SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
TANGAZO KWA WATEJA NA WANANCHI KWA UJUMLA:
- Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuwatangazia Wateja Wake na wananchi kwa ujumla kwamba, kuanzia tarehe 1 Septemba, 2009, Wateja wote wanaotumia umeme watatakiwa kulipa ushuru kwa ajili ya mfuko wa umeme vijijini.
- Ushuru huu unatozwa kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (GN) la tarehe 1 Agosti, 2008 na kama inavyoainishwa katika sheria ya Bunge kuhusiana na Wamlaka wa Umeme Vijijini (Rural Energy Act of 2005) Kifungu namba 19 (3) (c) na (d).
- Ushuru huu ni kwa ajili ya mfuko wa Umeme Vijijini ambao matumizi yake ni pamoja na kuongeza kasi ya usambazaji Umeme Vijijini na mafunzo kwa wajasiliamali ili kuboresha maendeleo ya jamii kwa kutumia nishati bora vijijini. Ushuru huu utakuwa ni asilimia tatu (3%) ya thamani ya umeme uliotumiwa katika mwezi husika, yaani juu ya gharama ya matumizi ya Umeme.
- TANESCO ni mkusanyaji tu wa ushuru huu ambapo makusanyo yote yatakabidhiwa kwa wakala wa Umeme Vijijini (REA).
- Ushuru huu utaonekana katika Ankara ya umeme kama ifuatavyo: VAT 18% + EWURA 1% X REA 3% hii inatokana na upungufu wa nafasi katika fomu ya Ankara, hata hivyo kwa sasa tunatengeneza fomu mpya ambayo itaonyesha kila gharama peke yake, tunategemea fomu hii itakuwa tayari kabla ya mwisho wa mwaka 2009.
Imetolewa na: OFISI YA MAWASILIANO
TANESCO MAKAO MAKUU