Tanesco msituchezee akili -- maboresho yenu ya LUKU yamekwama!

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Ndivyo hivyo. Leo mchana huu nilikwewnda kwa agent wa Tanesco kununua umeme kama ilivyoelekezwa na matangazo ya Tanesco ya zaidi ya wiki sasa. Yule agent kaniambia hakuna luku -- yaani amesitisha kuuza umeme kwa sababu waliokuja kununua umeme leo hawakupata vikaratsi 3 kama Tanesco ilivyotangaza -- mashine inatoa karatasi moja tu kama kawaida ya mauzo ya umeme na kwamba namba zake haziingii kwenye mita kabisa na wateja walirudi kulalamika na kudai hela zao, bila majibu.

Baada ya kuambiwa hivyo nikaja moja kwa moja kwenye computer yangu kuandika habari hii. Sijui wengine walionunua umeme leo wamepata masaibu gani.
 
Hawa jamaa ni vilaza sana, afu eti leo hawafanyi kazi kwa hiyo tukae na giza paka jumatatu wameniuzi sana.....vilaza wakubwa.
 
Nami nimesikia watu wanalalamika hivyo. Ndiyo maana wengina huamua kuiba umeme.
 
Na kwa ujinga wao leo badala ya kukifanya kitengo cha luku kufanya kazi masaa 24 wao wanafanya nusu siku! Akili ya matope matupu.
 
Zaidi ya 80% ya Watz hawafanyi kazi ipasavyo siajabu hata wewe mwenyewe haufiki kazini kabla ya 07:30 asubuhi muda uliopangwa na Serikali na siajabu kila siku unasign chini ya mstari, hili halioni ila unaona ya wenzio tu Tanesco, kifupi sisi Watz hakuna anayefanya ipasavyo wote wazembe kwa namna moja au nyingine aidha tunachelewa kufika sana kazini au tunawahi kutoka (kutoroka) au tunakwenda lunch kwa saa nzima, na yote hayo tunayafanya hatuyaoni kwa maana wanodhurika ni wengine ila mzunguko ukienda ukikufikia ndio unaanza kulalamika kama hayo ya Tanesco!

Hivyo kuwalaumu Tanesco kwamba hawafanyi kazi masaa 24 ni kuwaonea tu Watz karibu wote tuko hivyo, siajabu na wewe ukafit ktk hao niliowaleza hapo juu jibu unalo wewe mwenyewe kwenye nafsi yako!
 
Nilikuwa nataka kununua leo nikasita nakuhisi mipango yao lazima kuwe na itilafu.
 
Zaidi ya 80% ya Watz hawafanyi kazi ipasavyo siajabu hata wewe mwenyewe haufiki kazini kabla ya 07:30 asubuhi muda uliopangwa na Serikali na siajabu kila siku unasign chini ya mstari, hili halioni ila unaona ya wenzio tu Tanesco, kifupi sisi Watz hakuna anayefanya ipasavyo wote wazembe kwa namna moja au nyingine aidha tunachelewa kufika sana kazini au tunawahi kutoka (kutoroka) au tunakwenda lunch kwa saa nzima, na yote hayo tunayafanya hatuyaoni kwa maana wanodhurika ni wengine ila mzunguko ukienda ukikufikia ndio unaanza kulalamika kama hayo ya Tanesco!

Hivyo kuwalaumu Tanesco kwamba hawafanyi kazi masaa 24 ni kuwaonea tu Watz karibu wote tuko hivyo, siajabu na wewe ukafit ktk hao niliowaleza hapo juu jibu unalo wewe mwenyewe kwenye nafsi yako!
ID yako imenipa majibu kibao ya ulichoandika hapo juu.
 
Ndivyo hivyo. Leo mchana huu nilikwewnda kwa agent wa Tanesco kununua umeme kama ilivyoelekezwa na matangazo ya Tanesco ya zaidi ya wiki sasa. Yule agent kaniambia hakuna luku -- yaani amesitisha kuuza umeme kwa sababu waliokuja kununua umeme leo hawakupata vikaratsi 3 kama Tanesco ilivyotangaza -- mashine inatoa karatasi moja tu kama kawaida ya mauzo ya umeme na kwamba namba zake haziingii kwenye mita kabisa na wateja walirudi kulalamika na kudai hela zao, bila majibu.

Baada ya kuambiwa hivyo nikaja moja kwa moja kwenye computer yangu kuandika habari hii. Sijui wengine walionunua umeme leo wamepata masaibu gani.

Haya ndio madhara ya kukurupuka! Tangazo limetolewa wiki nzima kuwa: nunua umeme kuanzia tarehe 1 Sept, ktk Ofisi za TANESCO au Wakala walioorozeshwa na TANESCO . Siyo ma agent wote wanauza token!
 
Ndivyo hivyo. Leo mchana huu nilikwewnda kwa agent wa Tanesco kununua umeme kama ilivyoelekezwa na matangazo ya Tanesco ya zaidi ya wiki sasa. Yule agent kaniambia hakuna luku -- yaani amesitisha kuuza umeme kwa sababu waliokuja kununua umeme leo hawakupata vikaratsi 3 kama Tanesco ilivyotangaza -- mashine inatoa karatasi moja tu kama kawaida ya mauzo ya umeme na kwamba namba zake haziingii kwenye mita kabisa na wateja walirudi kulalamika na kudai hela zao, bila majibu.

Baada ya kuambiwa hivyo nikaja moja kwa moja kwenye computer yangu kuandika habari hii. Sijui wengine walionunua umeme leo wamepata masaibu gani.

