Tanesco...Ewe Tanesco, NAKUCHUKIA SANA!

Museven

JF-Expert Member
Aug 22, 2011
629
447
Ukweli sina maneno laini yanayofaa kutumika kueleza hisia zangu dhidi ya shirika hili la umma! Ni lini yamepita japo masaa 12 mfululizo bila umeme kukatika? Sikumbuki. Leo tu wamekata na kuwasha mara 6 mchana na sasa hivi ni giza! Hawasemi kama kuna mgawo, marekebisho wala nini. Ni hujuma au nini? Hayo maendeleo yatapatikanaje bila nishati hii muhimu ya uhakika? Ukweli TANESCO, NAICHUKIA.... NAICHUKIA KULIKO CHOCHOTE !!!
 
Pole, umeripoti? Maana pia usiporipoti hawawezi kujua hakuna power, unless ni feeder nzima imetoka eneo lako
 
Maskini mtoto wa watu ambae ni Malaika tu kwani yeye ni mtoto kwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati na ni Mjukuu kwa Chama Cha Mapinduzi;
 
Midomoni mwao walisema hakuna mgawo wa umeme, Ila nyoyoni mwao walijua kwa dhati kabisa mgawo wa umeme upo. Na sisi watanzania ndo tunaipata athari yake live bila chenga, japo kuna watanzania wengine hawaamini kama kuna mgawo wa umeme. Nadhani watakapoguswa wengi ndo tutapata maelezo ya kina, kwa sasa tunasulubiwa wachache tu na hakuna wa kutusemea zaidi ya kuambiwa kuna marekebisho tu madogo ya kiufundi.
 
Hawa F#*knesco jana wametulaza giza usiku wote mpaka leo umeme haujarudi. Nchi hii sijui Kama usanii utakuja kuisha. Hii laana sijui ni nani aliivulia nguo Tanganyika na Wananchi wake!!:frusty:
 
Yani kwa mwendo huu, maendeleo tutayaona kwa nchi majirani zetu tu. Nchi hii inajiendea tu kama mbuzi wa Albadili, kana kwamba hatuna viongozi! Hakuna kipaumbele katika mipango yetu. Issue ya nishati ya umeme inavyochezewa! ...kama hakuna ajuaye unyeti wake katika uzalishaji mali. Ama ndio kuhujumu uzalishaji wa ndani ili tukuze soko la bidhaa kutoka nje? Aghh.... Tanesco mnakera bwana!
 
Back
Top Bottom