Tanapa ajira- who know you?? Bila kimemo huajiriwi, mh ezekiel maige unajua hilo??

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Kati ya mashirika yenye bureaucrazy katika ajira ni TANAPA na NGORONGORO CONSERVATION.

Hakuna uwazi katika ajira. Watoto wa Vigogo fulani fulani au watu wenye majina ndo wanaajiriwa.

Solution: Nashauri Tume ya Utumishi waajiri Katika TANAPA.

Namshauri Waziri Ezekiel Maige afuatilie hii kitu, afanye uchunguzi.
 
tupe mfanoa hapa. Na wewe ushawahi kuomba kazi mara ngapi ukanyimwa and we have to know elimu yako ndugu na sio una certificate ya njuweni zenu umecompete na watu waliosoma degree obviosly utaishia kulalamika tu.
 
Ndugu Ivuga, Ndo maana nimesema Waziri afanye uchunguzi athibitishe. Maana hizo ni tuhuma nzito tena za muda mrefu.

Kawaulize Mweka au UD au Vyuo vyote wanaotoa graduates wenye fani hizo.

Hakuna criteria zilizo wazi au zinazoeleweka katika ajira
 
Mkubwa hiyo siyo TANAPA tu, mtindo huo upo almost katika taasisi zote za umma Tanzania!
 
Mifumo mingi chini ya utawala wa ccm ni mibovu sana,haiwezekani kutatua tatizo kwa njia ileile,solution pekee ni ccm kuondoka na mifumo yao mibovu,,
 
Nakubaliana na hoja kuwa kwa issue ya ajira, ni kila sehemu hapa nchini. Mtoa hoja wa kwanza, unless una specific mfano, kutaja sehemu hizi mbili tu kunaifanya hoja yako kuonekana haina nguvu. What about Division za wildlife, Fisheries, Forestry and Bee Keeping ect ambazo zipo pia chini ya wizara husika ?

Hivyo vyuo vinatoa wahitimu wengi, na hatutarajii wote waajiriwe mara moja na taasisi hizo mbili tu. Na pia kumbuka kuna SUA pia ambao wanatoa wahitimu ktk field hiyo, bila kusahau Tumaini University ect
 
Tanapa inahitaji iundwe upya inaumiwa mara kwa mara kwanza kwa zaidi ya mwaka sasa haina mkurugenzi mkuu inaendeshwa na makaimu , madirector wanapokezana , idara ya manunuzi na pr zinaitajiwa kuwekwa watu wenye ujuzi waliopo sasa ni mafisadi tu wanakupa kazi huku wanataka mgawane fedha .
Tanapa pameoza
 
Ahh sasa tumesharukia idara ya PR na manunuzi kutoka issue za ajira ?

Kutokuwa na mkurugenzi ni kosa lao au la serikali ? Serikali ndiyo inabidi iundwe umpya. Nchi inaongozwa na mafisadi, ss unashangaa idara moja, mbili za mashirika ?

Huyo waziri kila siku anapiga jaramba na waandishi wa habari, kwani hajui kuwa hakuna mkurugenzi ?
 
Hadi kazi ya kuuza baa siku hizi lazima umjue mtu, sio kazi za TANAPA tu.

Sijui hii nchi inaelekea wapi wajameni, utashangaa mwenye degree lower lower second kapata kazi kwa kumjua mtu na mwenye upper second anasugua mguu mtaani hana kazi kisa mtoto wa Kabwela asiemjua mtu.
 
sehemu nyingi sana kuna urasimu-ila kuna vjana wameajiriwa wiki hii TANAPA bila kuwepo kwa uchakachuaji wowote-kwa hio si mara zote kuna kuwaga na urasimu
 
Haya sasa, yale niliyosema Leo yamethibitishwa na CAG.

Soma Gazeti la Mwananchi ukurasa wa 3. Heading - CAG aibua uozo wa ajira TANAPA
 
Haya sasa, yale niliyosema Leo yamethibitishwa na CAG.

Soma Gazeti la Mwananchi ukurasa wa 3. Heading - CAG aibua uozo wa ajira TANAPA

mkuu nimekupata,ila nadhani haya mambo ya Tanapa/urasimu ulikuwepo tok kipindi cha Mkapa?
 
Kujua urasimu ulikuwepo toka lini haijalishi. Cha maana watu wajue kuwa TANAPA ina urasimu na inabidi Waziri Ezekiel Maige achukue hatua.
 
yaa,hya mashirika ya umma yangekua yanatoa ajira hizi kupitia kwenye ile secretalieti ya ajira ambayo iko chini ya utumushi?ayaaa yte manunguniko yasingekuepo,pia siyo tanapa pekee kuna hii mifuko ya jamii kama LPF,PPF,NSSF na PSPF,mambo ni haya ahya tu,mimi nadhani ilikuondoa urasimu na upendeleo inabidi ajitra zote za serikali na mashirika yte ya ummaa ya toe ajira kupitia bodi ya ajiraaa........:A S 39:
 
Back
Top Bottom