Tanesco itangazwe mufilisi

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,712
1,906
Habari za asubuhi wanajamii wenzangu.
Kwa kuwa nchi yetu imeingia mkenge kwa mikataba uchwala ya kufilisi nchi, k.m TANESCO na IPTL, DTL, Dowans Holdings SA na Richmond na kote huko tunadaiwa mabilion ya Shs. Kwa nini tusitumie busara kama wafanya biashara ili TANESCO itangazwe muflisi, maana haiwezi kulipa madeni yote hayo kirahisi wakati interest ikizidi kupanda shauri ya kuchelewa. TANESCO itangazwe muflisi iwe under receivership kwa LAT.
Shirika liwe transformed ligawanywe kwenye sehemu tatu:-
1. Power Producing and Generating CO.
2. Power Transferring and Installation CO.
3. Distribution, Procurement and Sales CO.
Hapa kwanza kazi ya kuzalisha umeme itafanywa na kampuni nyingine. Umeme utanunuliwa na kampuni nyingine na kusafilishwa kwenye centers.
Umeme utanunuliwa na kampuni nyingine itakayo uza kwa wateja. Hapo hawa wote watakuwa makini na kazi zao bila pressure za kuingiliwa na mtu mwingine.
HAPO TUTAVUA ZIGO LA MAGHARAMA YASIYOKUWA NA SABABU.
Nawasilisha tuchangie kujikwamua!!!!!!!
 
Je hapo hatutaongeza gharama ya umeme kwa mtumiaji? Tatizo siyo Tanesco ni serikali ya CCM. Labda serikali ya CCM tuitangaze mufilisi ili mambo yaende vizuri
 
Kwa kufanya hivi najua kabisa siasa haitakuwepo tena kwenye uzalishaji na usambazaji umeme. Ila angalizo tu ni kwamba kampuni hizi zote zisiwe na hawa mafisadi wa KIDUMU kwa kuwa mtoto wa NYOKA NI NYOKA TU watatumaliza hawa.
 
Ili kuweza kujikwamua yanahitajika maamuzi mazito saana. Bila hivyo tutapiga kelele hadi lioni sijui!!!!!!
 
Kwa kufanya hivi najua kabisa siasa haitakuwepo tena kwenye uzalishaji na usambazaji umeme. Ila angalizo tu ni kwamba kampuni hizi zote zisiwe na hawa mafisadi wa KIDUMU kwa kuwa mtoto wa NYOKA NI NYOKA TU watatumaliza hawa.
Hao mafisadi ndio wanao tufilisi nchi yetu, wanafanya kila mkakati kukwamisha mipango bora ya kimaendeleo kwakuwa hawapati maslahi ili waweke mipango ya muda mfupi wapate Ten percent (10%). Hawajali maendeleo ya nchi hao, ni mafisadi wezi wachumia tumbo, wamejaa serikali ya CCM!!!!!!!!!
 
Hivi nani aliwaambiwa kuwa TANESCO ni Maskini? Ni nani aliyewaloga nyie WAFILISTI=WA TZ??
TANESCO ina vyanzo vya fedha vya kumwaga!. Tatizo ni mafisadi ndio wanao lifilisi shirika pamoja na nchi yetu, wanajitahidi kwa kila hali kukwamisha mipango ya Shirika hilo kwa mfano kuingia mikataba feki kama ya RICHMOND!!! na DOWANS ili kutengeneza maslahi yao. Na inapotokea Mgongano gharama zinakuwa za TANESCO. Hawajali maendeleo ya nchi hao, ni mafisadi wezi wachumia tumbo, wamejaa serikali ya CCM!!!!!!!!!
 
Kwa mpango huo tatizo la Umeme nchini litakuwa HISTORIA!
Si wapo hata hapa jamvini wanasikia, kama hawapo wafikishiwe ujumbe , let them practice now ili tupone hizo karaha za mgao wa umeme!!!!!!!
Optimism is the faith that leads to achievement, Nothing can be done without hope and confidence. Helen Keller
 
Tenda ya nguzo za umeme ni ya EL. Nguzo moja ananunua TZS 100k yeye anaiuzia Taneso TZS 88k. Procurement hiyo inawaongezea wateja ugumu wa kuunganisha umeme maana nao inabidi waongeze bei kuwa milioni. Hebu tafakari nguzo zinapatikana Iringa/Mufindi lakini tenda ya kishkaji inamnufaisha fisadi EL na familia yake eti nautaka urais 2015? Mbona hawajawahi kuitangaza hiyo tenda?
 
Ni idea nzuri lakini

moja: operation cost itaongezeka sana na itakuwa mzigo mkubwa kwa mtumiaji wa mwisho.

mbili: nina wasiwasi na effectiveness wakati wa kurun hizo kampuni tatu, unless zote ziwe private, ila zikiwa under government itakuwa ni kazi bure. Maana kutakuwa na kutegeana sana katika utendaji na uwajibikaji.

Nionavyo mimi, tanesco inabidi isiwe centralized, kinachotakiwa iwe regionalized, inatakiwa kila zone iwe na kampuni independent katika maamuzi na pia katika uzalishaji wa umeme. Sio, umeme uzalishwe kidatu uletwe ubungo ndio uanze kusambazwa, au gas ya songas inazalishwa mtwara halafu inasafilishwa mpaka ubungo ndio ianze kuzalisha umeme, hii ni abnornal planning na pia ni wastage ya resources, kwanini mtambo wa kuzalisha umeme usijengwe hapo hapo songosongo na kuzalisha umeme tokea hapo ?

Natolea mfano tu, kampuni inaweza kugawanywa katika zone sita ambapo mikoa ambayo haitakuwa covered na hizi zone itajumuishwa kwenye zone ambayo ni nearest, kunaweza kuwa na kampuni kama ifuatavyo

1.eastern electric supply company
2.western electric supply company
3.northern electric supply company
4.southern electric supply company
5.lake zone electric supply company
6.southern highlands electric supply company

hizo kampuni zinakuwa independent kabisa na zinakuwa zinazalisha umeme kutokana na vyanzo vyao walivyovitafuta, zinasambaza na kuuza pasipo kutegemea maamuzi ya kutoka ubungo dar es salaam. Hii itaongeza sana uwajibikaji na pia itapunguza gharama ya distribution na kuondoa urasimu usio na ulazima.

Binafsi naamini nchi yetu imebarikiwa kuwa na vyanzo vingi sana vya umeme ambavyo havitumiki kwa sababu maamuzi yanasubiri mafisadi waliopo hapa dar es salaam.
 
Ni idea nzuri lakini

moja: operation cost itaongezeka sana na itakuwa mzigo mkubwa kwa mtumiaji wa mwisho.

mbili: nina wasiwasi na effectiveness wakati wa kurun hizo kampuni tatu, unless zote ziwe private, ila zikiwa under government itakuwa ni kazi bure. Maana kutakuwa na kutegeana sana katika utendaji na uwajibikaji.

Nionavyo mimi, tanesco inabidi isiwe centralized, kinachotakiwa iwe regionalized, inatakiwa kila zone iwe na kampuni independent katika maamuzi na pia katika uzalishaji wa umeme. Sio, umeme uzalishwe kidatu uletwe ubungo ndio uanze kusambazwa, au gas ya songas inazalishwa mtwara halafu inasafilishwa mpaka ubungo ndio ianze kuzalisha umeme, hii ni abnornal planning na pia ni wastage ya resources, kwanini mtambo wa kuzalisha umeme usijengwe hapo hapo songosongo na kuzalisha umeme tokea hapo ?

Natolea mfano tu, kampuni inaweza kugawanywa katika zone sita ambapo mikoa ambayo haitakuwa covered na hizi zone itajumuishwa kwenye zone ambayo ni nearest, kunaweza kuwa na kampuni kama ifuatavyo

1.eastern electric supply company
2.western electric supply company
3.northern electric supply company
4.southern electric supply company
5.lake zone electric supply company
6.southern highlands electric supply company

hizo kampuni zinakuwa independent kabisa na zinakuwa zinazalisha umeme kutokana na vyanzo vyao walivyovitafuta, zinasambaza na kuuza pasipo kutegemea maamuzi ya kutoka ubungo dar es salaam. Hii itaongeza sana uwajibikaji na pia itapunguza gharama ya distribution na kuondoa urasimu usio na ulazima.

Binafsi naamini nchi yetu imebarikiwa kuwa na vyanzo vingi sana vya umeme ambavyo havitumiki kwa sababu maamuzi yanasubiri mafisadi waliopo hapa dar es salaam.
Sawa kabisa Ndg Yangu, vile vile hiyo inawezekana wataalam wa umeme wakikaa chini bila kurubuniwa na wanasiasa na mafisadi, wakapanga vizuri inawezekana.
Cha muhimu ni kuwa na vyanzo vya uhakika vyenye tija ili tuweze kupata umeme wa uhakika!!! Haya mawazo bora yakachukuliwa na wahusika taifa letu likombolewe toka mikononi mwa majambazi wa Dowans, Richmond, IPTL and others my friend!!!!!!
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikijuliza hili swali. maana sielewi kabisa kama hawa Tanesco wanafanya biashara au huduma au msaada. Ni ukweli kuwa wananchi wengi wanahitaji umeme, umeme ni kitu cha muhimu ndiyo maana hata Tanesco wapandishe bei bado wananchi watajipanga kwenye ofisi za Tanesco kulipa au kutafuta huduma hiyo. Kitu kinachonishangaza ni kuwa pamoja na uhitaji mkubwa wa watu kutaka kuunganishiwa umeme jambo hilo limekuwa adimu na upatikanaji wake hauna tofauti na mtu anayetafuta madini kwenye ardhi yenye miamba migumu.

Biashara yeyote ni wateja wa kutosha, ninapopiga picha naona kama biashara ya umeme inalipa, sasa tanesco kama wako kibiashara hili hawalioni? je kama wangeunganishia watu wengi umeme kwa gharama zinazowezekana wasingepata wateja wengi na kupata faida itakayofanya wapunguze gharama kubwa inayotoza wanachi watumia huduma hiyo? maana wingi wa wateja maana yake ni kugawana gharama za uendeshaji na matokeo ni kushuka kwa bei ya umeme. Eneo ninaloishi zipo nyumba zaidi ya 80 ambazo hazina umeme, lakini tanesco wanataka tukawapigie magoti ili watupige bei, sisi tumeamua hatulipi wala hatutawafuata, kama ni bishara tutawaunga mkono kama ni huduma wataamua wenyewe lini watuletee huo umeme japo nyumba zetu zipo umbali usiozidi nguzo 4. ila kuna fisadi mmoja jirani mpaka umeme umemfikia ni nguzo kama 15, hiyo haiwasumbui maana wanachoangalia ni nani kanunua nguzo!!!
 
JK aiagiza Tanesco ipunguze gharama za umeme


Boniface Meena
RAIS Jakaya Kikwete ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuangalia uwezekano wa kupunguza gharama za kuunganisha umeme.Amelitaka kufanya hivyo ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kupata huduma hiyo akisema ikibidi, lifidie gharama hizo katika bili linazotoza kwa mwezi.

Rais Kikwete alisema hayo jana katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi kwa Taifa. Hotuba hiyo ilijikita katika mambo makuu matatu; ziara zake katika wizara, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na mchakato wa Katiba mpya.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, gharama za kuunganisha umeme zinazotozwa na shirika hilo sasa, zinawafanya wananchi wengi washindwe kupata huduma hiyo."Nimewakumbusha pia kuwa tunalo lengo la kuwapatia umeme asilimia 30 ya Watanzania ifikapo 2015.

Lengo hilo halitafanikiwa iwapo hatutatafuta namna ya kupunguza gharama au kutoa nafuu katika kuunganisha umeme kwa watu," alisema.Hata hivyo, alisema mgawo wa umeme bado unaendelea nchini, ingawa kwa muda wa wiki moja sasa, kumekuwa na nafuu kidogo.

"Hii imetokana na maji kuongezeka katika mabwawa ya Kihansi na Kidatu kutokana na mvua zinazonyesha katika Milima ya Udzungwa. Kwa sababu hiyo, uzalishaji wa umeme katika mabwawa hayo umeongezeka kiasi na kuleta nafuu kidogo iliyopo sasa," alisema.

Lakini akatahadharisha kuwa ahueni hiyo si ya kutegemea sana, kwani hali katika Bwawa la Mtera bado siyo nzuri, hivyo siku yoyote mvua hizo zitakaposimama au kupungua katika Milima ya Udzungwa, mgawo utarudi kwa makali yake ya awali.

"Hadi leo nizungumzapo nanyi, kina cha maji katika Bwawa la Mtera kimefikia mita 690.88 ambacho bado ni chini sana. Maji yapo juu ya kina cha ukomo wa chini kwa sentimeta 88 tu, hivyo bado tuna safari ndefu mpaka kufikia kina cha juu cha mita 698," alisema.

Kuhusu mapato na matumizi ya Serikali, Rais alisema miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu wa fedha (Julai – Desemba, 2010) makusanyo ya mapato ya Serikali yalikuwa chini ya lengo kwa asilimia nane.

Alisema hiyo imetokana na makusanyo katika Idara ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuwa chini zaidi kwa kipindi hicho.Kuhusu nidhamu na matumizi ya fedha za Serikali Rais Kikwete ametaka wale wote wanaofanya vitendo vya wizi, ubadhirifu wa mali za umma na kukiuka sheria na kanuni za fedha na ununuzi wa umma, wachukuliwe hatua.

"Juhudi za kuongeza mapato ya Serikali zitakuwa na maana iwapo kutakuwa na matumizi mazuri ya fedha za Serikali," alisema na kuongeza:

"Jambo hili nimekuwa nalisisitiza mara kwa mara na nililirudia nilipozungumza na viongozi na wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa."

Katika hatua nyingine, Rais alizungumzia maslahi ya watumishi wa umma akisema ni lazima wapate haki zao kwa wakati.Alisema watumishi kupandishwa cheo ni stahili yao na ni haki ya msingi. Hivyo, wakati wake unapofika na kama hakuna sababu za msingi lazima wapandishwe cheo.

Kuhusu Shirika la Reli Tanzania ((TRL) Rais Kikwete alihimiza uharakishaji wa mchakato wa kuachana na RITES na mchakato wa kuboresha reli ya Kati na TAZARA.
 
Kuna ki2 nimefikiria na nadhan inawezekana ikawa ni loophole ya kuwaibia tanesco. Nilikuwa nadhan ktk 3 pin plug ukitumia live (230 v) peke yake na kuachana na neutral yao then with suitable grounding (0 potential), nadhani energy meter yao haitafanya kazi kwa kuwa haitaweza kufanya kazi kwani there will not be flow of electricity ktk meter. Wana umeme mnaonaje hapo.? Hyo co loophole..?
 
Wabongo ni creative sana, ninaamini hapa umefikiria kuwaibia Tanesco na siyo kuwasaidia waondokane na hiyo loophole maana ungekuwa una nia nzuri ungewasiriana nao kisirisiri.
 
Uktaka kuchakachua, kama una nyumba unaishi na familia yako tu (sio na wapangaji) halafu unawaamini, fanya hv:
nunua luku meter halafu ingiza umeme lakini tofautisha nyaya mbili moja iwe direct kwenye luku na uweke taa chache na ule mwingine uende drect toka nje kwenda meter ya kawaida ambayo imefichwa na usupply jwa matumizi mengi km frj,jko,pac, hta, etc.
mengi zaidi watafute vshoka watakufanyia.
 
Hiyo kitu inawezekana kabisa nimewahi kufundishwa na Engineer wa Tanesco jinsi ya kufanya hiyo kitu ila na risk nayo ni kubwa ndugu!
 
Back
Top Bottom