TANESCO kuongeza bei ya umeme kwa 36%!

Pilato

Member
May 29, 2008
60
1
Kumekuwa na matangazo mikoani ya nayohusu wananchi kujitokeza kwa ajili ya mdahalo au semina SEHEMU ELEKEZI, iliyoandaliwa na EWURA pamoja na TANESCO ili kujadili kuhusu ongezeko hilo la umeme ambapo mtangazaji husema mananeno yafuatayo,

''kutokana na kampuni ya TANESCO kuamua kuongeza bei ya umeme kwa 36%, hivyo basi EWURA wameona kabla ya ongezeko hilo ili wananchi nao watoe mchango wao kama wanakubaliana au la, kila mwananchi unaombwa ufike sehemu husika (ELEKEZI) kwa ajili ya kutoa mchango wako kaaribuni''

Ninachokiona hapakwa hisia zangu ni kiini macho ambapo tayari jibu lipo vinywani mwao ila wanachofanya ni kutimiza taratibu nani wa kumlaumu au kuna nini hapa?
 
Hawa Tanesco uwezo wao wa kufikiri inawezekana ni mdogo sana. Kwa kubadilisha Mita za umeme toka Post Paid kwenda Prepaid (LUKU) hakuna saving? Kwani wasoma mita bado wanahitajika maeneo yanatumia LUKU? Badala ya kuongeza bei, kama hawana uwezo wa kuagiza LUKU za kutosha ili kupunguza wafanyakazi (wasoma mita) watafute wakala kama TRA wanavyofanya na watoe deadline ya wateja kubadilisha mita zao vinginevyo huduma ya umeme itasitishwa.
 
Kweli wewe ni Pilato. Tanesco kuongeza umeme asilimia 36 au kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 36? Mimi sijaelewa, fafanua.
 
Nimeperuzi hayo ombi la mapendekezo na makadirio ya TANESCO kutoka tovuti ya EWURA (zote 3 zinapatikana kwa Kiswahili na Kiingereza), na kwa mtazamo wangu hawana hoja ya msingi kuomba kupandisha bei ya umeme - tena hata 1%!. Hivi sasa gharama/bei ya/za umeme Tanzania inaongoza Afrika Mashariki. Ama turudi kwenye kuni, mafuta ya taa (yaliyochakachuliwa sijui), huku wakisema 'tunza mazingira', 'punguza uzalishaji karbon' nk.

Au ni mbinu ya kutafuta pesa kugharamia kampeni? Maana Mifuko ya Malipo Uzeeni siku hizi si dili tena, wananchi wanafichua mipango ya WENYE-NCHI! !
 
TANESCO ni moja ya mashirika ya umma ambayo ni mzigo mzito sana kwa umma. Hawa wanalipana bonus za ajabu ajabu kila baada ya kipindi fulani, wafanyakazi wanaoishi kwenye nyumba za shirika hilo hawalipii kabisa huduma ya umeme, na wale wanaoishi kwenye nyumba zao wanalipa pesa kiduchu wenyewe wanaita staff rate.

Ili yote haya wayapate, mtumiaji wa umeme wa kawaida anabebeshwa mzigo huo. Hii si haki hata kidogo, na kwa kweli tunahitaji kiongozi anayeweza kusema hapana kwa upuuzi huu.
 
ni lini tanesco itapata mbadala yani yawepo makampuni mengine yakuzalisha umeme kama ilivyo makampuni ya cm
 
nakuunga mkono dr phone, hakuna competitor wa TANESCO?
36% increase? Mtanzania wa kawaida atatoa wapi hela ya kulipia?
 
Hili shirika ni Kichomi na ni zigo la misumari kwa Umma.
Mpaka sasa ni 7% ya watanzania wana connection ya umeme tena umeme wenyewe sio wa uhakika.
Mgawo wa ajabu ajabu kila kukicha.
Mishahara yao sasa.
 
my god! nyie tanesco vipi? huduma zenu kwanza ni mbovu mno. kila siku mnatukatia umeme, mnaunguza vyombo vyetu vya ndani halafu leo mnatuongezea bei? hivi kwa nini tanesco hawapati mshindani kama yalivyo makampuni mengine kama ya simu na kadhalika ili wananchi wachague?

ivi mnajua kuwa sisi tunawalipia wafanyakazi wa tanesco bill zao? yaani eti wao wakilipa sh elfu 5 tu wanakuwa na unit kibao za kutumia hata miezi 6! huu ni wizi, wote tulipie umeme sawa.
 
Back
Top Bottom