Tanesco kukata umeme; watoto wafa temeke kwenye disco toto wakishehereka idd!

kaka noted..siunajuwa tena kiswahili wengine ni lugha ya pili au tatu...i meant to say..."baada ya umeme kakatika ghafla".....naomba isomeke na kueleweka hivyo....,nadhani miundombinu na hali ya TANESCO inajulikana.........
kule TABORA Mwaka juzi ni viyoyozi vilizidiwa nguvu watu wakaanza ku suffocate taratibu..bila kujijuwa wakawa wanaishiwa nguvu.........
Mimi ni dada, ha haaaaaaaaaaaa, mambo ya ID
kuhusu tatizo la viyoyozi au hitilafu yoyote ndani ya ukumbi sidhani kama ni fault ya Tanesco (sina uhakika sana kuhusu hili). kama ni kweli basi wakati mwingine tuache kulaumu chombo kisichohusika.
 
Kikwete atume rambirambi kama kawaida yaishe... mwisho itakuwa ni kafara ya aina fulani. Na wale wanaodhania kuwa hili haliwezi kutokea siku ya Krismassi au Pasaka na wao wanaishi katika ulimwengu wa kuishi kwa kudra. Pasipo kujiandaa na majanga tumejiandaa kwa maafa. Na bado wazazi hao hao wataenda kuwapigia kura watu wale wale walioshindwa. Msiniambie kuwa pamoja na kujiingiza katika teknolojia za kila namna kuonekana tumeendelea watu wameshindwa kuweka emergency lights kwenye kumbi kama hizo ambazo hazitumii umeme na zina sensors za kujiwasha zenyewe umeme unapokatika?

Embu angalia hivi: Je zingeweza kuleta tofauti taa zinapozimika ghafla? Nafahamu wengine watasema "unaleta mambo ya Marekani, sisi ni maskini".. screw em!

combo-red.jpg

SPECIAL PRICE
Manufacturer:
Lightworld

SKU
L-C-RW

List Price
$66.99

Our Price
$39.00 ea.

$39.00
Add Qty

Item Description
Combination LED energy saving exit sign and emergency lighting unit in one compact, modern design. Battery Included.
Arrows, Mounting, Single or Double Face Decisions, All can be made in the field.
Product Information

Category
Commercial Lighting

Light Source
LED

Width
2 3/4 inches.

Length
22 inches.

Height
10 inches.

Extends
1" inches.

Codes
Meets NFPA 101, NEC, OSHA

Listings
ETL, UL and CUL Listed

Warranty
5 Year Limited

Emergency Operation
90 Minutes Battery Backup

Canopy
Universal mounting canopy included

Number of Faces
Universal. Single or Double

Letter Color
RED

Housing Color
White

Remote Capacity
Call

... Mkjj, hiyo dola 40 inatosha kuhonga wakurugenzi wa halmashauri ili jamaa wapate kibali cha kufungua disco jingine, halafu wewe waongelea taa?! ...mweeeeh!
 
Waungwana

Kabla kuanza kutoa lawama, nawaombeni subira yenu kwanza.

Mimi ni mzazi, nafirikiria uchungu wanaoupata wazazi wa watoto waliofariki na walioumizwa kutokana na kisa hiki cha kusikitisha.

Suala la "disco toto" limekuwa kama desturi au utamaduni fulani, haswa wakati wa sikukuu. Ndio wakati pekee ambapo watoto hukusanyika na kucheza muziki wakifurahi kama watu wazima, kwa kuwa tu hakuna mahala popote ambapo pameandaliwa kwa ajili yao, ili nao waweze kuwa na wakati huo mara kwa mara, si wakati wa sikukuu pekee.

Miaka ya nyuma, watoto walio wakubwa - zaidi ya miaka 15 na kuendelea - walikuwa wasimamizi wa wadogo zao wakati wa kuenda "disco toto". Siku hiyo, kila mtoto alijiona kama vile amezaliwa upya, akiwa amevaa nguo yake mpya ya kusheherekea sikukuu. Baada ya chakula cha mchana, alasiri wanatoka kwa pamoja kuelekea mahali palipoandaliwa rasmi kwa SIKUKUU YAO. Kimsingi, sikukuu zote za Eid husheherekewa zaidi na watoto kuliko watu wazima. Lakini siku hizi, badala ya watu wazima (Waislam) kukumbushana waliyoyatenda wakati wa Ramadhan, wanakuwa mstari wa kwanza kwenda kwenye mabaa na kuwatembelea vimada wao, kurejea yale yote waliyoyaacha wakati wa Mwezi Mtukufu, kana kwamba HAWAKUSIKIA au HAWAKUJIFUNZA lolote wakati wa Mwezi Mtukufu. Watu wa aina hiyo, funga yao inakuwa haikubaliki, kwani ni dhahiri wanamkufuru Mungu.

Vyombo vya habari vimenukuliwa kwamba umeme unadaiwa kuzimwa na "vibaka" waliokuwa na nia ya kufanya uporaji kwenye ukumbi huo ulioandaliwa kwa ajili ya "disco toto" hilo. Kwa hiyo, hii ni kesi ya polisi, kwani si suala la "bahati mbaya" au "mapenzi ya Mungu", haya ni mauaji, huu ni uhalifu.

Ndio, tahadhari ilipaswa kuchukuliwa kabla ya maandalizi ya disco toto, kama vile kupata ukumbi ambao ulikuwa salama kwa madhumuni hayo. Nadhani waandaaji walisahau yaliyotokea Mwanza - disco toto kama hilo - au ilikuwa Tabora? Labda, wasimamizi wa Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa wangepaswa kuwa waangalifu zaidi, na hata polisi pia, kuhakikisha kwamba usalama ulizingatiwa zaidi, kwani inaonekana dhahiri kwamba mahali hapo (palipokuwa na mlango mmoja tu) hapakuwa salama.

Ingefaa pia kufanyike ukaguzi kwenye MIKOA YOTE kuhakikisha kwamba kumbi zote zenye mlango mmoja tu zifanyiwe ukarabati kuongea milango kufikia hadi minne, ili kuhakikisha usalama. Tujifunze kutokana na makosa yetu.

Wabillah Tawfiq. Wa Rahmatullah. Taala Wabarakatuh.

-> Mwana wa Haki

P.S. Innalillahi Wa Innalillahi Raaj'un!
 
Kuna vitu vingine vinatia hasira jamni ningekuwa kiongozi nanyonga wote waliohusika:mad2::mad2::mad2::mad2:
 
Ingefaa pia kufanyike ukaguzi kwenye MIKOA YOTE kuhakikisha kwamba kumbi zote zenye mlango mmoja tu zifanyiwe ukarabati kuongea milango kufikia hadi minne, ili kuhakikisha usalama. Tujifunze kutokana na makosa yetu.

Wabillah Tawfiq. Wa Rahmatullah. Taala Wabarakatuh.

-> Mwana wa Haki

P.S. Innalillahi Wa Innalillahi Raaj'un!

kuanzia Shauritanga hadi tukio hili la juzi unafikiri inachukua miaka mingapi kwa Watanzania kujifunza kutokana na "makosa"..?
 
Embu angalia hivi: Je zingeweza kuleta tofauti taa zinapozimika ghafla? Nafahamu wengine watasema "unaleta mambo ya Marekani, sisi ni maskini".. screw em!

Ni mentality mbaya sana ku dismiss vitu kwa kudai ni Umarekani au whatever. Kuna mengi sana mazuri ya kujifunza kutoka Marekani. Taifa hilo halijaendelea bure tu bila kufanya mambo vizuri/ usahihi....
 
Kikwete atume rambirambi kama kawaida yaishe... mwisho itakuwa ni kafara ya aina fulani. Na wale wanaodhania kuwa hili haliwezi kutokea siku ya Krismassi au Pasaka na wao wanaishi katika ulimwengu wa kuishi kwa kudra. Pasipo kujiandaa na majanga tumejiandaa kwa maafa. Na bado wazazi hao hao wataenda kuwapigia kura watu wale wale walioshindwa. Msiniambie kuwa pamoja na kujiingiza katika teknolojia za kila namna kuonekana tumeendelea watu wameshindwa kuweka emergency lights kwenye kumbi kama hizo ambazo hazitumii umeme na zina sensors za kujiwasha zenyewe umeme unapokatika?

Embu angalia hivi: Je zingeweza kuleta tofauti taa zinapozimika ghafla? Nafahamu wengine watasema "unaleta mambo ya Marekani, sisi ni maskini".. screw em!

combo-red.jpg

SPECIAL PRICE
Manufacturer:
Lightworld

SKU
L-C-RW

List Price
$66.99

Our Price
$39.00 ea.

$39.00
Add Qty

Item Description
Combination LED energy saving exit sign and emergency lighting unit in one compact, modern design. Battery Included.
Arrows, Mounting, Single or Double Face Decisions, All can be made in the field.
Product Information

Category
Commercial Lighting

Light Source
LED

Width
2 3/4 inches.

Length
22 inches.

Height
10 inches.

Extends
1" inches.

Codes
Meets NFPA 101, NEC, OSHA

Listings
ETL, UL and CUL Listed

Warranty
5 Year Limited

Emergency Operation
90 Minutes Battery Backup

Canopy
Universal mounting canopy included

Number of Faces
Universal. Single or Double

Letter Color
RED

Housing Color
White

Remote Capacity
Call

MKJJ,

Kabla ya kununua inabidi tuwaombe watengenezaji watumie maandishi ya kijani kwenye neno "EXIT" badala ya rangi nyekundu
 
Lawama kwa asasi husika ni lazima. Hili swala si la kuliacha lipite tu na ni vema tukaangalia namna ya kulizuia kutotokea tena katika siku zijazo.

Halmashauri ya jiji Temeke, wanahusika mojakwa moja na tukio hili, kwani wao ndio wanaosimamia shughuli zote katika Wilaya hiyo.

Kwa upande mwingine na hasa kwa watu waishio bara, inabidi kuangalia tena namna ya kusherekea sikukuu kama hizi. Wengi wa wazazi wanaona kuwa watoto wao waende kucheza disco kama ni sehemu ya kusherekea sikukuu. Na kwa wajujaji wachache huweka madisco yasiyokuwa na sifa nyingi za usalama na hivyo kusababisha majanga kama haya.

Visiwani wana utaratibu mzuri wa sherehe kama hizi, ambapo nyingi hufanyika katika maeneo ya wazi na yenye nafasi za kutosha kuweza kuhimili uwingi wa watu. Aidha huduma zote za dharura huwepo katika maeneo hayo. Ni vema kwa watu wa Bara kujaribu kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kusherekea sikukuu kwa mtindo wa Visiwani.
 
Hapana haya ni mapenzi ya Mungu.. msichunguze saana.

Kibunango.. kama kuna maeneo ambayo yamekaa kihatari sana yapo Zanzibar vile vile.. believe me.. siku moja ukija kushika kwenye majengo fulani hapo au masoko fulani.. utajua how unprepared watu wapo.. na msemo wa "mapenzi ya Mungu" utarudia hata visiwani. NI lazima tujiandae kwa majanga.
 
Yale machungu yaliyojitokeza mwaka juzi Tabora kwa watoto kufa kwenye disco kwa kukosa hewa ....safari hii yamejitokeza tena safari hii wilayani TEMEKE ambapo watoto zaidi ya watatu wamekufa na wengine kujeruhiwa ...mara baada ya umeme wa TANESCO kukatika ghafla kwenye eneo/mtaa ulipo ukumbi wa DISCO waliokuwa wakicheza..............huu ni mfululizo wa uzembe unaoendelea nchini!!!....magazeti ya leo yatakuwa na habari zaidi...

Ili si tatizo la TANESCO ni la serikali kwa ujumla! Sheria za biashara si nzuri, hata kama ni nzuri poor governance inaleta shida. Mwenye ukumbi wa disco alitakiwa kukamilisha vigezo vyote vya ukumbi wa disco ikiwemo standby generator; architecture/ design ya ukumbi - angalia makanisani paa liko juu sana ili kupata hewa ya kutosha muda wote; waandisi wetu wanaruhusu tu vi-structure vyenye paa za chini kuwa ukumbi wa disko.

Kwa nini watoto ufa kwenye sikukuu za Eid El Fitr tu? Mara mbili sasa!!
 
Kibunango.. kama kuna maeneo ambayo yamekaa kihatari sana yapo Zanzibar vile vile.. believe me.. siku moja ukija kushika kwenye majengo fulani hapo au masoko fulani.. utajua how unprepared watu wapo.. na msemo wa "mapenzi ya Mungu" utarudia hata visiwani. NI lazima tujiandae kwa majanga.
Mkuu MMJJ
Yapo maeneo hatari zaidi katika Zanzibar, lakini hayana mkusanyiko mkubwa wa watu, Katika mji mkongwe baadhi ya watu wanaishi katika majengo yasio na sifa ya kuishi watu. Hii inaweza kusababishwa na uwezo wao, ama tabia zao. Zaidi kuna maeneo yaliyojengwa kiholela ambayo yanashidwa kufikiwa kwa urahisi iwapo litatokea janga la aina yoyote ile.

Pamoja na yote, sherehe kama hizi utengewa maeneo mahsusi ili kuepusha kuwepo na majanga yasiotalajiwa.

Nikirudi nyuma sherehe kubwa kama za Idd huko visiwani hufanyika katika katika maeneo ya wazi, na ni kwa kuwaruhusu watu kujenga vibanda vya muda kwa biashara zao. Katika maeneo hayo vibanda vya muda, vibanda vya huduma za dharura hujengwa pia. Hii inatoa nafasi ya kuweza kukabiliana na janga lolote, tofauti na bara ambapo sikukuu inaonekana ni kwenda disco pekee.

Ni vema kwa halmashauri husika kutenga maeneo rasmi kwa ajili ya sherehe kama hizi, ambapo wataweza vilevile kuwavuta idara zenye kusimamia usalama karibu zaidi na washereheka.

Visiwani linapotokea janga watu hupenda kusema " Ni mtihani wa Mungu." Pengine tuna nafasi ya kujua Mungu ana mitihani mingapi kwa watu wake!
 
sitaki hata kulizungumzia hili.. nimelisikia toka jana.. na ninayo video ya ITV.. lakini tunazungumza ili kiwe nini? Kama hawakushtuka walipokufa 19 siku ya Idi katika mazingira yale yale.. kwanini mnafikiria watashtuka leo? Ni mapenzi ya Mungu.

Ukweli mtupu isipokuwa hapo nilipopigia mstari
 
I am totally against this toto disco idea for kids as youg as 6-7 years old!!! Hawa malaika wadogo walitakiwa wawe nyumbani na wazazi wao. Ukiondoa tatizo la milango ya dharura kutokuwapo lakini kuna mataizo mengine mengi zaidi...
-Tuna uhakika gani kama humo ndani kunakuwa na watoto peke yao na hakuna mijitu mizima mibazazi inayoweza kuwadhuru hawa watoto?
-Tuna uhakika gani kama humo ndani pombe haziuzwi kwa hawa watoto??
Disco Toto, Baby Toto or whatever we want to call it is a bad idea kwa watoto hawa wadogo!
 
Sio mapenzi ya mungu ni uzembe na hulka ya kutaka hela kwa wanaoendesha shughuli za burudani kama hii ya temeke na ile ya tabora. Serikali yetu inaangalia mwisho wa pua, baada ya lile tukio( la tabora ) hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kuhakikisha tukio kama lile halitokei tena.

tatito hapa ni serikali nzima kiujumla, nakubaliana na mwenzetu aliyesema kua tunaishi kimungu mungu tu, baada ya tukio kama hili kutokea tabora serikali ilitakiwa izinduke kutoka ktk usingizi mzito na kuweka standard procedure na regulation kwa waendesha kumbi za burudani, wala huwezi malumu mwenye ukumbi kwani yeye anaangalia faida tu, ni serikali ndio ilitakiwa imuwekee mipaka! baada ya tukio la tabora wakakurupuka kumtafuta mwenye ukumbi sijui kawatoa kesi imeisha, maana ukumbi kule kama kawa umefunguliwa! hii ndio madhara ya serikali isiyo na dira wala priority!
 
Pole wafiwa na watoto walioumia.

Hili wenda halitokei kwa sababu krismas na pasaka, watoto haweindi kucheza disco usiku. Hili tatizo wakulaumiwa ni wazazi wanaoruhusu watoto kwenda kucheza DISCO tena usiku.

Na tena labda sielewi, hili ni disco la aina gani? labda niulize ili nipate kwenda sambamba. Je ni disco wakimaanisha zile ngoma wanazopiga waislam mara nyingi wakati wa sherehe, ama ni lile disco la akina LUCKY DUBE?
Kuwalaumu Wazazi ni kuwafungulia milango serikali ipate sehemu ya kutokea.Janga kama hili yalishatokea huko nyuma na tume zikaundwa.

Hizi tume zimekuwa zinatumia mamilioni kama si mabilioni ya pesa ni vizuri tukawa tunasoma findings zao na kuzichambua tukajua ni nani wa kumnyooshea kidole la sivyo matatizo kama haya yataendelea kutokea tume zitaendelea kuandika upupu(labda) au Serikali kutofutilia mapendekezo ya tume.

Kama ile tume ya Tabora ingekuwa imefanya kazi yake vizuri na serikali ikafuatilia report yao hili lisingetokea hata kama linahusu vibaka.
 
Cha kujiuliza ni kwa nini vitendo hivi HAVITOKEI x-mas au pasaka..?

Ujumbe utafika tuu.

mkuu unamaanisha kuwa uislam, waislam na sherehe zao hairuhusiwi mambo ya kijinga kama disko? Na Ukristo, wakristo na sherehe zao ndo inaruhusiwa mambo hayo? kwa hiyo waislam wamechukizwa? Sijakupata mkuu.
 
Cha kujiuliza je ukumbi huo ulijengwa kwa ajili ya disco?If yes nani alitoa design na nani aliapprove iyo design.
If yes je walikagua/kufuatilia kama design inavyodemand.
Am told emergence exit chache na standby Generator haikuwepo?bse umeme wetu ni wa magumashi.
Ila walikufa ni watoto 8 kwa mujibu wa habari za mtaani UKU TMK na mmiliki wa jengo ati kasafiri na hawajui kaenda wapi!
FEDHA ILIONGEA
 
Back
Top Bottom