TANESCO wabwagwa na Dowans mahakamani

Wabongo tumezidi siasa na kurukia mambo,jazibz zinatuponza kukurupukia mambo bila kujua mathara, Kanini serikali ya sisi mmm haina msimamo?
 
Kuna watu hawafatilii ukweli wa habari wanakurupuka tu.Mleta mada sijui katumwa na nani awatie watu pressure?Pingamizi la Dowans kuhusiana na tanesco ndilo limetupiliwa mbali na TANESCO wanaruhusiwa kupinga malipo hayo ya DOWANS
 
Tusipoangalia Dowans itatusumbua sana na hili deni litakuwa linaongezeka kila kukicha!
 
Ikulu wameajiri watu wasiojua kingereza vizuri.. je huko tbc uhuru unatagemea nini? mwandishi kaenda mahakamani kusikiliza kesi halafu hakuambulia kitu ..karudi kapotosha
 
kitendawili, kwa kuwa downs ni ya watanzania,
na kwa kuwa tunauhakika kuwa wanatudai kwa siri,
kwa maoni yangu,sakata hili ni kama kutoa fedha ktk mfuko wa kulia na kuingiza ktk mfuko wa kushoto wa mtu huyo huyo aitwaye tanzania - shamful and terrible.
 
LAKINI MBONA MWANA NCHI WAMEANDIKA HIVI:

Mahakama Kuu yakubali Tanesco kuipinga Dowans
Monday, 20 February 2012 18:46
0digg

James Magai
MAHAKAMA Kuu Dar es Salaam imerejesha matumaini kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) baada ya kutupilia mbali pingamizi la Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans dhidi ya maombi yake ya kibali cha kukata rufaa.

Tanesco iliwasilisha maombi mahakamani hapo kutaka kibali cha kukata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu ya mahakama hiyo iliyoamuru kusajiliwa kwa tuzo ya Dowans ya Sh94 bilioni, iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC).

Hata hivyo, Dowans nayo kupitia kwa wakili wake, Kennedy Fungamtama iliweka pingamizi dhidi ya Tanesco ikiiomba mahakama hiyo iinyime kibali hicho cha kukata rufaa kwa madai kuwa haina haki ya kisheria kupinga hukumu hiyo.

Lakini katika uamuzi wake jana, Jaji Dk Fauz Twaib alitupilia mbali pingamizi la Dowans akisema Tanesco inayo haki ya kukata rufaa.

Kwa mujibu wa taratibu za kesi ya migogoro ya kibiashara, kama mshindwa tuzo akitaka kukata rufaa kupinga tuzo iliyotolewa kwa mshinda tuzo, anawajibika kwanza kuomba kibali cha kukata rufaa hiyo kwa mahakama iliyotoa tuzo hiyo.

Hata hivyo, katika uamuzi wake, Jaji Dk Twaib alisema kwa mazingira ya kesi hiyo, Tanesco haikuwa na haja ya kuomba kibali mahakamani hapo ili kukata rufaa hiyo na kwamba ingeweza kutumia utaratibu wa kawaida tu.

Uamuzi huo unatoa matumaini kwa Tanesco kuanza harakati za kuzuia kisheria malipo ya Sh110 bilioni ambayo inapaswa kuilipa Dowans baada ya hukumu ya ICC.

Akizungumza baada ya uamuzi huo, Wakili anayeitetea Tanesco, Dk Alex Nguluma kutoka Kampuni ya Rex Attorneys alisema kutokana na uamuzi huo sasa watakwenda kukata rufaa moja kwa moja Mahakama ya Rufani kupinga hukumu hiyo.

Hukumu ya ICC

Novemba 15, 2010 AICC, chini ya Mwenyekiti, Gerald Aksen akisaidiwa na wasuluhishi Swithin Munyantwali na Jonathan Parker, ICC iliiamuru Tanesco iilipe Dowans fidia ya Sh94 bilioni, kwa kuvunja mkataba baina yao kinyume cha sheria.

Kutokana na uamuzi huo, Januari 25, 2011 Dowans iliwasilisha maombi mahakamani hapo ikiomba tuzo yake hiyo isajiliwe ili utaratibu wa ulipwaji wake uwe na nguvu ya kisheria.

Hata hivyo, Tanesco kupitia kwa mawakili wake, Rex Attorneys kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliwasilisha pingamizi la usajili wa tuzo hiyo Februari 9, 2011.

Lakini, Septemba 28, 2011, Jaji Emilian Mushi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam aliamua tuzo hiyo ya Dowans ya Sh94 iliyotolewa na ICC isajiliwe na kuwa hukumu halali ya mahakama hiyo.

