TANESCO na Mkakati wa kuuza nyumba za wateja kulipia madeni

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
16,371
17,139
Wadau naleta kwenu hiyo sheria ambayo Tanesco wameitunga ya kuuza mali na nyumba za wateja wenye madeni......sidhani kama ni sawa na kama inaendana na katiba ya nchi!na vipi kama anaedaiwa ni mpangaji tu?hii sio sheria dhalimu na kukurupuka kama wale SSRA?
 
Huyo Badra Masoud alikuwa "AMELEWA" swaumu. Hakuna sheria/kitu kama hicho.

Kama kweli kipo aanze kuuza IKULU ya SMZ maana Zanzibar ndiyo mdaiwa namba moja SUGU. Akishamaliza akauze majengo wa Wizara ya ULINZI na JKT, akimaliza aende Majengo ya Wizara ya mambo ya NDANI. Akiwamaliza hao amfuate mama mchungaji Rwakatale auze St Marys zake, halafu ndiyo atugeukie sisi Wateja wadogo wadogo na tu-jumba twetu.

Huyo Badra Masoud anaongea kitu ambacho anajua kutoka moyoni hakitekelezeki! Sijui amefunga nini kuja kutulaghai Watanzania tena mbele ya Luninga!
 
...Waweke pia Mkakati na Utaratibu wa KULIPA vifaa vyetu vinavyopata hitilafu ama kuungua kutokana na Umeme wao wa Waka-Zima-Waka-Zima-Waka-Zima...!!!
 
Huyo Badra Masoud alikuwa "AMELEWA" swaumu. Hakuna sheria/kitu kama hicho.

Kama kweli kipo aanze kuuza IKULU ya SMZ maana Zanzibar ndiyo mdaiwa namba moja SUGU. Akishamaliza akauze majengo wa Wizara ya ULINZI na JKT, akimaliza aende Majengo ya Wizara ya mambo ya NDANI. Akiwamaliza hao amfuate mama mchungaji Rwakatale auze St Marys zake, halafu ndiyo atugeukie sisi Wateja wadogo wadogo na tu-jumba twetu.

Huyo Badra Masoud anaongea kitu ambacho anajua kutoka moyoni hakitekelezeki! Sijui amefunga nini kuja kutulaghai Watanzania tena mbele ya Luninga!

deni halifungi mtu usipolipa unapekwa mahakamani. mahakama ikijilizisha kuwa hutaki kulipa au umeshindwa ndipo faida kwa broke court wanapoanza kunufaika
 
hakuna taasisi au idara inaweza kuuza nyumba ya mtu kufidia deni bila kuwa na kibali cha mahakama
wanajidanganya kwani kama nyumba haikuwekwa dhamana kati yake na Tanesco wataiuzaje nyumba?
ni usingizi wa mchana.
 
Wanavyo ng'ang'ania hizo hela utadhani zinakwenda kweli kusaidia wananchi wa kawaida,kumbe ni miradi ya watu,ovyo sana.Tulipe halafu wakale,si ndio.Tutafikishana mbali.
Huyo Badra Masoud alikuwa "AMELEWA" swaumu. Hakuna sheria/kitu kama hicho.

Kama kweli kipo aanze kuuza IKULU ya SMZ maana Zanzibar ndiyo mdaiwa namba moja SUGU. Akishamaliza akauze majengo wa Wizara ya ULINZI na JKT, akimaliza aende Majengo ya Wizara ya mambo ya NDANI. Akiwamaliza hao amfuate mama mchungaji Rwakatale auze St Marys zake, halafu ndiyo atugeukie sisi Wateja wadogo wadogo na tu-jumba twetu.

Huyo Badra Masoud anaongea kitu ambacho anajua kutoka moyoni hakitekelezeki! Sijui amefunga nini kuja kutulaghai Watanzania tena mbele ya Luninga!
 
aende akauze VIFARU VYA JWTZ tuone kwa sababu .JWTZ ndo wadaiwa sugu pamoja na wizara yao ya ulinzi ndo aje auze nyumba zetu.
 
Civil Procedure Code chini ya Order XXXV. Nashangaa wameitafsiri vibaya. Inawaruhusu kufungua Summary Suit na siyo kuuza mali za wadeni. Ndo maana Malawi wanatuchemsha viongozi wetu hawajui kutafsiri sheria.
 
Duh! Watu kwa kukurupuka bwana!

anacho sema nisawa msilaumu lakini kama hiyo shelia ipo basi waikosea na wakigusa kwenda MAHAKAMANI mwisho wakesi wao ndio watakao shidwa na watalipa Fidia labda wawaomee huko MBAGARA na TANDALE waanze waone matokeo hata kama kesi ya madai haiwi ivyo inakuwaje uendelee kumpa umeme mtu ambae hajakulipa eti ili uuze nyumba yake ajaribu waone kama Tanesco ndio atafilisika kwa madeni hiyo ilikua TZ ya zamani watu mebadilika wasitafute kesi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom