Tanesco kunanini? Luku zimekuwa gumzo kila mahali

No admission

JF-Expert Member
Nov 26, 2011
215
68
Habari wana Jamvi;

Naomba niwasilishe hii mada ya ukosefu wa mita za LUKU. Toka mwaka jana (October 2010) wateja wapya wa TANESCO wamekuwa wakizungushwa bila kuelewa wapi waelekee kwani kumekuwa na tatizo kubwa la upatikanaji wa mita za LUKU. Tanesco wamekuwa wanatoa ahadi hewa kila ukienda kufuatilia na wiki kama mbili zilizopita afisa uhusioano wa Tanesco Badra Masudi alikiri kuwepo kwa tatizo la luku lakini akasema limeshatatuliwa lakini toka itolewe hiyo taarifa hakuna lolote linaloendelea.

Jamani Tanzania Tunaelekea wapi?
 
Hakuna meter za LUKU hili ni kweli, kuna ndugu yangua lipata tatizo la LUKU ilikuwa inaoverheat unapowasha A/C kwenye biashara yake amefuatilia miezi kadhaa mpaka mwisho ukajulikana ukweli hakuna meter za LUKU, bahati nzuri tatizo limegundulika lilikuwa kwenye circuit breaker.
 
Taarifa ya Tanesco wiki iliyopita, inasema shirika limepokea mzigo wa kutosha wa mita LUKU wale waliokuwa wanasubiri wawasiliane na ofisi za Tanesco za eneo lao, kulipia na kufungiwa mita.
 
Back
Top Bottom