TANESCO: mgawo wa umeme

Loyal_Merchant

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
623
267
Hivi mgao wa umeme umeisha au unaendelea..? Manake hapo siku za nyuma kulikuwa hakuna mgao. lakini sasa naona hali inazid kuwa mbaya na unakatwa bila mpangilio ili hali mvua zinaendelea kunyesha mpaka mafuriko. Inakuwaje hili...?
 
hata jana maeneo ya buguruni kulikuwa na mgao,toka sa 12 jioni mpaka watu wanalala ulikuwa haujarudi.
 
tunaomba wadau wa tanesco watupe update kwanini inarudi story ya mtera wakati mvua zinanyesha?
 
Hamiemi Mikocheni, kwa vile Mtukufu Rais ana nyumba pale makutano ya Mt. Migombani na Chato, huwa umeme haukatiki pale!
 
Hamiemi Mikocheni, kwa vile Mtukufu Rais ana nyumba pale makutano ya Mt. Migombani na Chato, huwa umeme haukatiki pale!

huku nako wanakata maaka hapa ofisini mara nyingi naona generator ndilo linafanya kazi.hata pale kwa mpemba tunapogonga menu mara nyingi unakuta joto kwa kwenda mbele
 
Yaani kwa sasa hawana mpangilio wowote, wanakata umeme tu bila taarifa wala sorry. Nathubutu kusema tatizo la umeme sio maji peke yake nadhani kuna mambo mengi zaidi. Sasa watuambie kunani?
 
kuna maeneo wanahamisha nguzo kupisha ujenzi wa barabara.Mfano ni wakati wa kuanzia Mwenge kwenda Tegeta ,Bunju..na pia kipande kati ya Mbezi Beach-Goba-na Kimara
 
huku nako wanakata maaka hapa ofisini mara nyingi naona generator ndilo linafanya kazi.hata pale kwa mpemba tunapogonga menu mara nyingi unakuta joto kwa kwenda mbele
Kaka uko Mikocheni gani hiyo, sisi tupo uswazi mitaa ya CCM, hata kuwe na mgao wiki nzima kweyu shwari...
 
Hivi mgao wa umeme umeisha au unaendelea..? Manake hapo siku za nyuma kulikuwa hakuna mgao. lakini sasa naona hali inazid kuwa mbaya na unakatwa bila mpangilio ili hali mvua zinaendelea kunyesha mpaka mafuriko. Inakuwaje hili...?

Jana nilijiuliza hili swali baada ya kufika hm nikaambiwa mchana kutwa kulikuwa umeme hakuna.. Hata juzi pia.. wiki jana yote kulikuwa na kitu kama mgao ingawa tanesco hawajatujulisha wateja wao.
Hivi bwawa lina upungufu wa maji tena??????
 
Nahisi ndio Janja ya kupitisha kiulaini
Zabuni ya kuzalisha umeme kwa majenereta
Nchi hii watu wajanja sana!yetu macho
 
Back
Top Bottom