TANESCO inaendesha mgao usio rasmi

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
WanaJF

Sisi wakazi wa Mbezi Beach tumekuwa tukiumizwa bila kupewa sababu ya msingi na hawa "ndugu" zetu wa TANESCO, kwani wamekuwa - kwa takriban mwezi mmoja sasa - na desturi (si tabia) ya kukata umeme bila kutoa taarifa, wakati mwingine mara mbili au tatu kwa siku, kwa muda mfupi na kisha kurejesha, na kama wanakata mara moja, basi umeme unarejeshwa baada ya saa sita au zaidi.

Meneja Uhusiano wa TANESCO, "dada" yangu, Badra Masoud, alitamka rasmi wiki iliyokwisha kwamba "mgao" wa umeme sasa haupo tena. Je, kinachoendelea huku Mbezi Beach - KILA SIKU - nini, kama si mgao?

Mwenye habari zaidi atuelimishe. LAKINI INAKERA!

./Mwana wa Haki
 
Kwa sababu huko mitaa ya kwenu hakuna Kigogo wa TANESCO anaeishi huko!
Sisi mitaa ya kwetu tunaishi na Vigogo wa Tanesco, huo mgao tunausikia redioni na kwenye TV.
Kama umekereka sana nunua SOLAR pannel uachane na Upuuzi wa TANESCO
 
Back
Top Bottom