Tanesco Kuvunjwa?

John Mashaka amegusia swala ambalo lipo karibu kabisa na moyo wangu. Kwamba maendeleo yanaenda sambamba na matumizi ya umeme si siri. Hata ukisema kilimo kwanza, kilimo cha maana kitahitaji umwagiliaji na umeme.

Kutoka kwa mtu anayesifiwa kama John Mashaka, nilitegemea uchambuzi utakaozama zaidi ya kusema tunahitaji umeme, fedha zinazofujwa zingeweza kutupa umeme, na bunge litunge sheria nzuri.

Kwamba tunahitaji umeme, kama nilivyosema juu hapo, ni kile kinachoitwa "stating the obvious". Ni kama kusema baharini kuna maji. Lakini unaweza kusema alihitaji sehemu ya kuanzia. Kwamba fedha zinafujwa na zingeweza kusaidia hili ni kuonyesha msimamo dhidi ya rushwa na ufisadi. Hili ni zuri.

Kwamba bunge litunge sheria nzuri ni kuangalia sehemu ya tatizo tu. Mikataba hii mikubwa ya nishati inapoingiwa, hususan na makampuni ya kimataifa, ibara za usuluhishi mara karibu zote zinalenga kwenye usuluhishi katika mahakama za kimataifa ambako sheria za Tanzania hata zikiwa nzuri, mara nyingine zinaweza zisitumike, na sheria za kimataifa kuhusu usuluhishi zitumike. Nilitegemea Bwana Mashaka angetumia mfano wa karibuni, ambao ameutaja kwa kulalamika tu, wa serikali ya Tanzania kuilipa Dowans mabilioni ya shilingi, kama fundisho kwa watendaji wetu kuwa makini na kufanya uchambuzi wa kutosha kaabla ya kusaini mikataba hii.

Nilitegemea pia kuona chochote kuhusu mpango mpya wa Hydro Electric Power wa mto Rufiji. Napokea habari tofauti kuhusu mpango huu.

Gazeti la "This Day" la Disemba 7 limeandika jinsi gani Kikwete anavyokosa nafasi ya kuacha urithi wa jina zuri katika angalau hili (Ona hapa ) wakati huo huo Business Times limeripoti kwamba inaonekana makubaliano yatapatikana kati ya Tanzania na Brazil katika mpango huo huo wa Stiegler's Gorge (Ona hapa . Nilitegemea mtu mwenye kufuatilia habari za nishati nyumbani ama atujuvye kuhusu habari hizi kwa undani, uzuri na ubaya wake na kama anaunga mkono huu mradi ama la, au kama hana habari za undani sana basi azitaje tu ili wengine wanaomfuatilia nao wazijue na kuchangia zaidi.

Nakubaliana na Bwana Mashaka, lakini nikitafuta habari mpya katika maandiko yake siioni.

Wapi uchambuzi kuhusu vyama vya ushirika vya umeme wa wananchi katika kutafuta ufumbuzi? Hata kama si kwa miradi mikubwa ya HEP, wapi uchambuzi kuhusu kuvunja hodhi ya TANESCO katika nyanja ya nishati ya umeme, na kuruhusu wananchi kuzalisha na kuuziana umeme katika vyama hivi?

Hata kama tunazungumzia TANESCO, wapi uchambuzi kuhusu wapi "point of diminishing returns" ya TANESCO ilipo leo? Na je, TANESCO haiwezi kufaidika zaidi kwa kuongeza uwezo wa kuzalisha umeme, kuongeza wateja, na kupunguza bei ya umeme ambayo ni kati ya bei kubwa kabisa za umeme Afrika ?

Are we running the danger of stating the obvious too much, and not stating the not so obvious at all ?
 
Mashaka angewaaachia wanasiasa wazungumzie huo fisadi kwa kina, yeye angetupa analysis ya kiuchumi wa mifumo mbali mbali ya kuzalisha umeme kutoka small hydro power plants, small gas plants, wind na vyanzo vyengine

Pia angetuonyesha faida na hasara kiuchumi ya mifumo hiyo kushikiliwa na serikali au kuwa ni ya kikanda, au kuwa ya mashirika binafsi.

Kwa uandishi huu wa leo hajaitendea haki taaluma yake, wala hajatusaidia wananchi kutupa taarifa mpya yoyote.
 
Is there a danger of "stating the obvious too much" and not being pointed in the details among our professionals?

I wanted to write a piece to murder machete Nchimbi, he was quoted on Michuzi decreeing he wants a "national dress" ready in six months. I found out I couldn't, simply because I don't have a verbatim quote, and my attribution of the story was from Michuzi blog. My sense of credibility forbade me from writing without having a verbatim quote. So I felt it wasn't fair to write a comprehensive piece without more direct info and details.

I could write a lot more on a lot more topics, but I want to be detailed. Perhaps I need to relax this a bit, but to me credibility is a big thing, and our professional's writing should reflect this, especially when presented in a way to give people reason to believe they are reading an "expert opinion". As they say, the devil is in the details, are we detailed enough ? How can our bustling intellectuals and professionals inform in a meaningful way, and not just rally the masses behind some crusade banner without even knowing that Jerusalem is not just over the next village if they are not detailed enough ?

John Mashaka is quoted above expressing dissatisfaction in the state of our energy, particularly the culminating unmet needs, institutional corruption and lack of adequate regulations. All noble sentiments to be sure. I spent some time reading his piece only to find a general rant, perhaps inspiring to some, but certainly not that informative or worthwhile to me, especially from one so highly regarded in some quarters.
 
Kiranga

Hamna, hizo 'expert opinions' tunazoambiwa hakuna hata details za uchambuzi, sawa na makala zinazoweza kuandikwa na mtu alokuwa hana hata idea ya uchumi au sheria.

Yeye kama ni mchumi anapaswa kutuandikia kwa jicho la mchumi, maybe sio kama analysis report anayoweza kuipeleka kwa 'boss' wake kazini, lakini walau ikaribiane na hiyo kwa kidogo.

Hata kama hutaki kuandika kwenye taalum yako uliyobobea, basi hakikisha kuwa kuna details za kutosha including all the current affairs on the subject, sio kutuletea maelezo mengi ambayo yanapigiwa kelele saa zote na wanasiasa.

Hatuhitaji wana siasa saa zote, tunachohitaji ni wataalamu wa kuwakosoa na kuwarekebisha wanasiasa kwenye chambuzi zao wanazotoa. Na sio kufanana nao kimtizamo, unless of course he is one of them.
 
Zibeni nyinyi basi hayo mapungufu yake.

Tumeanza kwa kukupa links mbili hapo kuhusu mradi mpya wa HEP. Link moja ikisema mradi hauendelei, nyingine ikisema serikali iko karibu kukamilisha.

Umeambiwa kuhusu vyama vya ushirika vya wananchi kuzalisha umeme, ama kwa miradi midogo ya HEP au kwaalternative energy. Umeambiwa kuhusu kuondoa hodhi ya TANESCO kwenye umeme na jinsi gani hata kama hatuondoi hodhi hii moja kwa moja kwa haraka, TANESCO inavyoweza kuongeza uzalishaji, kupunguza gharama na bei, na kuongeza wateja na mapato.

Maana ya forum ni kujadiliana, soma, jielimishe, na wewe tupe mchango wako.

Habari ya kutaka mtaalamu mmoja, au magwiji wachache, kutaka kutuambia yote inanikumbusha TED Talk ya Chimamanda Ngozi Adichie kuhusu "The danger of a single story".

Mchango wako pia unatakiwa, wewe unaonaje ?

[video]http://www.ted.com/talks/chimamanda_adichie_the_danger_of_a_single_story.ht ml[/video]
 
Zibeni nyinyi basi hayo mapungufu yake.

Mwandishi anatakiwa ampe msomaji something to work with. Huyu hajatupa.

Licha ya mifano iliyotolewa na Kiranga hapo, tumejaribu kumuonyesha next time atupe nini ilituweze kupata mdahalo na mchango wa manufaa zaidi.
 
Tumeanza kwa kukupa links mbili hapo kuhusu mradi mpya wa HEP. Link moja ikisema mradi hauendelei, nyingine ikisema serikali iko karibu kukamilisha.

Umeambiwa kuhusu vyama vya ushirika vya wananchi kuzalisha umeme, ama kwa miradi midogo ya HEP au kwaalternative energy. Umeambiwa kuhusu kuondoa hodhi ya TANESCO kwenye umeme na jinsi gani hata kama hatuondoi hodhi hii moja kwa moja kwa haraka, TANESCO inavyoweza kuongeza uzalishaji, kupunguza gharama na bei, na kuongeza wateja na mapato.

Maana ya forum ni kujadiliana, soma, jielimishe, na wewe tupe mchango wako.

Habari ya kutaka mtaalamu mmoja, au magwiji wachache, kutaka kutuambia yote inanikumbusha TED Talk ya Chimamanda Ngozi Adichie kuhusu "The danger of a single story".

Mchango wako pia unatakiwa, wewe unaonaje ?

[video]http://www.ted.com/talks/chimamanda_adichie_the_danger_of_a_single_story.ht ml[/video]

Mr. Kiranga,
John Mashaka, Mwanakijiji, Nyani Ngabu aside, you are one of the bright heads in here. I suggest that we collaborate ( all mentined names above) to bombard these ****** in our government to change tune. We can work collectively through internet to come up with topics that will let these people know that we are serious. WE need change in our system. The kinds of Rostam, Lowassa, Karamagi and the rest must face Justice for their crimes and corrupt practices.
 
Hasanteni wale wote mliomuwa kuungana na mimi kupinga matumizi ya lugha ya kingerza pale pasipo na sababu, hii ni vita ambayo nimeamuwa kuinzisha humu jamvini, kingereza kitumike pale ambapo ni lazima kufanya hivyo, kwa wale wanaodhani kutumia kingereza ndio utaonekana humu kwamba wewe ndio msomi wanajidanganya wenyewe, maana kenya mpaka machizi wanaokula jalalani wanaongea kingereza.

Hakuna sheria kuwa JF iwe kwa ajili ya wabongo tu na lingine ni moja ya kutoa maoni na yasomwe na kila mtu. Hivyo kutumia lugha ya kiingereza haswa kwa masuala nyeti kama hii maada saaafiii sana, ili hata wenzetu wasiojua kiswahili wasome; hiyo ni International language asilimia kubwa wanaweza kusoma na suala hilo ni nyeti sana. Hongera Mashaka, keep it up!!
 
Pointi hiyo. sijui kwa nini humu majungu kiasi hicho?
 
Wanaobondea lugha inawezekana wana pointi, kwa maana ya kwamba majadiliano yalenge kuhusisha watu, na kama watu wengi hawajui Kiingereza makala ya Kiingereza inaweza kuwa haifikii watu wengi.

Lakini pia inawezekana Mashaka kalenga wataalam ambao hawana tatizo na Kiingereza. Ninachoshangaa ni kukosekana kwa majadiliano ya kina kuhusu details hata baada ya wengine kuheshimu matakwa ya baadhi kuhusu lugha.

Inaonyesha tu kwamba suala la lugha linatumika kama kichaka cha watu kujifichia, hata mtu akija na analysis ya Kiswahili anaweza kuambiwa "Kisahili chako kigumu"
 
John Mashaka amegusia swala ambalo lipo karibu kabisa na moyo wangu. Kwamba maendeleo yanaenda sambamba na matumizi ya umeme si siri. Hata ukisema kilimo kwanza, kilimo cha maana kitahitaji umwagiliaji na umeme.

Kutoka kwa mtu anayesifiwa kama John Mashaka, nilitegemea uchambuzi utakaozama zaidi ya kusema tunahitaji umeme, fedha zinazofujwa zingeweza kutupa umeme, na bunge litunge sheria nzuri.

Kwamba tunahitaji umeme, kama nilivyosema juu hapo, ni kile kinachoitwa "stating the obvious". Ni kama kusema baharini kuna maji. Lakini unaweza kusema alihitaji sehemu ya kuanzia. Kwamba fedha zinafujwa na zingeweza kusaidia hili ni kuonyesha msimamo dhidi ya rushwa na ufisadi. Hili ni zuri.

Kwamba bunge litunge sheria nzuri ni kuangalia sehemu ya tatizo tu. Mikataba hii mikubwa ya nishati inapoingiwa, hususan na makampuni ya kimataifa, ibara za usuluhishi mara karibu zote zinalenga kwenye usuluhishi katika mahakama za kimataifa ambako sheria za Tanzania hata zikiwa nzuri, mara nyingine zinaweza zisitumike, na sheria za kimataifa kuhusu usuluhishi zitumike. Nilitegemea Bwana Mashaka angetumia mfano wa karibuni, ambao ameutaja kwa kulalamika tu, wa serikali ya Tanzania kuilipa Dowans mabilioni ya shilingi, kama fundisho kwa watendaji wetu kuwa makini na kufanya uchambuzi wa kutosha kaabla ya kusaini mikataba hii.

Nilitegemea pia kuona chochote kuhusu mpango mpya wa Hydro Electric Power wa mto Rufiji. Napokea habari tofauti kuhusu mpango huu.

Gazeti la "This Day" la Disemba 7 limeandika jinsi gani Kikwete anavyokosa nafasi ya kuacha urithi wa jina zuri katika angalau hili (Ona hapa ) wakati huo huo Business Times limeripoti kwamba inaonekana makubaliano yatapatikana kati ya Tanzania na Brazil katika mpango huo huo wa Stiegler's Gorge (Ona hapa . Nilitegemea mtu mwenye kufuatilia habari za nishati nyumbani ama atujuvye kuhusu habari hizi kwa undani, uzuri na ubaya wake na kama anaunga mkono huu mradi ama la, au kama hana habari za undani sana basi azitaje tu ili wengine wanaomfuatilia nao wazijue na kuchangia zaidi.

Nakubaliana na Bwana Mashaka, lakini nikitafuta habari mpya katika maandiko yake siioni.

Wapi uchambuzi kuhusu vyama vya ushirika vya umeme wa wananchi katika kutafuta ufumbuzi? Hata kama si kwa miradi mikubwa ya HEP, wapi uchambuzi kuhusu kuvunja hodhi ya TANESCO katika nyanja ya nishati ya umeme, na kuruhusu wananchi kuzalisha na kuuziana umeme katika vyama hivi?

Hata kama tunazungumzia TANESCO, wapi uchambuzi kuhusu wapi "point of diminishing returns" ya TANESCO ilipo leo? Na je, TANESCO haiwezi kufaidika zaidi kwa kuongeza uwezo wa kuzalisha umeme, kuongeza wateja, na kupunguza bei ya umeme ambayo ni kati ya bei kubwa kabisa za umeme Afrika ?

Are we running the danger of stating the obvious too much, and not stating the not so obvious at all ?
correction...TANESCO tarrif is the lowest in EA and now the lowest in SADC after SA got 60% raise in theirs...when u speak of unbundling the utility ,its a matter of IPP's coming with clean contracts this is because EWURA has 5 licences for unbundling(transmission,generation and distribution )..what TANESCO need is the freedom to run independently and not kisiasa, right now all off grid stations are actually loss making , while u run ruvuma,kigoma,mbinga ,ludewa thermal stations as 50bn as operation costs..returns are hardly 1bn I think these plants should be taken off TANESCO's responsibility and run directly by the government or government shouldn't charge VAT on fuel running the plants..unbundling might make TANESCO under or perform..a private distibutor leasing TANESCO grid ( Artumas ) failed to operate in Lindi and Mtwara regions due to unfavourable prices..so these things have to be done kwa umakini mkubwa..increase of dam capacity and Stiegler's Gorge but also investing in coal and gas which is independent of the whether
 
Wanaobondea lugha inawezekana wana pointi, kwa maana ya kwamba majadiliano yalenge kuhusisha watu, na kama watu wengi hawajui Kiingereza makala ya Kiingereza inaweza kuwa haifikii watu wengi.

Lakini pia inawezekana Mashaka kalenga wataalam ambao hawana tatizo na Kiingereza. Ninachoshangaa ni kukosekana kwa majadiliano ya kina kuhusu details hata baada ya wengine kuheshimu matakwa ya baadhi kuhusu lugha.

Inaonyesha tu kwamba suala la lugha linatumika kama kichaka cha watu kujifichia, hata mtu akija na analysis ya Kiswahili anaweza kuambiwa "Kisahili chako kigumu"

Kiranga, you and mashaka need to talk. You are bright guys
 
Hasanteni wale wote mliomuwa kuungana na mimi kupinga matumizi ya lugha ya kingerza pale pasipo na sababu, hii ni vita ambayo nimeamuwa kuinzisha humu jamvini, kingereza kitumike pale ambapo ni lazima kufanya hivyo, kwa wale wanaodhani kutumia kingereza ndio utaonekana humu kwamba wewe ndio msomi wanajidanganya wenyewe, maana kenya mpaka machizi wanaokula jalalani wanaongea kingereza.

Jamani mbona mnamshambulia John Mashakav for nothing? Yeye kaandika article yake kwa kiingereza kutokana na audience aliyoilenga yeye na mtu mwingine kaichkua hiyo article kaibandika hapa JF sasa kosa la John nini hapa?

Kama hampendi kiingereza, ukiona article iliyoandikwa kiingereza usiisome wala kuchangia!!!!

Tiba
 
mashaka tanesco ni ulaji wa watu uvunjwe ili iweje?
 
Back
Top Bottom