TANESCO board split on MD Rashidi's fate

The best person (mzawa) kuliongoza shirika kama Tanesco angekuwa Idrisa. Track record yake hata akiwa BOT ilikuwa nzuri. Mlishawahi kusikia matumizi mabaya ya account ya EPA au scandal yeyote wakati wa tenure yake pale BOT.

DCP iliyotafuna mabilioni ya fedha kuliko mwanaye EPA ilizaliwa wakati wa mzee rukhsa akiwa Raisi, Kikwete, Waziri wa Fedha na Rashidi, Gavana wa Benki Kuu. IPTL iliitangulia Richmond na wahusika wakuu wa IPTL ni hao hao - Mwinyi akiwa Raisi, Kikwete akiwa Waziri wa Nishati na Rashidi akiwa Benki.

Doa pekee labda ni hizo payment zilizofanyika kwenye account yake kupitia kwa Andy Chenge. La kustaabisha ni kuwa hamna/hakuna mtu aliyemfuata kumuuliza his side of story (kama anayo hiyo obligation).

Dili la Rada lisingewezekana kama lisingemshirikisha Gavana wa Benki wakati huo akiwa Dr. Idris Rashidi. Msaidizi mkubwa wa Chenge kama mwanasheria alikuwa mtaalamu wa fedha na msimamizi mkuu wa Benki Kuu ambaye alikuwa Rashidi.

Hatoi posho au magari kwa wa wabunge/wanasiasa .
Critics wake should come out with suggestions na siyo kulaumu tu. Kama mnaona hafai basi angalau msuggest nani anaweza kuchukua nafasi hiyo.

Labda hatoi posho kwa kuwa ni mchoyo - anajilipa yeye tu na wasaidizi wake au washirika wake wana nguvu zaidi ya hao wanasiasa. Umewahi kujiuliza baada ya hicho kiasi kikubwa cha fedha kuingizwa kwenye akaunti yake bado anatafuta nini TANESCO.
 
Asavali niondoke nikabeba mabox kuliko kukaa hapa,hamu sina kwa mambo ya hovyo Idrisa ni history hana vision ya kuongoza Tanesco!eti oh mtu makini oh namfahamu yaani uozo wote aliofanya bado mijitu inamfagilia.
 
Zitto nadhani una maslahi ktk issues za Dr rashidi na dowans vinginevyo usinge shabikia uozo huu eti rashidi ni mzuri wakati bei ya umeme inapanda kila siku, mgao mkali, n.k.

Kwa ufupi ni kwamba rashidi hana tena uwezo wa kufikiri zaidi ya hapo. Kinacho onekana pale tanesco eti inapata faida ni kutokana na kutowalipa IPTL, aggreko, dowans ndio maana inaonekana walau wanapata faida lakini kusema kuna improvement yoyote pale ni hakuna.
 
DCP iliyotafuna mabilioni ya fedha kuliko mwanaye EPA ilizaliwa wakati wa mzee rukhsa akiwa Raisi, Kikwete, Waziri wa Fedha na Rashidi, Gavana wa Benki Kuu. IPTL iliitangulia Richmond na wahusika wakuu wa IPTL ni hao hao - Mwinyi akiwa Raisi, Kikwete akiwa Waziri wa Nishati na Rashidi akiwa Benki.

Dili la Rada lisingewezekana kama lisingemshirikisha Gavana wa Benki wakati huo akiwa Dr. Idris Rashidi. Msaidizi mkubwa wa Chenge kama mwanasheria alikuwa mtaalamu wa fedha na msimamizi mkuu wa Benki Kuu ambaye alikuwa Rashidi.

Labda hatoi posho kwa kuwa ni mchoyo - anajilipa yeye tu na wasaidizi wake au washirika wake wana nguvu zaidi ya hao wanasiasa. Umewahi kujiuliza baada ya hicho kiasi kikubwa cha fedha kuingizwa kwenye akaunti yake bado anatafuta nini TANESCO.
Hebu njoo na ushahidi wa moja kwa moja. Dili la Rada lisingewezekana km asingemshirikisha????? Huu si ushahidi wa kiutendaji. Hawa na banker wa serikali. Serikali wanaweka pesa zao pale, mwenye fedha akizitaka je?? Rejea vizuri historia ya EPA maana mchezo huu umefanyika wakati wanahamisha zile akaunti toka NBC
 
Zitto,

..je, ni kweli kwamba Dr.Rashidi alituhumiwa ktk ripoti ya Tume ya Bunge iliyoongozwa na Edward Oyombe Ayila kwa ku-mismanage fedha za Import Support?

..wakati huo Dr.Rashidi alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara BOT. baada ya hapo akapelekwa NBC kuwa DG, na baadaye akateuliwa kuwa Governor.

..vipi kuhusu zile tuhuma za kujipatia mkopo toka PPF yeye na Frederick Sumaye?

..na hizi tuhuma za majuzi zinazomkabili yeye na Andrew Chenge?

..inawezekana kwamba jamaa ni efficient hapo Tanesco, lakini ifike mahali tuwakatae hawa watumishi wenye rekodi za kifisadi-fisadi.
 
Unaweza kuwa sahihi JokaKuu lakini kumbuka nchi yetu imejaa saana kupakana matope. Hebu angalia hoja za Mrema hapo pembeni, watu wanaandika tu ili kuchafuana. Hiyo issue ya import support na nyinginezo mbona asifikishwe mahakamani?
 
JF ina mambo mwingine anasema Richmond alisaini Dr Idris!
Richmond hakusaini Rashidi ila amedai kuwa hataki lawama pamoja na kwamba anataka mitambo ya kifisadi ambayo ni chakavu inunuliwe....Alitaka aondoke lakini bado wanamwitaji,kazi bado haijaisha,mitambo bado haijanunuliwa,kisingizio cha uchapa kazi,almost break even pamoja kwamba hakusaini Richmond aka Dowans anayoipenda ndio pazia la kuuwa soo.
 
Unaweza kuwa sahihi JokaKuu lakini kumbuka nchi yetu imejaa saana kupakana matope. Hebu angalia hoja za Mrema hapo pembeni, watu wanaandika tu ili kuchafuana. Hiyo issue ya import support na nyinginezo mbona asifikishwe mahakamani?
hizi tuhuma hazifikishwi mahakamani kwa sababu ni karibia wote walio kwenye position wanahusika au wanalindana.
Ndio maana sisi tulio hapa kwenye JF na kwingeneko tuna sema haya iliwote tuelewe adui yetu ni nani na jinsi gani ya kumuondoa, sio kumtetea au kumuhifadhi. Leo hii unaweza kufurahia, lakini kuna siku yata kukuta na hapo hutakuwa na wakukusaidia bali haki ikiwepo basi utapata kilicho chako.
 
Richmond hakusaini Rashidi ila amedai kuwa hataki lawama pamoja na kwamba anataka mitambo ya kifisadi ambayo ni chakavu inunuliwe....Alitaka aondoke lakini bado wanamwitaji,kazi bado haijaisha,mitambo bado haijanunuliwa,kisingizio cha uchapa kazi,almost break even pamoja kwamba hakusaini Richmond aka Dowans anayoipenda ndio pazia la kuuwa soo.
Vipi hamkuingia gizani kwa kuwepa DOWANS? Vipi sasa gharama za IPTL ni nafuu kuliko DOWANS. Yale mafuta yanauzwa kiasi gani. Tuache siasa za majungu. Ubishi na kuchanganya siasa na professional zimeligharimu Taifa.
 
bnhai,

..Viongozi karibu wote Tanzania ni wachafu.

..ukiona kiongozi amepelekwa mahakamani ujue wenzake wameamua kumtoa kafara tu.

..kesi kama za Liyumba na Mramba kwangu mimi naona ni suala la "funika kombe" tu.

..kwenye kesi kama ya Liyumba sasa imekuwa ni vichekesho tu manaake mashahidi wa mashtaka wanatoa kauli za kumsafisha mshtakiwa.

..Mramba anashtakiwa kwa kusababisha hasara ya Bilioni 11. wakati huohuo serikali imeamriwa na mahakama kulipa Bilioni 15 baada ya Waziri Magufuli kutoa amri ya kuvunja kituo cha mafuta kule Mwanza. kwa hali ya kawaida si Magufuli naye angepaswa kupelekwa mahakamani?
 
Nadhani hii ya Liyumba niliisema pia siku za mwanzo baada ya shahidi wa kwanza kuwa Liyumba atakuwa acquitted na serikali italipa fidia ya mabilioni.
Binafsi nashindwa kuelewa hii ya Rashid maana SFO walifanya uchunguzi ambao walikuwa na uwezo wa kushinikiza lolote kupitia kwa serikali yao lakini mpaka sasa kimya. Je, kuna ukweli upi katika haya? Ukiunganisha wapo watu wengi na wanafanya kazi zao kwa uadilifu lakini wanachufuliwa kwa sababu ya uadilifu wao.
Binafsi nilijipa fursa ya kupitia mahesabu ya TANESCO nikaridhika na utendaji.
Suala la mgawo, TANESCO peke yao hawaliwezi. Unahitajika uwekezaji wa hali ya juu. Nina hakika kama tutataka kuwa na umeme nchi nzima basi hata makusanyo ya serikali hayawezi kutosha. Hapa ni utashi wa serikali zaidi kuliko shirika.
 
bnhai,

..kesi ya Liyumba siilewi vizuri.

..kama gharama za mradi zimekuwa inflated basi siyo Liyumba peke yake anayepaswa kuchunguzwa. hapa inabidi Contractor na Project Consultant nao wachunguzwe.

..au labda Liyumba alikuwa anatoa malipo pesa ambayo Contractor hajadai, na Project Consultant hajaidhinisha.
 
Kama huielewi vizuri kwanini unaitolea mfano to me it does not make any sense. Ishu ya liyumba ni kwamba jamaa anatuhumiwa kutumia vibaya madaraka but swala linakuja is it possible and sensible kwa mtu moja au wawili peke yao kuwa ndio walioidhinisha hizo pesa?

Pili kama wao wameidhinisha utaratibu wa kiutendaji unasemaje what is the maximum limit wanaweza kuspend nadhani katika chombo kama BOT hicho kitu kinakuwapo. Sasa utakuja kuta kuwa bodi ndio inayohusika but what is board? Board ni wawakilishi ambao ni representative wa wadau au washirika wakuu ambapo kwa BOT ni serikali so mwisho wa siku unarudi katika mzizi ambao mwishoe unajiuliza who was in power unakuta Mr Big Ben. sasa je inakuwaje? Hivyo Liyumba mwishoe ataachiwa huru na serikali itamlipa mabilioni ya fedha kwa fidia ya usumbufu nothing else!!!!

Tuje kwa Idrissa muheshimiwa Zitto na bnhai nadhani wanaelimisha watu ambao either hawataki kuelewa au hawafahamu. Waswahili wanasema sikio la kufa halisikii dawa. Tujiulize kwanini Dr Idrissa amekuwa centre of the attention. Jibu unapata jamaa amekuwa akiwatolea uvivu wanasiasa na watendaji wabovu ofisini kwake. Alipokuwa BOT alihakikisha vimemo vilivyokuwa vikimpitia havitekelezi akapewa jina Chuma simple alikuwa akiwabania wazee ulaji.

NBC alitimua wafanyakazi wazembe na waliletwa na vigogo akawa anaonekana adui simply kwasababu alikuwa hapendi majungu. Kuna issue moja niliwahi kutolea mfano alikwenda mkurugenzi mmoja kumsemea kuhusu mwenzie (umbeya ambayo sifa yetu watanzania) akawa amewaita watu wote katika mkutano walipozungumza wakamaliza mkutano akasema tena nimesahau jamaa anasema ulikuwa unalalamika je ni kweli mbele za watu jamaa akawa ameona haya.
Tuje kwenye utendaji NBC alipoteuliwa aliikuta ikiwa hoi akaweza kuitoa katika loss ikawa inatengeneza profit mpaka wakawa wanawapeleka vijana shule. Alipoondoka BOT NBC ikaanza kupata loss tena imetokea wapi utajaza wewe msomaji!!!!.

Tuje Tanesco tatizo kuu lilipo tanesco ni kitendo cha Idrissa kuwadai Tanga Cement na kampuni moja ya simu bili zao na kuwapa notisi. Jamaa hakubali kuyumbishwa na wanasiasa wala watoto wa wakubwa. Likewise kama zitto alivyosema for the first time in many years Tanesco limeweza kubreak-even na likaweza kutazamika kwa financial institutions. Je!! Netgroup wamefanya nini? acheni unafiki jamani na majungu!!!.

SFO mie nawasubiri kwahamu watoe findings na utekelezwaji wao wanasema tu Dr Idriss amepokea $600,000 je tujiulize zilitokea wapi (since ni allegation tu) (sisemi kama idriss hajausika maana naye ni binaadamu but je ukweli uko wapi nadhani tuwaachieni mahakama). lakini pana maswali ya kujibu nani ametuma hizo $600,000 na je zimelipwa kwa ajili ya kitu gani? Utaratibu wa malipo ukoje tukishapata maelezo hayo na tukajua amehusika vp ndio tumhukumu venginevyo tunazungumza siasa na utumbo mtupu.

I rest my case!!!
 
Na mwisho nasema kama Mkapa hajafikishwa mahakamani ufisadi hautaisha
 
Mdondoaji,

..of course suala la Liyumba silielewi vizuri, na ndiyo maana nikauliza maswali kuhusu nafasi ya Contractor na Project Consultant.

..kuhusu suala la Rada una maelezo gani ya kumtetea Dr.Rashidi?

..pia madai kwamba Tume ya Bunge ya Edward Oyombe Ayila ilipendekeza Dr.Rashidi achukuliwe hatua nayo una utetezi gani?
 
Vipi hamkuingia gizani kwa kuwepa DOWANS? Vipi sasa gharama za IPTL ni nafuu kuliko DOWANS. Yale mafuta yanauzwa kiasi gani. Tuache siasa za majungu. Ubishi na kuchanganya siasa na professional zimeligharimu Taifa.
Dawa ni kutupa jongoro na mti wake....Kusema kweli mimi ni mtizamaji tu,sina isight,na kwa wenye insight kama wakipita hapa lazima watakuwa wanatucheka sana....Maana wanajua ni karata gani ya kucheza kwa wakati gani kwasababu hata sisi tunasubiri wao watasema nini and so tunachambua upi mchele ipi chuya.Hata hivyo nia hasa ya mafisadi ni kutulazimisha sisi tu "play by their rules" kwamba sasa heri nusu shari kuliko shari kamili....Gharama za IPTL ni kubwa sana hivyo tununue mitambo ya Dowans..Na ndio maana kuna wasiojali shari kamili,kwani hukusikia kuna wenye kudai kuwa heri wakae gizani kuliko kununua mitambo ya Dowans?

All in all inategemea ni kwanamna gani ufisadi unakugusa,how it has impacted your life and how you feel about it...Kuna watu wamezoea harufu mbaya na wanaweza hata wakala na kupiga stori bila hata kujali uvundo huo,wanaweza kusahahu harufu hiyo na kuendelea na shughuli zao,vile vile kuna wanaoweza kusahau ufisadi kwani umeshazoeleka na mawazo ya watu wa namna hiyo certainly yataonekana kama mawazo ya ajabu ajabu,on the other hand,kuna wasioweza kuzoea uvundo huo(ufisadi)inakuwa vigumu kuendelea na shughuli za kawaida kwani uvundo hauvumiliki.

However,accountability ndiyo itakayodignify professionalism,binafsi hapa sizungumzii kuhusu kashfa zinazomkabili through out his courier,pointi yangu mimi hapa ni the overall role anayoplay kwenye issue hii,kwa jinsi anavyo act si kwamba hataki siasa,maana kama that was the case angeshajiuzulu.

Kama uteuzi wake ulikuwa wa kisiasa to begin with,then sioni ni kwavipi performance yake itakuwa nje ya misingi hiyo,ambayo ndio iliyopelekea yeye kuwekwa kwenye post hiyo.....Kama wale wanaopendelea aendelee kuwepo hapo wanamwelekeo wa kusapoti uvundo wa ufisadi ambao unawanufaisha baadhi ya wanasiasa,then wale wanasiasa wasioweza kuvumilia uvundo wa ufisadi lazima watapinga hatua zozote zenye kuonekana zinawanufaisha mafisadi....The same applies kwetu sisi wananchi,kuleta madai ya mgao ni kutufanya wananchi wajinga kwani mgao haukuanza leo...Sijui sana kuhusu IPTL,lakini na yeye hakuhusika?
Ili kuumaliza ufisadi ni lazima tu sacrifice big times,tena inawezekana kwamba inabidi tu start from scratch....Kuach remnants ni kuaccept defeat,if we are to get rid of it once and for all,then we MUST start from scratch.
 
Moja tu - Amechukua u CEO pakiwa na hasara ya 162bn kwa mujibu wa audited accounts za 2006. 2007 hasara ilishuka mpaka 67bn. 2008 imeshuka mpaka 30bn na mpaka june 2009 tayari TANESCO ilikuwa imebreak even. Kama sio mgawo wa Septemba, Oktoba na Novemba wangepata faida mwaka huu.

Mbili - kwa mara ya kwanza Taasisi za fedha zimekopesha TANESCO 400bn na wana service mkopo huo bila tatizo lolote na hivyo kuweka mazingira ya kukopa zaidi.

Tatu - Shirika lina mpango wa muda mfupi, wa kati na mrefu wa kuzalisha na kusambaza umeme. Miradi yote ya kuanzia mwaka jana imekwamishwa na Serikali kama Mhisa mkuu.

Nne - Sasa Shirika lina rejesta ya mali zake zote (zenye thamani ya 1bn usd) na wakati Rashidi anaingia CAG alitoa disclaimer audit opinion kwa kuwa pamoja na mambo mengine Shirika halikuwa na orodha na thamani halisi ya mali zake. NHC wana tatizo hilo na Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma iliwatimua na mpaka leo hawajaweza kufanya kama TANESCO.

Tano - Yupo very clear anataka Shirika lifike wapi kwa muda gani. Kwa mfano kama Mhisa pekee (serikali) angetekeleza commitment zake na faida iliyotarajiwa mwaka huu ikawa realised, lengo lilikuwa ni kustain faida kwa miaka mitatu ili TANESCO iuze hisa zake DSE na hivyo public listed company - kuongeza uwazi kwa mujibu wa masharti ya PLCs.

Niendelee?

Zitto

mbona uko shallow hivyo? Hiyo hasara iliyopunguzwa uliomba kupata detailed schedule kujua ni ongezeko la Revenue au kupungua kwa gharama za uendeshaji kabla ya conclude?Kwa mfano kama malipo ya Richmond yalisimamishwa na unacompare vipindi hivyo viwili lazima utaona tofauti.je bei ya umeme iliongezwa? kwenye uhasibu tunaita analytical Review sio unakurupuka tu nakusema ooh hasara imeshuka kwa hiyo rashid ni mkurugenzi mzuri jiulize what were the factors leading to that?je accounting procedures zimebadilishwa.. kwa mfano unaweza kukuta kuna vitu vilikuwa vinakuwa expensed sasa viko capitalized wher u just charged depreciation in the PL kwa bottom line number inaonekana nzuri,kuna mambo mengi ....inabidi ujue accounts...... Yani mtu anahusika kuchannel pesa za rada unamwita best CEO .. anyway haishangazi sasa ... waarabu wa pemba hujuanan kwa vilemba...
 
Thats why i luv JF,critical and professional analysis,tunahitaji vichwa kama hivi..Hii inanikumbushia Mkapa anapodaiwa kuukuza uchumi na huku umasikini ukishamiri,na ukiangalia kiundani,matumizi ya mafisadi kwa kushirikiana na makaburu ndo vilikuwa vigezo kwamba uchumi unakuwa,mfano manunuzi ya mashangingi,matumizi yake kwenye mafuta nk....Hizo factors leading to zinakuwa ignored,shukrani sana mkuu kwa hii analysis,nakubaliana nayo moja kwa moja.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom