Mwana Mtoka Pabaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 15,118
- 16,470
hovyo kabisa.
Hawa si ndo wanaimba wimbo kuwa hawana hela?
Upuuzi gani huu wanafanya?
Sisi huku tunapandishiwa bili wao wanapewa bure. Billions, ili kulinda ndoa au?
hovyo kabisa.
Hawa si ndo wanaimba wimbo kuwa hawana hela?
Upuuzi gani huu wanafanya?
TANESCO wana madeni makubwa halafu wanafutia wengine madeni kisa Muungano wakati wazanzibari wanasema tunawanyonya, kama ni hivi bora Muungano ufe
Lini Zanzibar walilipa umeme tangu umevushwa? Je, bilioni 50 wamelipa kiasi gani wanachodhani ni halali? wamesamehewa zote. Zbar hawajalipa umeme, wanalipiwa na mkulima na manyakazi wa Tanganyika. Hawajalipa elimu ya juu wanalipiwa na mMtanganyika! Mishahara inatoka hazina muulize Mramba na Mkulo. Kama hawawezi kulipa mshahara watawezaje kulipa umeme? Hiyo ya Richmond n.k ni kutafuta sababu tu kwasababu mgao hawaujui. Wamewahi kusamehewa umeme hata kabla ya Richmond.Walichokuwa wanakidai Zanzibar kina uhalali, na wala hawajafanyiwa hisani. Walikataa kupandishiwa bei ya umeme kwa hoja ya kwamba ongezeko hill limechangiwa zaidi na uzembe, ufisadi na kutokuwajibika kulikofanywa na Tanesco na wadau wake, na si kutokana na mfumuko wa bei. Niliwahi kumsikia mwakilishi mmoja akihoji kuwa vipi madhara ya rushwa iliyoliwa na mtendaji wa Tanesco ailipe mzanzibari??? Hivyo wakataka iwekwe unit cost ya kuzalisha umeme bila ya kuingiza fidia wanazolipwa Richmond na gharama nyenginezo wanazopata Tanesco kwa kuingia mikataba mibovu
Ikumbukwe katika mikataba kuna kipengele kinachoeleza kuwa upande mmoja hautowajibika kutokana na uzembe (negligence), uharibifu (damages) au ufisadi (corrupt practices) utakaofanywa na upande wa pili au washirika wake. Kimantiki Zanzibar wanahoji uhalali wa ongezeko la bei ya umeme kuanzia mwaka 2008 na wako tayari Tanesco walete mchanganuo wao wa gharama za matumizi ili ibainike kwa kiwango gani ongezeko limechangiwa na mfumuko wa bei na kuongezeka kwa gharama za maisha, na kwa kiasi gani limechangiwa na ubadhirifu na utendaji mbovu, ili kila upande ubebe msalaba wake mwenyewe
Bora muungano uvunjike kuliko hii hasara tunayoipata
Ukiwa mjinga ni bora unyamaze,
Kwa wasiofahamu, ngoja niweke wazi.
Tanesco haijaisamehe zanzibar isipokuwa ni mkataba baina ya nyerere na Karume waliokubaliana kuhusu nishati ya umeme.
Ikumbukwe kuwa zanzibar ilikuwa na vyanzo vyake vya umeme kama generator na mashine maalumu zilizopo ndani ya meli, na umeme ililetwa toka nchi za arabuni. Baada ya kuungana Nyerere akamuomba karume asitishe ule mpango na kumuahidi kuwa watapata umeme wa gharama nafuu kama ule wanaoupata znz.
Kama hamjui ulizeni sio mkurupuke.. HUU NI MKATABA NA SIO FADHIRA.
1. kama sii kuwa na nhi moja ni bora Tanganyika na Zanzibar zikawa huru na kujiunga na Afrika Mash ....ni tija kubwa kuliko Muungano wa sasa!
2. Bara wanaburuzwa ...angalia Mtoto wa Mwinyi mzanzibari NI WAZIRI WA AFYA BARA!!!
SASA KUHU BARA MUUNGANI INATUSAIIA NINI?
Hili si deni la leo au jana. Tangu umeme uvushwe Wazanzibar wamekuwa wanatumia bure Baru baru! Kinachouma si wao kupewa zawadi, ni kauli zao za kinafiki kuwa hawafaidiki na muungano huku wakijua umeme wanaotumia ni zao la muungano.WaBara kama imewauma Kwanini msiende mahakamani kama mlivyofanya kwa ile kuzuia TUZo ya Dowans kulipwa mabilioni na Tanesco?
Acheni kulalama. Kama imewauma mahakama zipo wazi kwa ajili yenu.
Walichokuwa wanakidai Zanzibar kina uhalali, na wala hawajafanyiwa hisani. Walikataa kupandishiwa bei ya umeme kwa hoja ya kwamba ongezeko hill limechangiwa zaidi na uzembe, ufisadi na kutokuwajibika kulikofanywa na Tanesco na wadau wake, na si kutokana na mfumuko wa bei. Niliwahi kumsikia mwakilishi mmoja akihoji kuwa vipi madhara ya rushwa iliyoliwa na mtendaji wa Tanesco ailipe mzanzibari??? Hivyo wakataka iwekwe unit cost ya kuzalisha umeme bila ya kuingiza fidia wanazolipwa Richmond na gharama nyenginezo wanazopata Tanesco kwa kuingia mikataba mibovu
Ikumbukwe katika mikataba kuna kipengele kinachoeleza kuwa upande mmoja hautowajibika kutokana na uzembe (negligence), uharibifu (damages) au ufisadi (corrupt practices) utakaofanywa na upande wa pili au washirika wake. Kimantiki Zanzibar wanahoji uhalali wa ongezeko la bei ya umeme kuanzia mwaka 2008 na wako tayari Tanesco walete mchanganuo wao wa gharama za matumizi ili ibainike kwa kiwango gani ongezeko limechangiwa na mfumuko wa bei na kuongezeka kwa gharama za maisha, na kwa kiasi gani limechangiwa na ubadhirifu na utendaji mbovu, ili kila upande ubebe msalaba wake mwenyewe
Wilaya ya Maswa wamekosa maji takribani wiki moja sasa baada la idara ya maji wilayani humo kushindwa kulipa deni la mil 25 leo hao wanasamehewa mabilion..kwanini tusidai Tanganyika yetu