TANESCO wanakoelekea sio kuzuri!

Codon

JF-Expert Member
Dec 16, 2011
629
93
Wana Jf nisaidieni mgao gani unakuwa Asubuhi then mnarudishiwa 1hr mnakatiwa masaa mengine 8!Naniline moja tu(Nodic)!Wasio ifahamu inanzia pale kimara bucha upande wakushoto kama unatoka mjini mpaka karibu na kibamba,pia ikifika kimara mwisho inaanza kula pande zote mbili ndio inaenda mpaka maeneo machache yakibamba!Jamaa watanesco wanakata sana hii line sijui haina watu wakubwa?Tumechoka sasa.
 
tunarudi tulikotoka tanzania ni asilimia isiyozidi kumi tu ya watu ndio wanaona miaka inaenda mbele, sisi wengine naona inarudi nyuma. Na karibu tutafikia zama za stone age!
 
Hahaaa!Kweli wewe!Namna hii?TRC,TAZARA kwisha!Elimu bure sasa mkopo!Wewe umenifungua macho.Siwapigii tena simu.HIVI 2015 mbona mbali mno?
 
Mie usiku huu wamekata na kurudisha ghafla TV, Fridge imeungua, nimepiga customer care wanatoa pole tu, na wamekata tena, hapa ni maeneo ya mbezi beach- jogoo, giza na joto hakulaliki, kesho unaamka kama mgonjwa, watanzania hebu tuungane huyu ngeleja na watendaji wake watoke pale, EWURA ndio sijui wako wapi! Nimeichukia serikali yangu kupita kiasi, huwa sipigi kura ila 2015 yangu moja lazima iongezeke. Mtu unafikia kuchukia uraia wako! Jamani TANESCO na wahusika wote mnatupa shida sana.
 
Pole sana,sisi maeneo yakimara toka asubuhi mpaka mida hii no Ngereja at all!
 
My friend umesikia kuhusu solar power,ni heri ukaanza kujipanga kuitumia,

Yani ndiyo dawa tu kwa kujinusuru na giza tororo linakuja!
Na sijui Wajomba zangu hapo kjjn watatumia nini maana mafuta ya taa ni iko juu sawa na petrol super.

Kwa kweli serikali ya magamba ni JANGA KWA TAIFA LETU!

Ila hakika MWISHO wao waja!
 
Na bado na huu ni mwanzo picha ndo kwanza linaanza watu mwang'aka je kwa style hii mwisho wa picha 2015 tutafika kwelii??.

Bora yenu nyie usiowaka kabisa sis huku mwenge mpaka sasa watu wamekula hasara ya kutosha tv,radio,freg,tube light zimabutuka kweli kweli.
Mara umeme unakuwa mdogoooo ukirudi saa unakuja wa nguvu sana tena wakutosha kama dk 5 hivi unafanya uharibifu then unasepa.
Mafundi now ndio mda wenu wa ku enjoy bana.
 
Huku Kigamboni wameshakata tangu saa nne asb. Hatujui watarudisha saa ngapi. Bila shaka huu ni mgao...Tanesco tuambieni sababu za mgao huu tunaoendelea nao sasa na lini utaisha.

Tumo ndani ya shida hii tangu mwaka 2006 na hatujui lini itaisha. Tunalazimishwa shida hii tuizoee kama tulivyoizoea shida ya maji.

Matatizo ya maji yalianza kidogo kidogo mwaka 1987, wakati huo Naibu wa Wizara ya Maji na Madini na Nishati alikuwa Hayati Ditopile Mzuzuri aliahidi kumaliza tatizo la maji kwa kuvuta maji toka Mzenga na kutoka mto Rufiji. Lakini mpaka leo tatizo bado unsolved na tunaishi nalo na hatujui litaisha.

Naamini hata umeme itakuwa ni vivyo hivyo....
 
Tunapaswa kurudi kwenye meza na kuopanga upya kuhusiana na tatizo la umeme. Tuliahidiwa wakati wa bajeti mipango kabambe na kuelezwa kuwa ifikapo Disemba mwaka jana, mgawo utakuwa ni historia. Tanesco hivi sasa haitaki kukiri kwua kuna mgawo lakini sisi wateja wake tunapata umeme kwa mgawo. Ni dalili kwua Tanesco imeshindwa na serikali haitaki kukiri udhaifu wake wa kushindwa kutekeleza kile ilichotuahidi kupitia bajeti.
najiuliza, kama asilimia kumi tu ya watanzania ndio wanaopata huduma ya umem na hali uiko hivi, je ikiwa asilimia 50 ya watanzania wanapata umeme hali itakuwaje? na katika hali kama hii, hivi hizi ahadi za kuongeza kiwango cha watanzania wanaotumia umeme si ni ndoto zisizotekelezeka?
 
Mie usiku huu wamekata na kurudisha ghafla TV, Fridge imeungua, nimepiga customer care wanatoa pole tu, na wamekata tena, hapa ni maeneo ya mbezi beach- jogoo, giza na joto hakulaliki, kesho unaamka kama mgonjwa, watanzania hebu tuungane huyu ngeleja na watendaji wake watoke pale, EWURA ndio sijui wako wapi! Nimeichukia serikali yangu kupita kiasi, huwa sipigi kura ila 2015 yangu moja lazima iongezeke. Mtu unafikia kuchukia uraia wako! Jamani TANESCO na wahusika wote mnatupa shida sana.


mbaya zaidi wametiongezea gharama za umeme kwa asilimia 40. nilifikiri utendaji utaboreshwa kumbe hamna kitu. jamani kweli sisi tunafaa kuishi misituni tu huku kwingine tunajingángániza hatukuwezi tuwaachie wazungu tu.
 
kiongozi mbona hawa jamaa walishafika pabaya siku nyingi...............................!
Mi nakushangaa ukisema wanapoelekea sio kuzuri wakati wameshafika huko ..................................!
wanaaboa sana hawa washikaji........................1
 
Kuna kiongozi mmoja wa kisiasa wa chama cha upinzani alicoment kauli ambayo mpaka leo sitaisahau Alisema hivi "watanzania wenzangu huwezi kuondoa balaa bila kutokea balaa"
 
TANESCO hawana maana yoyote. Na ili mradi wameamua hawatuelezi taratibu zao za Washa Zima ili vitu vyetu viungue, kazi zetu ziharibike na kwa ujumla kuathiri maisha yetu dawa ni kuwatelekeza, tuandamane shirika lote wapewe redundancy, Mawaziri husika wajiuzulu na wale wote wanaolamba pesa yetu tunapolipia bill za umeme k.m. EWURA, TRA. Wanalipwa mishahara ya nini? Nampongeza jamaa aliyempa notisi Fundi wa Tanesco aliye mlaji kwa jinsi alivyo na makabrasha mwili mzima. To hell
with you Tanesco people and to hell with Nishati people wherever you are. May mad dogs chew your ......les and ...nts.
 
Kigamboni wameshakata saa sita na dk 46 mchana.

Mvua zote hizi bado tu tunashida ya umeme!!!!????
 
Inaelekea huko tuendako umeme utapatikana kwa siku 2 au 3 tu kwa wiki nzima. Siku za mgao zinaweza kuwa J3, J5 na Ijm au J4, Alh na J2. Naona kadri tunavyovumilia ndivyo hali inavyozidi kuwa mbaya zaidi.

Sijui mwaka 2015 mtu atanishawishi vipi nikipigie kura chama chenye rangi inayofanana na Tanesco!!!???
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom