawo wa umeme unakuwepo pale inapolazimika mgawanyo wa matumizi ya umeme uwepo, lakini kwa sasa hatuna mpango huo kwani nishati hiyo inapatikana kwa kutosha.

Alisema sehemu ambayo umeme umekatika kwa muda mrefu, si tatizo la mgawo bali ni marekebisho ya mitambo inafanyika ama hitilafu ya dharura imetokea.

"Kwa mfano hivi karibuni pale mjini, kuna gari liligonga nguzo kubwa na kusababisha kukosekana kwa umeme kwa saa nane maeneo yote ya njia ya kwenda Mkuranga, lakini baadhi ya wateja wetu waliamini ni mgawo huo…ni matatizo tu ya kiufundi," alisema.

Hata hivyo, alisema hivi sasa shirika lake linajitahidi kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari kila tatizo la kiufundi linapotokea ili kuwaondolea hofu.

Hivi karibuni wakazi wa Makongo Juu, Tabata walilalamikia katizo la umeme katika makazi yao bila kupewa taarifa huku wakiamini shirika hilo limeanza kutoa mgawo bila taarifa.


CHANZO: NIPASHE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom