TANESCO iitwe SHIMUKU

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,619
2,567
Ndugu wanaJF, kwa vile siku hizi umeme unakatika muda wowote na bila taarifa na kuwatia Watanzania hasara isiyo na kifani, nashauri jina libadilishwe na kuitwa Shirika La Muda Wowote Umeme Kukatika (SHIMUKU) au kwa Kiingereza Any Time Power Off (ATPO).

Jana Mbagala umeme ulikatika mara 6 na asubuhi hii tangu saa 12:00 hadi saa 3:30 umeshakatika mara 5. Sijui kama sababu yake ni matengenezo au mgawo. Hata kama ni matengenezo, je ni kila siku na kila saa? Ukiwa na kazi inayotegemea umeme inakutia hasara kubwa kwa vile inatokea mara kwa mara bila taarifa na hivyo ni dhambi mbele ya Mungu na Watanzania kuendelea kuliita shirika hili Tanesco. Nawasilisha!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom