TANESCO msitake tuwatukanie wazazi wenu

Wanalambwa nyu.... nini hawa TAA ZIMA,muhimu hapa ni vitendo watanzania tuingie barabarani,huu ndo muda wa kutiana adabu,kama vipi BAVICHA watuongoze tuzame road

Wenzetu wanaandamana huko Greece kutokana na maisha kuwa magumu na mimi naunga mkono maandamano yanayoanzishwa kwa pressure ya ndani inayosababishwa na waTZ kuchoka na haya ndio maandamano ya kweli na yenye tija kwani kila mtu ataandamana hadi haja yao ipatiwe majibu practical.
 
daaah mi ndo nishasahau matumizi ya taa, wanarudisha wakati nimelala na kukata kabla sijaamka. ila afadhali tu jumapili mchana hawakati ndo muda wa kunyoosha vivazi vyote

We subiria Jumapili ijayo kama utaona umeme. Hali ni mbaya mno
 
duu poleni wajamini ndio maana nikahama nchi kuwa mbeba box
sijawahi ona umeme unakatika nshasahau hilo.sisi tuna vyanzo vingi vya umeme
lakini ufisadi,ujinga,rushwa vimetawala.shirika libinafsishwe tu hakuna njia mbadala,
nlishasema haiwezekani kwa shirika kama tanesco kuwa na uwezo wa kuzalisha,kusambaza,
kuuza umeme peke yake lazima kuwe na makampuni mengine shindanishi yatakayozalisha umeme,
mengine yawe na kazi ya kuweka miundo mbinu na Tanesco wawe waanuza ila kuyalipa haya makampuni
inawezekana sana mbona nchi tajiri wanafanya hivo na maisha ni mswano?????
Tanzania nchi yangu inaliwa na wachache,maskini wakilala kwa njaa...wananchi amkeni sasa mtalia mpaka lini?
 
Kuna mradi wa kigoma wa megawati 200,pia mtwara tutazalisha kwa gesi megawati 1000,tumeagiza mafuta mazito kama tope nayo yataenda mwanza kuzalisha megawati 8000,huo tutauza hadi uganda.....vilevile kuna megawati 5000 zipo njiani wiki ijayo zitakua bandarini.....lengo ni kupunguza mgao mtaa wa magogoni......Kasi ya megawati itaongezeka mwaka huuu....huku barabara zitawekwa lami kwa kilometa 11,000:::::megawati nyingine zitaenda MSOGA
 
Yaani umeme sisi tunapata nadhani masaa matatu kwa masaa 24 yaani siku moja. Inaboa sana ndugu zangu hakuna tangazo wala nini inauma sana.
wenzetu wakiwa wanapiga hatua za kimaendeleo kwenye sekta ya nishati na zile za sayansi na teknolojia, sisi tumebaki kumulikana na simu za tochi
 
Kweli wanatukera mkuu,twende nao taratibu watatupatia tu umeme.



Mi nashauri umeme ukiwa stable na sisi tugome kuutumia. Maana tushazoe kwenda kazini bila kunyoosha nguo, tushazoe pika na kuni kwani majiko ya umeme yako stoo, sasa friji twafanya kabati la kuweka vyombo kwani ukiweka nyama au samaki zaoza.
 
Mibwege ya Tanesco tayari imekata umeme. Huku Menge hatuna umeme tangu jana, leo wamewasha muda mfupi tu na tayari wameuchukua.
 
Back
Top Bottom