Katika uamuzi wake, Jaji Mushi alikubaliana na hoja za Dowans na kutupilia mbali pingamizi la Tanesco na kuamuru tuzo hiyo isajiliwe na kuwa hukumu halali ya mahakama hiyo.

Jaji Mushi alisema baada ya kupitia mwenendo na hoja za pande zote, alibaini kwamba si sawa kwa mahakama hiyo kuingilia uamuzi wa ICC.

Alisema kwa kufanya hivyo ni kuruhusu kuhoji tena masuala ya kiukweli na ya kisheria ambayo pande husika zenyewe kupitia kwa makubaliano yake ziliyakabidhi kwa ICC kuyachunguza na kuyaamua.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

 
Kwani Dowans wameshinda leo kesi? Wameshinda toka mahakama ya kimataifa ya biashara. Makanjanja wa sheria ndio walikuwa wanachelewesha malipo kwa Dowans kwa kujidai kuweka pingamizi.

"Mahakama" waliyo "shinda" Dowans sio mahakama kama watu wengi wanavyofikiri, ni mahakama ya usuluhisho ya kibiashara ambayo ni ya hiari kwa pande zote mbili na muhimu zaidi haina nguvu zozote kisheria. Kwa hiyo maamuzi ya mahakama hiyo hayna uzito wowote kisheria. Kwa kifupi Tanesco na Dowans wanacheza mchezo wa kuigiza kwa niaba ya Watanzania.
 
"Mahakama" waliyo "shinda" Dowans sio mahakama kama watu wengi wanavyofikiri, ni mahakama ya usuluhisho ya kibiashara ambayo ni ya hiari kwa pande zote mbili na muhimu zaidi haina nguvu zozote kisheria. Kwa hiyo maamuzi ya mahakama hiyo hayna uzito wowote kisheria. Kwa kifupi Tanesco na Dowans wanacheza mchezo wa kuigiza kwa niaba ya Watanzania.

Makataba wao na mingi ya Kimataifa huamuliwa na hiyo mahakama na inatambulika kisheria na nchi zote wanachama na usijidai maamuzi ya mahakama hiyo hayana uzito. Tena yana uzito kweli kweli kuliko hata mahakama yako.

Usitake kupotosha jamii, tutakushushia sheria zao hapa ili uelewe.

Kwa kukujuza tu. Dowans, watalipwa kwani hawana makosa hata kidogo. Mahakama yoyote ile duniani ni lazima washinde.

Hakuna kesi ya kushinda TANESCO wala Tanzania. Ingekuwa hawajaleta mitambo ndio, ingekuwa haijafanya kazi (mibovu) ndio. Lakini kwa mujibu wa mkataba wao, hata ungekuwa wa maneno tu bila maandishi, ni lazima washinde. Kwanini umewapa viwanja vyako? wakafunga mitambo uka saini kuwa imekuwa "tested and commissioned"? ikafaya kazi, ukane baadae, ukijidai oooh siitaki. Huitaki? kwanini uliruhusu ije, ifungwe, iwashwe? ili uwadhulumu?

Hapo hata kama hamna mkataba wa maandishi inakula kwako. Tena unalipa na gharama zote za kesi na interest juu.

Hapa Watanzania tusijidanganye, hivi vi kesi kesi ni kujizidishia gharama tu. Kesi za biashara za kimataifa hazina mchezo.

Na hiyo mahakama unayosema haina uzito, ukikataa hukumu zake, unawekwa kwenye bllack list ya kibiashra za kimataifa, hapo ndio unaweza kukosa hata spare za pasi yako nyumbani. Hapo sasa.

Muulize Nyerere alifanywa nini na Tiny Rawlings (LONRHO) alijidai kucheza na kampuni yake. Mwenyewe ilibidi akubali yaishe, aliminywa mbavu kila pembe ya dunia. Haikuchukua hata miaka miwili, akanywea, na alisema yeye hageuki nyuma atakuwa jiwe. Alimeza matapishi yake.

Usicheze na hizi biashara za kimataifa, si ulimuona yule mama Kilintoni akitembelea Ubungo? uanfikiri alikuja kucheza mdundiko yule? baada ya kuja tu yeye, mitambo imewashwa na kazi inafanya na kuuzwa (kimagirini) imeuzwa na kesi inaendelea. Wewe kalaga-baho.
 
Mbona tushaanza kulipa siku nyingi, si ndio ile 42% iliyoongezwa na Tanesco, Haina shida tutalipa tu, Hasara Roho Pesa Makaratasi Tz tunayo mengi.
 
Back
Top Bottom