TANESCO: Mipango lukuki, Umeme hakuna

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,941
9,947
WanaJF, nimemsikiliza Msemaji wa TANESCO, Bi. Badra Masoud akihojiwa na mtangazaji wa TBC1 Bwana Marin Hassan Marin kwenye kipindi cha Jambo Tanzania asubuhi hii.

Nimeshangaa kumsikia akielezea mipango lukuki mara tutazalisha megawatt 100, mara megawatt 200, mara megawatt 60:

Kila mara ni mipango ya megawatt tu mbona hakuna umeme?

Watanzania tunataka umeme siyo mipango ya kilowatt wala megawatt ambayo haitoi tija tangia imeanza kutajwa na Waziri Ngeleja pamoja na TANESCO.
 
Ukitaka kufanya siku yako iwe njema msikilize JK mwenyewe anavyomudu KUSOMA MAKARATASI yaliyoandikwa idadi ya MIRADI na Location itakakojengwa!..hakika utafurahi hata kama ulikuwa na ugomvi na jirani, mnayamaliza!
 
Jamani jamani TANESCO!! Yaani nilikuwa namweangalia Badra akitoa mipango ya TANESCO jinsi ya kumaliza tatizo la umeme na muda huohuo umeme umekatika hapa nilipo kwa kuwa mgawo ni wa kutisha na battery ya ka laptop kangu ni mbovu, naondoka niende kuwinda tu basi. Kero imekuwa kero
 
Ndugu watanganyika wenzangu balaa la giza tororo limeongezeka,jana mitambo ya kuzalisha umeme songas imezimwa mpaka alhamisi! Natamani kuhamia nji ingine hii imeuzwa ooooh
 
Mipango wanayopanga inaendana kabisa na akili zao, hizo nafasi walizonazo ndani ya shirika sidhani kama walipewa kwa sababu wanaziweza ama ni kwa sababu ya vyeti vyao (nadhani hawa waliajiriwa kwa sababu ya vyeti na si nn wanaweza kulifanyia shirika na umma wa watz), mtz kama mm sihitaji kujua hizo logistics za megawat shenzi nn nn, nachotaka mm ni kuona kwangu na mshine ya kusaga na kukoboa kunawaka, kama akili na uwezo wa kufanya kazi/kuchukua maamuzi jenzi zingekuwa ni nguo nadhani viongozi wa tanesco wangebaki uchi wakibakiza mikono yao tu kusitiri maungo yao ya uzazi
 
Ndugu watanganyika wenzangu balaa la giza tororo limeongezeka,jana mitambo ya kuzalisha umeme songas imezimwa mpaka alhamisi! Natamani kuhamia nji ingine hii imeuzwa ooooh

Upo nchi gani? Maana Mh. January Makamba na Zitto Kabwe wamepiga marufuku mgao wa umeme!
 
WanaJF, nimemsikiliza Msemaji wa TANESCO, Bi. Badra Masoud akihojiwa na mtangazaji wa TBC1 Bwana Marin Hassan Marin kwenye kipindi cha Jambo Tanzania asubuhi hii. Nimeshangaa kumsikia akielezea mipango lukuki mara tutazalisha kilowatt 100, mara kilowatt 200, mara kilowatt 60: Kila mara ni mipango ya kilowatt tu mbona hakuna umeme? Watanzania tunataka umeme siyo mipango ya kilowatt ambayo haitoi tija tangia imeanza kutajwa na Waziri Ngeleja pamoja na TANESCO.

Kimbunga,

Takwimu zake anaongelea Megawatt siyo Kilowatt..

Anywayz, KASUMBA ya ahadi ndiyo inayoendesha kila jambo ndani ya Serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete - Kila jambo ni ahadi, ahadi, ahadi - strange!
 
The same week DOWANS is sold is the same week SONGAS shuts down its generators....what a coincidence
 
mie sijaona umeme toka nilipoamka jana mpka ninapochangia hapa
ukipata nji ya kwenda usiniacha dearest ..................makamba anashangaa kwa nini kuna mgao
ama kweli tutaishi kimjini mjini
 
the same week dowans is sold is the same week songas shuts down its generators....what a coincidence

wamezima kweli dakiki tano zilizopita nimekatiza hapo songas kimyaaa kama kaburini! This country bwana mambo hayaendi kimpangilio why?
 
Kimbunga,

Takwimu zake anaongelea Megawatt siyo Kilowatt..

Anywayz, KASUMBA ya ahadi ndiyo inayoendesha kila jambo ndani ya Serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete - Kila jambo ni ahadi, ahadi, ahadi - strange!
Mkuu mimi sijui kutofautisha kilowatt na megawatt!! Ahsante kwa ilimu yako. Pamoja na hayo mipango yao ni mingi mno ila hakuna umeme ila mara ni tunategemea kuzalisha megawatt 100 mara megawatt 500, n.k, n.k lakini kila mara ni giza giza giza sijui hizo watt ziko wapi na zita materialize lini. Naona TANESCO hawajui walifanyalo. Siku hizi ndg. Ngeleja ameacha kabisa kuongelea hizo megawatt kwa kuwa huenda naye akazomewa kwa kuwaongopea watz kila uchao!!
 
The same week DOWANS is sold is the same week SONGAS shuts down its generators....what a coincidence

Mkuu kweli haka ka coincidence ni ka ajabu!! Mafisadi ni watu wa ajabu na hatari wanaweza kuwa wametega ili mitambo ikodishwe manake giza linatisha na hao wanunuzi wapya wanajifanya kushangaa kwamba kuna mitambo ambayo inaweza kuzalisha umeme lakini haitumiwi na nchi iko gizani!! Gia nzito hiyo
 
Viongozi wa Tz wanaweza majungu, fitina, kuwaandama wapenda maendeleo, kuhusu maendeleo ya mwananchi sahau......
 
Back
Top Bottom