Tanesco: Vintanzi vya mikataba vinatuua

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
885
60
Send to a friend
WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wamesema shirika hilo halitaweza kwenda mbele iwapo serikali haitaliondoa kwenye vitanzi vya mikataba ya kifisadi.

Walitoa dukuduku hilo jana walipokutana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kwenye jengo la Tanesco makao makuu, Jijini Dar es Salaam. Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi hao, Mwenyekiti wa Majadiliano wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwandani, Biashara na Taasisi za Fedha (Tuico), Abdul Mkama.

“Tutashirikiana na Mkurugenzi wetu bega kwa bega kuhakikisha shirika halifii mikononi mwetu, tunaweza kushindana katika biashara ya umeme ikiwa serikali itatuondoa katika mikataba mibovu,” alisema Mkama.

Alitaja mikataba ambayo imeliathiri shirika hilo kimaendeleo ni wa IPTL, Richmond, Songas, Atmus na uuzaji holela wa mali za Tanesco. Mali zilizouzwa kiholela ama kutolewa tu kama sadaka alizitaja kuwa ni majengo yaliyotolewa, kiwanda cha Kiwira na shamba la kuzalisha miti ya kutengenezea nguzo na nyaya za umeme la Kiwira.

Akizungumza kwenye ziara hiyo, Mkurugenzi wa Shirika hilo, William Mhando, alielezea shirika kwa sasa limeanza kupumua na dalili zinaonekana kwa kupunguza hasara. Alisema hasara imepungua kutoka bilioni 168 mwaka 2006 wakati likiendeshwa na Net Group Solutions mpaka kufikia bilioni 5, mwaka 2009.

Waziri Ngeleja, hakuzungumzia kuhusu udhaifu wa serikali katika mikataba inayoifilisi Tanesco na badala yake akasema waongeze ubunifu ili kuongeza mapato.

“Hakuna ubishi kwamba wananchi wamekosa imani na shirika, wizara, hatutakiwi kukata tamaa badala yake tutekeleza mipango tuliyojiwekea ili turejeshe imani yao," alisema Ngeleja. Alitamba kuwa serikali kwa kushirikiana na Tanesco wameweka mikakakati ambayo itatoa jibu la kudumu litakalofanya Tanzania kusahau tatizo la umeme.
SOSI: MWANANCHI
"Nasema bila aibu, macho makavu kwamba ifikapo 2015 mgao wa umeme nchini utabaki kuwa historia,” alieleza Ngeleja
 
Ngeleja acha hadith,mgao hamtoumaliza,kwanza isaidieni TANESCO kuvunja mikataba angamizi,hasa huo wa IPTL ambao JK alisaini.
HEBU FIKIRIA KIPENGELE CHA MKATABA KINASEMA,ETI UMEME UMEZALISHWA HAUKUZALISHWA TANESCO WANALIPA PESA,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom