Tanesco hawana mita[luku]

Mimi nimelipia Bukoba TANESCO kwa ajili ya umeme wa kijijini,jibu ni ilo ilo kuwa hawana LUKU,sasa ni mwezi wa tano toka nilipe karibu ya laki 6 kwa ajili ya umeme.Ushauri wa bure kwa TANESCO-Waondoe gaharama ya mita za LUKU kwenye charge yao ya kuwekewa umeme,kisha waruhusu watu binafsi kuagiza na kuuza LUKU madukani ili watu wawe free kununua LUKU popote zinapopatikana,vinginevyo kukaa na fedha za mteja aliyelipia kuunganishiwa umeme kwa muda mrefu siku moja mteja ata cancel nia ya kuwekewa umeme na kuwapeleka TANESCO mahakamani kudai interest kwa fedha mliyo kaa nayo bila kuunganisha umeme.
 
sasa imekuwa mazoea kwa tanesco kila weekend kuanzia ijumaa mpaka jumapili luku machine zote hazifanyi kazi ..kisa ni 'mtandao mbaya' ..jamani investment yote tuliyofanya kuweka mkonge -fiber optic- kutoka asia mpaka tanzania ..na mwengine kutoka south africa mpaka tanzania mtandao gani unakuwa slow kila siku? Mbona wenzetu kenya jamani hakuna excuse hizi za kijinga kijinga...
Hii ni sabotage dhidi ya tanesco...na wananchi..ni dhulma kwani tanesco hapa waliomba kuongezwa bei ya umeme lakini kama huwezi kuuza umeme kila siku...tanesco wanapata nini?
Sasa inatosha ondekeni tanesco kazi imewashinda....ngeleja wacha siasa za uongo ...hakuna mgao mgao upo kila siku bila ya hodi na pia kila weekend upo kwa njia ya kutofanya kazi machine za luku...huu ni ubabaishaji wa hali yajuu...ukosefu wa luku sasa ni tatizo....mwamzo wakitoa ecxuse ati maagent hawanunui umeme wa kutosha ..sio kweli hata tanesco hakuna luku...
Shirika limekua goi goi...uchumi unaporomoka no body cares !!!!! Hakuna kuwajibishwa mtu....watu wa it wapo na hakuna anewauliza inakuwaje luku kila siku zinaharibika? Hakuna kuwajibika
badria wewe kinara msemaji wa tanesco tunataka maelezo kwa nini kila weekend na mwisho wa mwezi luku hazifanyi kazi.....kwa nini wanaohusika wasiwajibishwe?
Tanesco kwa hili mujue munaimaliza nchi..umeme ndio kila kitu....
Ngeleja wacha porojo za siasa wajibikeni kwa wananchi...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom