Tanesco Ifunda: Ni kweli sayansi eneo hili imechemka kwenye uchawi?

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Jamani kwa wale wakazi wa maeneo ya Ifunda, Iringa au yeyote anayeweza kutolea ufafanuzi wa jambo hili, kuna sehemu TANESCO wamepigisha 90 degree turn power line yao ili kutopita juu ya Makaburi Fulani, sasa nimekuwa nikipata maelezo mengi juu ya sababu ya that divergence kutoka katika source ( siyo TANESCO) mbalimbali! Kwa yeyote ambaye ana jibu la kueleweka naomba ili niachane na kutafauta jibu, maana nimechoka kupata majibu mengi tofauti kwa ishu moja!
 
Si ude ukajionee mwenyewe??? Mimi nimeshaenda kujionea. Kuona ndio kuamini, kama ulishaambiwa mara nyingi ukashindwa kuamini, ni nini kitakufanya uamini ukiambiwa hapa JF nenda ukajionee.

WAZEE WA KUCHOMA NDIZI
 
Jamani kwa wale wakazi wa maeneo ya Ifunda, Iringa au yeyote anayeweza kutolea ufafanuzi wa jambo hili, kuna sehemu TANESCO wamepigisha 90 degree turn power line yao ili kutopita juu ya Makaburi Fulani, sasa nimekuwa nikipata maelezo mengi juu ya sababu ya that divergence kutoka katika source ( siyo TANESCO) mbalimbali! Kwa yeyote ambaye ana jibu la kueleweka naomba ili niachane na kutafauta jibu, maana nimechoka kupata majibu mengi tofauti kwa ishu moja!

Mkuu NU,

Nadhani hoyo 90 degree turn ya line ya TANESCO ipo kati ya njiapanda ya Tosamaganga na Ipogolo IR.

Mimi binafsi nimekuwa nikisikia hadithi moja kuhusu hiyo turn ya line ambayo inahusisha nguvu za mizimu ya makaburi yale ambayo yapo kando kando ya barabara upande wa kulia ukiwa unatoka IR kwenda Mbeya.

Inasemekana wakati TANESCO wanajenga line ile ya umeme, ilikuwa kila walipotaka kupitisha umeme juu ya yale makaburi nyaya zilikatika vipandevipande na walipojaribu kulazimisha zaidi, sio tu nyaya zilikatika bali hata wafanyakazi waliokuwa wanafanya shughuli ile walipoteza maisha kimiujiza.....ambapo maelezo ya haraka yaliyotolea ni kwamba akina ''mkwawa'' waliolala pale hataki usumbufu. Na ndipo TANESCO walipoamua kuvusha line upande wa kushoto then baada ya hatua chache wakarudisha upande wa kulia.

My understanding (not confirmed by TANESCO);

Pale kwenye makaburi kumepandwa miti, sijui jina lake lakini miti ilie mara nyingi hupandwa sehemu za makaburini kwa sababu hudumu muda mrefu sana, huwa haiathiliki na moto wala ukame na miti hii hupandwa kwa style fulani fulani ambazo huwawezesha ndugu wa walio lala hapo kupatambua kirahisi katika miaka mingi mbeleni.

Line za TANESCO kama zingepitishwa pale, zilikuwa zipite right juu ya makaburi yale ambapo kumepandwa miti niliyoieleza hapo juu, miti ile inakua so ingefikia wakati TANESCO wangelazimika kuikata ili isiathili line yao.

Nafikiri, ilie kukwepa gharama za kuhamisha makaburi yale na pia kukwepa usumbufu na ndugu wa wenye makaburi yale, Tanesco waliamua tu wayakwepe kwani ilikuwa ni njia rahisi sana kwao kufanya hivyo kuliko kuingia kwenye malumbano makali na wenye makaburi ambapo ingewabidi pengine kulipia gharama za kuyahamisha.....hata hivyo pengine haingekuwa rahisi sana kutokana na mila na desturi za wenye makuburi yale pengine kuamini kuwa mababu zao hawapashwi kusumbuliwasumbuliwa wakisha zikwa na hasa kama wao (mababu) walitoa wito wakuzikwa mahala pale kabla ya vifo vyao.

Huo ndio mchango wangu on this matter.

Cheers
 
Asante sana NL, nadhani na wengine watachangia, naamini sio vibaya kufanya vitu kama maana nimekuwa nikiuliza namna ambavyo Nguvu za Giza zinavyoweza kuzuia Power isikatize. B.T.W Asante kwa Analysis yako.
 
marekebisho. 90 turn ipo baada ya kupita njiapanda ya Tosamaganga unapoanza mtelemko mkali kuelekea Tanangozi. Kuna makaburi sehemu mbili ktk line ile ya umeme,na yametenganishwa kwa umbali wa kama mita 400 hivi.

Ukitoka Iringa utatangulia kuona makaburi hayo yasiyo na kasheshe,mita 400 mbele utaona line ya umeme imehamia kushoto kwako,20m ahead kuna hayo makaburi yenye kasheshe. Makaburi haya hujulikana kama makaburi ya Martin Kiyeyeu.

Hear say ni hizi; Miti ya pale kwa kiyeyeu ilipokatwa matawi yake,asubuhi waliona mti uko vilevile kama jana haukukatwa. Lakini makaburi yale mengine miti ile imepunguzwa matawi bila noma. tanesco walipopitisha umeme,umeme ulifika nguzo inayokaribia makaburi,electron flow ikafia hapo. Kaburi dume liko umbali wa mita moja toka barabara ya lami. Yaani hata wajenzi wa barabara walichemsha. Ni mpaka uone kwa macho ndo utaamini kisemwacho.
 
Asante sana Malila, mimi hayo makaburi nimeyaona tu nikipita kwenye gari, But I have never been there physically
 
Mkuu NU,

Nadhani hoyo 90 degree turn ya line ya TANESCO ipo kati ya njiapanda ya Tosamaganga na Ipogolo IR.

Mimi binafsi nimekuwa nikisikia hadithi moja kuhusu hiyo turn ya line ambayo inahusisha nguvu za mizimu ya makaburi yale ambayo yapo kando kando ya barabara upande wa kulia ukiwa unatoka IR kwenda Mbeya.

Inasemekana wakati TANESCO wanajenga line ile ya umeme, ilikuwa kila walipotaka kupitisha umeme juu ya yale makaburi nyaya zilikatika vipandevipande na walipojaribu kulazimisha zaidi, sio tu nyaya zilikatika bali hata wafanyakazi waliokuwa wanafanya shughuli ile walipoteza maisha kimiujiza.....ambapo maelezo ya haraka yaliyotolea ni kwamba akina ''mkwawa'' waliolala pale hataki usumbufu. Na ndipo TANESCO walipoamua kuvusha line upande wa kushoto then baada ya hatua chache wakarudisha upande wa kulia.

My understanding (not confirmed by TANESCO);

Pale kwenye makaburi kumepandwa miti, sijui jina lake lakini miti ilie mara nyingi hupandwa sehemu za makaburini kwa sababu hudumu muda mrefu sana, huwa haiathiliki na moto wala ukame na miti hii hupandwa kwa style fulani fulani ambazo huwawezesha ndugu wa walio lala hapo kupatambua kirahisi katika miaka mingi mbeleni.

Line za TANESCO kama zingepitishwa pale, zilikuwa zipite right juu ya makaburi yale ambapo kumepandwa miti niliyoieleza hapo juu, miti ile inakua so ingefikia wakati TANESCO wangelazimika kuikata ili isiathili line yao.

Nafikiri, ilie kukwepa gharama za kuhamisha makaburi yale na pia kukwepa usumbufu na ndugu wa wenye makaburi yale, Tanesco waliamua tu wayakwepe kwani ilikuwa ni njia rahisi sana kwao kufanya hivyo kuliko kuingia kwenye malumbano makali na wenye makaburi ambapo ingewabidi pengine kulipia gharama za kuyahamisha.....
hata hivyo pengine haingekuwa rahisi sana kutokana na mila na desturi za wenye makuburi yale pengine kuamini kuwa mababu zao hawapashwi kusumbuliwasumbuliwa wakisha zikwa na hasa kama wao (mababu) walitoa wito wakuzikwa mahala pale kabla ya vifo vyao.

Huo ndio mchango wangu on this matter.

Cheers

hilo suala ni gumu kulielezea, si rahisi kama unavyolisema. hebu check na ma engineer wa barabara/tanesco. kuna kitu kinaitwa hifadhi ya barabara au ROW (right of way). wajenzi wa barabara (TANROADS) na pia wa TANESCO kisheria hawawezi kuanza kujenga mpaka wapewe eneo (corridor) la kujenga na client ambaye anaweza kuwa ni serikali.
Rais huwa anabatilisha hati za viwanja ambazo zipo ndani ya eneo la hifadhi ya barabara kama hizo ili zijengwe barabara na line za umeme kwa ajiri ya maendeleo ya nchi. na watu wenye maeneo kama hayo huweza kulipwa na serikali fedha nyingi tu.
Suala la makaburi yale yanayoongelewa ni very special case. hata umbari kutoka barabarani ni mfupi sana, achilia mbali nyaya za tanesco kwani tulitegemea barabara/nyaya zihamishwe au kaburi lihamishwe
ndiyo maana watu wanakimbilia kuamini vingine
 
So what is your ''here say''?
 
So what is your ''here say''?

here say!!!!! nilisikia kuwa mpango ulikuwa ni wa kuhamisha makaburi lakini ilishindikana baada ya negotiations za muda mrefu na wale ndugu (line ya machifu). pia nilisikia kuwa mwanzoni nyaya zilifungwa kama kawaida kupita juu ya yale makaburi lakini umeme haukuweza kupita. waligundua ni pale baada ya ku trace all the way. tehetehe
hivyo that was the option
 
Makaburi yale yametangulia kabla ya barabara kujengwa,naam umeme umeletwa juzi tu hapa. Mizengwe ipo pale. lile kaburi la Martin kiyeyeu ni kubwa kama kibanda halafu limewekewa kama vidirisha feki fulani hivi. Madereva wa safari ndefu wanapajua pale.
 
here say!!!!! nilisikia kuwa mpango ulikuwa ni wa kuhamisha makaburi lakini ilishindikana baada ya negotiations za muda mrefu na wale ndugu (line ya machifu).

Kumbe we are talking the same ''here say'' niliona umesema si rahisi kulielezea swala lile kama vile nilivyoeleza kny post yangu ya kwanza re.ugumu wa kunegotiate na wahusika wa makaburi yale!
 
Duh! Kazi kweli kweli! Hivi pale hapawezi kuiingizia Serikali ya Mkoa au hata Mtaa Mapato? Naona kama ni eneo zuri sana kwa Utalii! Mbona Wenzetu Majengo tu waliyojenga Watawala wao Zamani yanatumika kama sehemu za Utalii na Watu wanavutika sana, Nenda Ujerumani Uone Makasri ya King Ludwig yanavyoingiza Pesa katika Serikali yao! This is a strange thing to hear that Umeme unashindwa kupita juu ya Makaburi, kama hili lina ukweli basi kuna haja Serikali kupaangalia mahala pale kwa jicho la Kitega watalii! Ni Muhimu kudocument sehemu kama hizi for easy of communicating information naamini watu wengi tu hawafahamu hii scenario but nimejaribu kuuliza watu wengi wamenipa majibu kama haya!
 
Mkuu naomba usiishie hapo, tafuta jamaa wa tanesco ili wamalize kabisa mzizi wa fitini......hizi shuhuda zilizotolewa hapa zote ni ''here say'' tu hakuna mwenye uhthibitisho kabisa na haya but i believe tanesco can confirm hii mystery!
 
4.jpg

Kaburi la Martin Kiyeyeu eneo la Malolo kilomita 30 kutoka Iringa kuelekea Mbeya ni maarufu kwa kisa cha kweli pale mafundi wa umeme waliposhindwa kupitisha waya wa umeme juu ya kaburi hilo. Walipojaribu kufanya hivyo waya zilikatika. Ndio sababu unaweza kuona hapo mbele waya zimekatisha barabara! Haya kuna wataalamu wa kutupa ufafanuzi wa kisayansi?! Kwa hiyo sayansi ya nguvu ya Giza ina nguvu kuliko sayansi ya Mzungu?
 
Mpwa wazungu lazima wakubali saa nyingine utaalam wao haufui dafu kwetu. Waafrika Ndivyo Tulivyo, siyo Miafrika Ndivyo Ilivyo.
 
hehehehe umeona mzee hapo electons zilidunda kwenye kaburi hilo jeupe huyo mzee alyezikwa hapo ndo Ndundami wa enzi hizo naona hata Mtwa Mkwawa alikuwa haoni ndani kwa sayansi ya Kibongo.
 
Ndiyo maana hatuendelei kwa sababu ya kuendekeza uchawi,kweli miafrika ndivyo illivyo.Kama uchawi ungekuwa dili zile nyungo zingekuwa zinatusaidia usafiri asubuhi tuwahi kazini,lakini hovyo kazi kukaba watu usiku.
 
Hujataka tu kuzipanda mamii.
 
Back
Top Bottom