TANESCO board split on MD Rashidi's fate

Kwa jinsi ninavyofahamu, Dr. Rashid angekuwa one of the best CEO kama ambavyo mnasema basi tungeona performance yake pale Tanesco. Uwezo wa mtu unapimwa na performance yake! Kama mnataka kumtetea kwa kusema eti anaingiliwa na bodi ya wakurugenzi, waziri husika, katibu mkuu na baadhi ya wakurugenzi wizara ya nishati na madini basi angejiuzuru mapema na huo ndio weledi duniani kote!!

Professionalism means meticulous adherence to undeviating courtesy, honesty, and responsibility in one's dealings, plus a level of excellence that goes over and above the commercial considerations and legal requirements. Professionalism is not about your job title or self-proclaimed worth. It is not about self-perception at all. Professionalism is about personal ethics, quality work and a quality attitude.

Na kama kuna mazingira ya watu kukushurutisha ufanye jambo ambalo ni kinyume na wewe unavyoamini, you resign!!

Hata kama Rais atakuomba urudi unampa masharti ya kurudi, akishindwa kukutekelezea you quit!!!

He is just another failure, period!!!!

Ukitaka kuiona utaona utaiona. Hawezi kuwa 100% ila kuna mambo kasawazisha sana TANESCO. Ongea na wafanyakazi
 
Siasa...........! tungeacha mashirika yakawa na bodi huru na kuziwekea malengo na kuzipima kutokana na malengo mashirika haya yangeenda vizuri sana. Siasa zinaingia sana na huyu Rashidi ni mmoja wa CEOs anayewakatalia wanasiasa waziwazi. Wanamchukia sana. Mfano kawaambia Wizara walipe pango la jengo la TANESCO, wizara eti hawataki..... CCM nao wameng'ang'ania Rest House ya TANESCO dodoma, amewatimua. Wamekasirika. Basi ni matatizo tu..... Sasa kwenye kampeni wanataka waweke CEO goigoi awape pesa maana Rashidi hatakubali na wao wameshazoea.....

Kwa hili la kuwa na bodi huru na kuunga mkono mh, na ulipokuwa unaliongelea bungeni kwamba wabunge wasiwe board members nilishangazwa sana na jinsi hoja ilivyopingwa.

If you have a weak board of directors you will definetely have a weak management team. Angalia mfano hai katika kesi ya Liyumba, mashahidi (board members) wanaeleza wazi kuwa they had a weak board of directors that could not even question the governor (who ridiculously was the board chairman)!!

Haya yalishafanyiwa utafiti tka miaka ya tisini kule UK (Sir Robert Smith: Effectiveness of Non executive Directors), South Africa (King I & II reports) na tafiti zingine nyingi tu.
 
Ukitaka kuiona utaona utaiona. Hawezi kuwa 100% ila kuna mambo kasawazisha sana TANESCO. Ongea na wafanyakazi
Zito Kabwe, wafanyakazi wape posho mbilimbili na safari za kutosha daima watakusifu na kukuona Mungu mtu, kuwauliza wafanyakazi ubora wa Idriss Rashid huwezi kuupata ukweli.
nenda maliasili na utalii ulizia ubora wa Zakhia , utashangaa anavyoabudiwa, nenda Hazina ulizia Blandina Nyoni utashangaa na Roho yako, nenda Ardhi ulizia mtu anaitwa Getrude Mongela utaambiwa, wanawasifu kwasababu walikidhi haja ya matumbo yao.
 
Facts are there - labda hujazitafuta tu. Kote alikopita kuanzia NBC, BOT etc

Hiyo naweza kufanya homework kupata details. Lakini mh huyu Dr. kama anaingiliwa kwenye maamuzi au ushauri wake haufanyiwi kazi kwanini asijiondoe? Hapo ndipo tunadefer unapopewa kazi inabidi uifanye kwa uhuru sasa kama unaingiliwa then u quit simple. Lakini kama anaendelea means he there not to perform but kuchuma then aende zake. Au ndiyo wale wanaozeeka na performance inapungua kinyume na uhalisia.
 
labda vijana/mkuu wanataka/anataka kutekeleza kwa vitendo uamuzi wao kwamba more opportunities kwa vijana in the context kwamba idrisa ni kijana
 
Zito Kabwe, wafanyakazi wape posho mbilimbili na safari za kutosha daima watakusifu na kukuona Mungu mtu, kuwauliza wafanyakazi ubora wa Idriss Rashid huwezi kuupata ukweli.
nenda maliasili na utalii ulizia ubora wa Zakhia , utashangaa anavyoabudiwa, nenda Hazina ulizia Blandina Nyoni utashangaa na Roho yako, nenda Ardhi ulizia mtu anaitwa Getrude Mongela utaambiwa, wanawasifu kwasababu walikidhi haja ya matumbo yao.

Hilo mkuu nalo ni tatizo lingine watu wanatanguliza matatizo yao kabla ya mambo mengine. Labda mh. ZITTO atupe yeye alikuwa anamaanisha nini? Wafanyakazi waulizwe ok je watajibu kuwa turbines zimeongezwa? Au ndiyo hayo ya hizo samani? Mh tusaidie hapo.
 
Facts are there - labda hujazitafuta tu. Kote alikopita kuanzia NBC, BOT etc

Mkuu hatukatai mtu waweza kuw ana rekodi nzuri sana huko ulikotoka.......hivi scandal ya RADA ikoje sasa hivi....ameshakuwa cleared?.....vipi na ule utetezi wake wa Bank ya Meridian......?

.......otherwise wanachosema Mugerezi + Brooklyn......ili kulinda heshima kama Professional.......unaachia ngazi.........

Hatuwezi ku-count kashfa za mtu kwenye "perfection"......eti hawezi kuwa 100% perfect.......if you get what i mean...........
 
labda vijana/mkuu wanataka/anataka kutekeleza kwa vitendo uamuzi wao kwamba more opportunities kwa vijana in the context kwamba idrisa ni kijana

Mkuu mimi sielewi hawa jamaa unajua mtu unapukuwa mkubwa kiumri tunaamini kuwa unakuwa na busara zaidi hata maamuzi yako yanakuwa mazuri lakini whats the problem with our leaders? Poor decisions, no vision etc.
 
Mimi kwa taarifa nilizo pata toka wakati ule alipokuwa BOT ni i.e Governor alikuwa ni Mtu Competent sema miaka ya Mwanzo, lakini wana siasa walimuharibu na yeye akakubali kuharibiwa, kwa sasa namuona hafai hata, labda tusema kwamba wana siasa wana muhitaji kwa shughuli zao za kifisadi.
Sasa tukiachana na Historia yake huko nyuma, tuangalie utendaji wake wa hapo Umeme ambao upo wazi, kama yeye angekuwa mtu makini, tusinge ingia mkataba wa Richmond, na kama alilazimishwa, basi asinge kuja kutetea ununuzi wa Dowans na matawi yake, jingine tusinge ingia kwenye mgao wa sasa, jingine ni matumizi mabaya ya fedha tena za mkopo kwenye shughuli ambazo si za uzalishaji au zilizotarajiwa kuwezeshwa kutokana na huo mkopo.
Kwa binadamu au kitu chochote kuna vitu vinavyo onekana na vilivyo fichika, na hivyo ni vashiria vya mtu kuwa mzuri au mbaya, sasa kwa kuangalia hivyo viashiria vinavyo onekana na visivyo onekana kiutendaji utaona Idrisssa hafai amekosa kuwa mtu wa msimamo na ameunga mkono/ na kutekeleza vitu vinavyo dumaza uchumi.
Mbona alimkatalia Mwenyekiti wa Bodi Gari, sasa alishindwa nini kuzui matumizi mabaya ya fedha za Mkopo, Yeye ni mwanauchumi, ana uwezo mkubwa wa kumshauri EL, na JK je aliwashauri nini kuhusu maafa ya mikataba ya Richmond nk.
 
Zito Kabwe, wafanyakazi wape posho mbilimbili na safari za kutosha daima watakusifu na kukuona Mungu mtu, kuwauliza wafanyakazi ubora wa Idriss Rashid huwezi kuupata ukweli.
nenda maliasili na utalii ulizia ubora wa Zakhia , utashangaa anavyoabudiwa, nenda Hazina ulizia Blandina Nyoni utashangaa na Roho yako, nenda Ardhi ulizia mtu anaitwa Getrude Mongela utaambiwa, wanawasifu kwasababu walikidhi haja ya matumbo yao.

Miafrika ndivyo tulivyo...kila kitu tumbo street, hivyo ukiniwezesha kuvimba tumbo nitakusifia tu hata km unaharibu kinoma!!
 
Mimi namuona Rashid kama fisadi tu. Huyu si ndiye aliyehamishiwa $600,000 na Chenge kwa kusaidia dili la rada? SFO walipombana akababaika. Aachie ngazi Tanesco huku akisubiri kesi yake. Tusipende sana kuwafagilia watu wanaopora utajiri wetu. Zitto anamtetea huyu fisadi kwa sababu zilizo wazi. (Refer utetezi wa ununuzi wa mitambo chakavu ya Dowans). Rashidi aliwekwa pale na Rostam baada ya kumtumia kule Vodacom. Aliwekwa Tanesco mahsusi kwa ajili ya ku-facilitate wizi wa kutisha wa kundi la mafisadi papa kupitia mikataba feki. Kwa kuwa wanaona hawajamaliza kazi ya kutuibia kwa njia ya mikataba mingi feki ya nishati ndio maana wanataka aendelee pale.
 
Hana umakini wowote kwani nakumbuka akiwa Gavana wa Bank kuu kulikuwa na Bank moja inaitwa Meridian Biao Bank na ikafilisika na nadhani tetesi zilianzania Amerika ya Kusini kuwa imafilisika na Idrisa Rashid akaitetea sana kuwa hapa Tanzania ipo imara lakini baada ya muda ikafilisika
kuporomoka kwa NBC kulianza wakati Idrisa akiwa Mkurugenzi Mtendaji, hata mipango ya kuipiga bei kwa makaburu aliibaliki yeye!! ila huyu jamaa ana ngekewa sana maana badala ya kumfuta kazi wakati alipoifilisi NBC akapandishwa cheo na kuwa Gavana!
 
The best person (mzawa) kuliongoza shirika kama Tanesco angekuwa Idrisa. Ni mtu ambaye hababishiwi na wanasiasa. Track record yake hata akiwa BOT ilikuwa nzuri. Mlishawahi kusikia matumizi mabaya ya account ya EPA au scandal yeyote wakati wa tenure yake pale BOT.Doa pekee labada ni hizo payment zilizofanyika kwenye account yake kupitia kwa Andy Chenge. La kustaabisha ni kuwa hamna/hakuna mtu aliyemfuata kumuuliza his side of story (kama anayo hiyo obligation).
Hatoi posho au magari kwa wa wabunge/wanasiasa .
Critics wake should come out with suggestions na siyo kulaumu tu. Kama mnaona hafai basi angalau msuggest nani anaweza kuchukua nafasi hiyo.
 
Namuomba Mh. Zitto atupe facts zake zinazomfanya pengine aamini kuwa Dr. Rashid ana perform ku-deserve hizo sifa ili wadau tuzichambue.

I personally consider Dr. Rashid as one of the learned man, but totally disagree on his competence (ability to deliver tangible results).

Efficiency is measured by ability to deliver quality and reliable services with minimum cost possible. Lakini mchumi huyu amekuwa akiwabebesha mizigo walalahoi kwa kuwaongezea bei ya umeme badala ya kutafuta namna ya kubana matumizi na kutafuta njia mbadala wa kuzalisha umeme sustainable.

Kwa taarifa nilizonazo Tanesco imeingia mkataba uchwara na kampuni moja(jina kapuni) wa ku supply transifoma. Bei ya transifoma za kawaida (hizi tunazowekewa mitaani) ni mil 2-3 lakini jamaa (jina kapuni) ana supply kwa over 8 mil.

Binafsi sijaona mafanikio yoyote aliyoyaleta pale Tanesco.
 
Heeeeeeeeeeee, are you serious? Tuwe wakweli kidogo enh. Usije kuwa kama jamaa mmoja humu anayesema Makweta siyo Mbunge. Rashidi kaingia NBC lini, katoka lini kwenda Benki Kuu na kabla ya hapo alikuwa nani na hali ya kifedha ya NBC ilikuwaje etc.
Kuweka rekodi sawa, NBC haikuwahi kufilisika toka imeanza mpaka Mkapa alipokuja kuiuza bila kujali mawazo ya Nyerere na Watanzania. NBC haikuwahi kupata hasara wakati wote Rashidi akiwa Mtendaji Mkuu na hata alipokuwa Gavana. NBC haikuuzwa wakati wa Rashidi akiwa Benki Kuu na ilipouzwa yeye alienda kufanya kazi NMB - Benki ya Walalahoi na sio NBC kwa makaburu. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
The best person (mzawa) kuliongoza shirika kama Tanesco angekuwa Idrisa. Ni mtu ambaye hababishiwi na wanasiasa. Track record yake hata akiwa BOT ilikuwa nzuri. Mlishawahi kusikia matumizi mabaya ya account ya EPA au scandal yeyote wakati wa tenure yake pale BOT.Doa pekee labada ni hizo payment zilizofanyika kwenye account yake kupitia kwa Andy Chenge. La kustaabisha ni kuwa hamna/hakuna mtu aliyemfuata kumuuliza his side of story (kama anayo hiyo obligation).
Hatoi posho au magari kwa wa wabunge/wanasiasa .
Critics wake should come out with suggestions na siyo kulaumu tu. Kama mnaona hafai basi angalau msuggest nani anaweza kuchukua nafasi hiyo.

Heri mwananchi wa kawaida hana muda wa kumpima Dr. Rashid kwa vigezo vya kutowapa posho mbili mbili wabunge or the likes. Kipimo chao ni kimoja tu...Je Tanesco wanawapatia umeme wa kutosha katika kipindi chote cha mwaka kwa bei competitive???

Kwa taarifa tu, mfumuko wa bei umefikia 'double digit' na sababu kubwa inayoelezwa ni kukosekana kwa umeme kulikosababisha wazalishaji nchini kutumia nishati ya mafuta ambayo ni ghali zaidi na hivyo kupelekea kupandisha bei bidhaa wanazozalisha!!!
 
Other members of the TANESCO board of directors are Victor Mwambalaswa, Agnes Bukuku, Juma Bakari, Vintan Mbiro, Semindu Pawa, Beatus Segeja, and Ngosi Mwihava.

Hivi hawa wote kuna hata mmoja mwenye ABC za mambo ya umeme?

Watajifunza wakiwa ndani ya system...
 
Namuomba Mh. Zitto atupe facts zake zinazomfanya pengine aamini kuwa Dr. Rashid ana perform ku-deserve hizo sifa ili wadau tuzichambue.

I personally consider Dr. Rashid as one of the learned man, but totally disagree on his competence (ability to deliver tangible results).

Efficiency is measured by ability to deliver quality and reliable services with minimum cost possible. Lakini mchumi huyu amekuwa akiwabebesha mizigo walalahoi kwa kuwaongezea bei ya umeme badala ya kutafuta namna ya kubana matumizi na kutafuta njia mbadala wa kuzalisha umeme sustainable.

Kwa taarifa nilizonazo Tanesco imeingia mkataba uchwara na kampuni moja(jina kapuni) wa ku supply transifoma. Bei ya transifoma za kawaida (hizi tunazowekewa mitaani) ni mil 2-3 lakini jamaa (jina kapuni) ana supply kwa over 8 mil.

Binafsi sijaona mafanikio yoyote aliyoyaleta pale Tanesco.

Moja tu - Amechukua u CEO pakiwa na hasara ya 162bn kwa mujibu wa audited accounts za 2006. 2007 hasara ilishuka mpaka 67bn. 2008 imeshuka mpaka 30bn na mpaka june 2009 tayari TANESCO ilikuwa imebreak even. Kama sio mgawo wa Septemba, Oktoba na Novemba wangepata faida mwaka huu.

Mbili - kwa mara ya kwanza Taasisi za fedha zimekopesha TANESCO 400bn na wana service mkopo huo bila tatizo lolote na hivyo kuweka mazingira ya kukopa zaidi.

Tatu - Shirika lina mpango wa muda mfupi, wa kati na mrefu wa kuzalisha na kusambaza umeme. Miradi yote ya kuanzia mwaka jana imekwamishwa na Serikali kama Mhisa mkuu.

Nne - Sasa Shirika lina rejesta ya mali zake zote (zenye thamani ya 1bn usd) na wakati Rashidi anaingia CAG alitoa disclaimer audit opinion kwa kuwa pamoja na mambo mengine Shirika halikuwa na orodha na thamani halisi ya mali zake. NHC wana tatizo hilo na Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma iliwatimua na mpaka leo hawajaweza kufanya kama TANESCO.

Tano - Yupo very clear anataka Shirika lifike wapi kwa muda gani. Kwa mfano kama Mhisa pekee (serikali) angetekeleza commitment zake na faida iliyotarajiwa mwaka huu ikawa realised, lengo lilikuwa ni kustain faida kwa miaka mitatu ili TANESCO iuze hisa zake DSE na hivyo public listed company - kuongeza uwazi kwa mujibu wa masharti ya PLCs.

Niendelee?
 
Zitto ndugu yangu sawa inawezekana anafaa ila tutaishije na doa la RADAR? Mbona tumeshindwa kuishi na doa la RICHMOND tukamvua Uwaziri Mkuu mtu ambaye wadau wanakiri ni mtendaji wa hali ya juu? Unataka kusema LILA na FILA sasa VINATANGAMANA?
 
Back
Top Bottom