Tanesco msituchezee akili -- maboresho yenu ya LUKU yamekwama!

ndivyo hivyo. Leo mchana huu nilikwewnda kwa agent wa tanesco kununua umeme kama ilivyoelekezwa na matangazo ya tanesco ya zaidi ya wiki sasa. Yule agent kaniambia hakuna luku -- yaani amesitisha kuuza umeme kwa sababu waliokuja kununua umeme leo hawakupata vikaratsi 3 kama tanesco ilivyotangaza -- mashine inatoa karatasi moja tu kama kawaida ya mauzo ya umeme na kwamba namba zake haziingii kwenye mita kabisa na wateja walirudi kulalamika na kudai hela zao, bila majibu.

Baada ya kuambiwa hivyo nikaja moja kwa moja kwenye computer yangu kuandika habari hii. Sijui wengine walionunua umeme leo wamepata masaibu gani.

nimenunua kwa wakala baada ya kuona foleni ni kubwa pale tanesco mikocheni lakini nilipoingiza kwenye luku ikakubali, nikagundua kwa wenye mita za vichochoroni a.k.a za vishoka ndio zinagoma mpaka ufike kwenye ofisi zao
 
Zaidi ya 80% ya Watz hawafanyi kazi ipasavyo siajabu hata wewe mwenyewe haufiki kazini kabla ya 07:30 asubuhi muda uliopangwa na Serikali na siajabu kila siku unasign chini ya mstari, hili halioni ila unaona ya wenzio tu Tanesco, kifupi sisi Watz hakuna anayefanya ipasavyo wote wazembe kwa namna moja au nyingine aidha tunachelewa kufika sana kazini au tunawahi kutoka (kutoroka) au tunakwenda lunch kwa saa nzima, na yote hayo tunayafanya hatuyaoni kwa maana wanodhurika ni wengine ila mzunguko ukienda ukikufikia ndio unaanza kulalamika kama hayo ya Tanesco!

Hivyo kuwalaumu Tanesco kwamba hawafanyi kazi masaa 24 ni kuwaonea tu Watz karibu wote tuko hivyo, siajabu na wewe ukafit ktk hao niliowaleza hapo juu jibu unalo wewe mwenyewe kwenye nafsi yako!

well said!!
watanzania wengi ni tu wazembe, tunapenda kulalamika, tunapenda mteremko, maneno mengiiii.
taasisi zote zipo hivyo.wafanyakazi wengi wapo hivyo.kila mtu ajirekebishe.
 
Tumechoka walopitisha hizo dill n kutuachia uchafu wao wanakula kuku kwa mrija namaluku yao ya dezo kibao eeh mwenyezi mungu nipe nchi hii kuiongoza kwa miezi sita tu
ndivyo hivyo. Leo mchana huu nilikwewnda kwa agent wa tanesco kununua umeme kama ilivyoelekezwa na matangazo ya tanesco ya zaidi ya wiki sasa. Yule agent kaniambia hakuna luku -- yaani amesitisha kuuza umeme kwa sababu waliokuja kununua umeme leo hawakupata vikaratsi 3 kama tanesco ilivyotangaza -- mashine inatoa karatasi moja tu kama kawaida ya mauzo ya umeme na kwamba namba zake haziingii kwenye mita kabisa na wateja walirudi kulalamika na kudai hela zao, bila majibu.

Baada ya kuambiwa hivyo nikaja moja kwa moja kwenye computer yangu kuandika habari hii. Sijui wengine walionunua umeme leo wamepata masaibu gani.
 
Leo asubuhi nilikuwa kwenye mstari pale Ilala Petrol station kwa wakala wa LUKU nikashuhudia watu kibao wakilalamika kwamba baada ya maingizo ya zile seti mbili za namba, maingizo ya umeme hayaingii. ilipofika zamu yangu ya kununa nikaenda nyumbani, lakini baada ya kuingiza seti zile mbili zanamba, manunuzi ya umeme yaliktaa kuingia. Nikarudi kwa wakala na nikakuta watu kibao zaidi wakilalamika hivyo hivyo.

Tanesco toeni jibu kwa haraka. Au wanaringia hiyo monopoly waliyo nayo na ndiyo maana hawajali kitu?
 
Nafikiri Tanesco kuna kitu wanafuatilia kama si kuweka mfumo mpya. Tusilalamike sana, kama umenunua umeme kwa njia walizosema na ukapata tatizo lolote, wapigie simu maana number zao zipo kwa kila agent wa Tanesco.
 
Hivi tutaacha lini kulalamika? Tuwapeni muda jamani, haya mambo yatarekebishwa tu! Ila kama mita yako ni ya vishoka itakuwa imekula kwako!
 
Ndivyo hivyo. Leo mchana huu nilikwewnda kwa agent wa Tanesco kununua umeme kama ilivyoelekezwa na matangazo ya Tanesco ya zaidi ya wiki sasa. Yule agent kaniambia hakuna luku -- yaani amesitisha kuuza umeme kwa sababu waliokuja kununua umeme leo hawakupata vikaratsi 3 kama Tanesco ilivyotangaza -- mashine inatoa karatasi moja tu kama kawaida ya mauzo ya umeme na kwamba namba zake haziingii kwenye mita kabisa na wateja walirudi kulalamika na kudai hela zao, bila majibu.

Baada ya kuambiwa hivyo nikaja moja kwa moja kwenye computer yangu kuandika habari hii. Sijui wengine walionunua umeme leo wamepata masaibu gani.

Mimi yamenikuta hayo niliambiwa kwamba nikinunua napata karatasi 3 lakini nilipewa karatasi moja na dada muuzaji nikamuuliza mbona kuhusu karatasi 3 akaniambia usiwe na wasiwasi ukiingiza utaingia kufika home nikaambulia patupu kurudi akanipa namba nipige hiyo namba ipo bize kuanzia jana asubuhi mapka napoandika ujumbe huu. inaonekana tanesco hukurupuka kwenye kila kitu wanachotaka kufanya.
 
Mimi nilipata karatasi 3. Na 1 na 2 zilionyesha ch1 na ch2 lakini ya 3 ikawa rejected
 
heri nyie mliopata huo umeme, mie foleni iliyopo imebidi niahirishe kutumia umeme mwezi huu, hapa najaza mafuta ya taa kwenye chemli zangu maandalizi ya giza usiku
 
Ndipo akajitokeza mzee mmoja na kueleza kuwa maboresha yanalenga kuwakamata wale wote waliounganishia umeme na vishoka. Na kwamba kwa wasiopata vikaratasi vitatu wako matatani! Na ndio maana maelekezo ni wao kuwasiliana na ofisi za TANESCO. Hivyo usitokwe mapovu bure, huenda ni mmoja wao.

Mimi sikupata vikaratasi vitatu na siko matatani. LUKU ilifanya kazi vizuri tu. Nahisi kuna mita za zamani na za sasa. Za zamani ndo unapata vikaratasi vitatu na za sasa unapata kikaratasi kimoja.
 
Back
Top Bottom