Nimekwenda kununua umeme kwa "wakala" kama tangazo linavyosema. Nilikuta foleni kubwa kiasi na kupitia hiyo nimejifunza jambo. Baada ya watu kadhaa kununua umeme alitokea bwana mmoja ambaye alipata karatai moja tu badala ya tatu (mbili zikiwa ni key changer).

Yule dada aliyekuwa anahudumu akamwambia kuwa nenda kajaribu kuingiza hizo token na kama zikigoma chukua namba ya TANESCO imebandikwa hapo nje uwapigie kwani ndio maelekezo yao yalivyo. Mie sikuridhika na hali hiyo ndipo nikaanza kufanya utafiti kwa nini baadhi wapate karatasi moja tu.

Ndipo akajitokeza mzee mmoja na kueleza kuwa maboresha yanalenga kuwakamata wale wote waliounganishia umeme na vishoka. Na kwamba kwa wasiopata vikaratasi vitatu wako matatani! Na ndio maana maelekezo ni wao kuwasiliana na ofisi za TANESCO. Hivyo usitokwe mapovu bure, huenda ni mmoja wao.
 
Mimi nilifikiri hawa jamaa kwavile wanajiendesha kibiashara, wangefanya kazi masaa mengi zaidi ili wakusanye fedha za kujiendesha badala ya kuomba ruzuku ya serikali( kodi yetu) kila siku! Hawa siyo wabunifu/uchungu na shirika lao. Pamoja na monopoly waliyonayo hivi sasa kwenye umeme, bado biashara inawashinda!
 
Mie nilipata ujumbe huu:
TANESCO will be upgrading LUKU system on 01/09/12. You are required to purchase LUKU from vendors. Thereafter, you will continue purchasing LUKU with M-PESA.
 
Nimekwenda kununua umeme kwa "wakala" kama tangazo linavyosema. Nilikuta foleni kubwa kiasi na kupitia hiyo nimejifunza jambo. Baada ya watu kadhaa kununua umeme alitokea bwana mmoja ambaye alipata karatai moja tu badala ya tatu (mbili zikiwa ni key changer). Yule dada aliyekuwa anahudumu akamwambia kuwa nenda kajaribu kuingiza hizo token na kama zikigoma chukua namba ya TANESCO imebandikwa hapo nje uwapigie kwani ndio maelekezo yao yalivyo. Mie sikuridhika na hali hiyo ndipo nikaanza kufanya utafiti kwa nini baadhi wapate karatasi moja tu. Ndipo akajitokeza mzee mmoja na kueleza kuwa maboresha yanalenga kuwakamata wale wote waliounganishia umeme na vishoka. Na kwamba kwa wasiopata vikaratasi vitatu wako matatani! Na ndio maana maelekezo ni wao kuwasiliana na ofisi za TANESCO. Hivyo usitokwe mapovu bure, huenda ni mmoja wao.

Uwongo huo. basi watu wote wamefungiwa luku na vishoka? kama ni hivyo basi wafanyakazi wote wa Taesco ni vishoka pamoja na magari yao n.k.

nani aaminike? Watz waende ofisi gani sasa wapate kufungiwa Luku ya halali?
 
Yule dada Badra inabidi atoe tamko haraka, ama sivyo kuna watu watalala giza hadi J3 na Tanesco kukosa mabilioni!
 
Uwongo huo. basi watu wote wamefungiwa luku na vishoka? kama ni hivyo basi wafanyakazi wote wa Taesco ni vishoka pamoja na magari yao n.k.

nani aaminike? Watz waende ofisi gani sasa wapate kufungiwa Luku ya halali?

Unachotakiwa kufanya ni hivi: Ukienda kutaka kufungiwa Luku, kuna fomu pale lazima uipate ya kuwataka mafundi watakaokufungia Luku watie saini zao na kujifunga kabisa kwamba wao siyo vishoka!
 
Nimekwenda kununua umeme kwa "wakala" kama tangazo linavyosema. Nilikuta foleni kubwa kiasi na kupitia hiyo nimejifunza jambo. Baada ya watu kadhaa kununua umeme alitokea bwana mmoja ambaye alipata karatai moja tu badala ya tatu (mbili zikiwa ni key changer). Yule dada aliyekuwa anahudumu akamwambia kuwa nenda kajaribu kuingiza hizo token na kama zikigoma chukua namba ya TANESCO imebandikwa hapo nje uwapigie kwani ndio maelekezo yao yalivyo. Mie sikuridhika na hali hiyo ndipo nikaanza kufanya utafiti kwa nini baadhi wapate karatasi moja tu. Ndipo akajitokeza mzee mmoja na kueleza kuwa maboresha yanalenga kuwakamata wale wote waliounganishia umeme na vishoka. Na kwamba kwa wasiopata vikaratasi vitatu wako matatani! Na ndio maana maelekezo ni wao kuwasiliana na ofisi za TANESCO. Hivyo usitokwe mapovu bure, huenda ni mmoja wao.
mimi nimepata hivyo vikaratasi vitatu na nimeingiza namba lakini hakuna umeme unaoingia...nimekwenda kwa hawa jamaa wa luku wameniambia inabidi kwenda tanesco kubadiishiwa sijui vidudu gani! hiyo ni mpaka j'tatu na nikiangalia kilichosalia kwenye luku kunifikisha j'tatu ni 0.64! '***** zao tanesco!
 
Uwongo huo. basi watu wote wamefungiwa luku na vishoka? kama ni hivyo basi wafanyakazi wote wa Taesco ni vishoka pamoja na magari yao n.k.

nani aaminike? Watz waende ofisi gani sasa wapate kufungiwa Luku ya halali?

Sina la kusema zaidi.
 
Back
Top Bottom