Tanesco W'anza Kuchokonoa - Muungano

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Zanzibar hatarini kukumbwa na giza totoro tena

2008-07-01 11:29:03
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar


Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), limeiandika barua Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) likitishia kuikatia huduma ya umeme.

Barua hiyo imeeleza kuwa, hatua hiyo inatokana na SMZ kutotumia viwango vipya vya ununuzi wa nishati hiyo.

Akizungumza na Nipashe mjini hapa, Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Bw. Mansour Yussuf Himid alisema walipokea barua hiyo mwishoni mwa wiki.

Tishio hilo linakuja siku chache baada ya Zanzibar kumaliza kipindi kigumu cha zaidi ya mwezi mmoja cha kukaa gizani kutokana na hitilafu iliyotokea katika kituo cha Ras-Fumba.

Kituo hicho kilichoko nje ya mji wa Zanzibar, hupokea umeme kutoka Bara kwa kupitia baharini.

Hata hivyo, Waziri alisema tishio hilo lililotolewa na uongozi wa Tanesco linakwenda kinyume na makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa pande mbili za Jamhuri ya Muungano kati ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Bw. Edward Lowassa na Waziri Kiongozi, Bw. Shamsi Vuai Nahodha.

Alisema baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (EWURA) mwezi Desemba, mwaka jana, kupandisha gharama za malipo ya umeme, Zanzibar ililalamika kuwa mamlaka hiyo haina nguvu kisheria ya kuipangia Zanzibar viwango gani vya bei vitumike kwa vile siyo taasisi ya Muungano.
_________________________________________________________

Yaani hata Wazenji hawajaanza kupata nuru kamili ya macho jamaa wanatishia ila siamini kama wana ubavu wa kuwazalilisha Wahafidhina na Serikali yao maana ,safari hii sio wataomba warudishiwe ASP bali watavunja kila kitu. Bila ya ridhaa ya mtu yeyote. Nasubiri sehemu ya pili ya giza totoro.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom