Tanesco na huduma za kitapeli

haki na usawa

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
481
135
Naomba kuwaasa Tanesco kuleni haraka kwani dawa yaja
Angalieni TTCL nguzo ilikuwa ikidondoka wanakusema na hawairudishi mapema
Leo wanacholeta wananchi wanakikataa kwanini hamuoni?
Je mwasubiri muambiwe nini? Gharama za kuunganisha juu na hata mtu akilipa mbona hamfungi hizo waya?
Je mwaona watu wote mazuzu hadi watoe kitu kidogo?
Je mna ubavu wa kuhimili ushindani kama shirika lingine likianza kazi?
Je hamjui kuwa watu wengi wamechoshwa na wanataka watu wengine wa kutoa umeme?
Kaeni mkijua kuwa mtadondokea pua siku itakapofika? na kwasasa kuweni miungu watu na hata mkiamua kuzima mchana kutwa zimeni lakini dawa yenu iko jikoni. Naomba mlale sana na msiamke maana nanyi mmelewa fedha haramu za wanyong'e na mnaelea katika damu zao.
"HAKUNA CHA MKURUGENZI WALA SECRETARY WOTE LENU MOJA NYONYENI SANA DAWA YAJA NA WENGINE MTAKUFA KWA PRESA ANDIKENI WOSIA MAPEMA"kwani hamtaamini atakapopatikana mbadala wenu na nyie kukosa watu na hakika waya zetu zitauzwa kutundikia nguo na kujengea.
 
Yaani ndugu yangu ukiongelea Tanesco unaongelea serikali,hii ni kampuni yetu watanzania wote,inauwawa kama kampuni na viwanda vingine vilivyouliwa. Wanasubiri kuibinafsisha ili watanzania tukawe vibarua kwenye mali zetu wenyewe.
 
Tanesco wanakera sana na Serikali ipo nyuma yao. Umeme tunalipa lkn haupo, sasa hivi hapa niko home na umeme ulishakatwa masaa kibao yaliyopita. Ngoja wachine walete umeme wao feki wataona tutakavyowahama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom