William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,374
Hii unaitoa wapi ? Tumeingia vita ya Kagera dola ikiwa kati ya sh. 7.00 na sh. 8.00. na tumemaliza vita dola ikiwa bado sh. 8.00. Miaka mitano baadaye 1984 dola ilikuwa bado ni chini ya sh. 10.00. Haya madai yako unayatoa wapi ? Kama kuna kitu alikitaa Mwalimu kata kata ni misaada yenye masharti na sharti mojawapo lilikuwa ni kushusha thamani ya fedha yetu. Unajua kwa nini alituomba tufunge mkanda ? Utanisamehe huu ni mchango wangu wa mwisho, kwaheri.
- Mkulu Mag3, hapa tupo ukurasa mmoja, unajua kwa kawaida huwa situpi risiti ya anything katika maisha yangu, hoja yako ni nzito na ninataka kuweka ushuhuda kwamba Mwaka 1983 nilisafiri kwenda majuu na nilinunua dola za US hii benki ya NBC karibu na Sanamu, dola moja kwa Shillingi 8.00,
Mwaka 1987 miwishoni nilisafiri tena kwenda majuu, benki hiyo hiyo nikanunua dola moja kwa shillingi 16.00, na ninazo risiti mpaka leo, ninakumbuka Mwalimu akilalamika kwenye hotuba yake ya Mbeya, kuhusu kupanda kwa bei ya matrekta ya kilimo kufikia Shillingi Laki Sita za Tanzania then,
- Balaa la kupanda kwa dola kulinganisha na shillingi, lilianzia kwenye Utawala wa Miwnyi na alipokuja Mkapa, ikawa a free fall!
Respect.
FMEs!