TANESCO, Mgao umeanza kimya kimya?

Mponjoli

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
668
152
Habari wadau

Hivi karibuni kama wiki mbili kumetokea kukatika kwa umeme kila siku jioni mida ya saa moja usiku na kurudi kuanzia saa saba usiku hadi saa tisa usiku. Tatizo hili limejitokeza kwa maeneo mengi ya dar es salaam, mbeya, singida na kwingineko.

Wadau sijui kwa maeneo yenu hili limekaaje. Maana isije ikawa mgao umeanza kimya kimya bila taarifa. Ukataji wowote wa umeme kisheria unatakiwa utangazwe siku kadhaa kabla. Tanesco wamekuwa wakitangaza ukataji wa umeme unaotokea mchana tu, ukataji wa usiku unaenda kimya kimya.
 
Dar es salaam maeneo ya Ubungo Kimara hadi Kiluvya ndio wahanga wa mgao huo wa umeme.
Je sisiemu wanawakomesha wananchi kwa kumchagua Mnyika wa Chadema?
 
Kazi kwenu na bado mulitegemea nini kwa kuwarudisha MAFISADI?
Hawa Wa Mnyika itakuwa KUWAKOMOA TU, Ila aiwezi kuwa milele, wavumilie!
 
They want to justify a new and modern Richmond, this time will be properly calculated.
 
Maeneo ya Mbagala yote naona tukae kimya,

Mbagala kumekuwa na tatizo sugu la kukatika kwa umeme kila siku jioni na kurudi mtu unapokuwa umeshalala usiku kwa muda mrefu, lakini cha ajabu, wakati wa kampeni ulipoanza, umeme haukuwa unakatika, hadi tukaanza kuwashukuru tanesco kwa kurekebisha tatizo la kukatika katika kwa umeme.

Cha ajabu ni kwamba, toka raisi aapishwe, tumerudi tena kwenye mgao usio na mpangilio kila siku jioni, mbaya zaidi unakatika almost usiku mzima na kusababisha hasara kuwa sana kwa sisi watumiaji. Ukiwapigia simu tanesco kuwauliza au hata ukienda ofisini kwao (kitu ambacho nimefanya) na nimeandika barua kuonyesha kulalamika kwangu kwa kukatikakatika kwa umeme huku, jibu wanalonipa ni simple,, Kuna tatizo katika njia za umeme, mafundi wanafanyia kazi, utarudi.

Swali la msingi, je? tatizo hili katika njia linachagua wakati wa kampeni na wakati usio wa kampnei? na je? kwa nini mchana haukatiki (muda ambao binafsi sipo nyumbani) na unakatika usiku (muda ambao nipo nyumbani nataka nitumie umeme?

Nimekasirika hadi sasa nimeamua hata kwa mkopo, nitafute suluhisho langu kwa suala hili la umeme, siwezi kuendelea kuishi wanavyotaka tanesco, no way.
 
Back
Top Bottom