Special thread; Tamthilia ya Siri za Familia Inayorushwa EATV

Ni tamthilia nzuri na naipenda sana shida ipo kwenye muendelezo mfano siku ile carlos anamfumania sheila na abdul asubuhi aliondoka kavaa suti kabisa na sheila ndo alimfunga tai ila alirudi kavaa jinzi na shat na koti...jumatatu apa juzi walionyesha ya jumanne nyingine(yani ile ya kesho yake) lakini jana tukaona nyingine...kuna vipengere vingi vinaonyweshaga kama ya kesho yake lakini havionyweshwi.

Kuhusu Episode tofauti kuonyeshwa hiyo ni kweli. Ni Kosa la Transmission EATV. Badala ya kurusha Episode ya 38 walirusha ya 39 so nadhani ikabidi warudie baada ya kupata taarifa.

Kuhusu makosa ya kiufundi, yapo madogo madogo ambayo watu makini kama wewe unaweza kujua. Tulikuwa na Changamoto za kutengeneza Episodes 49 kwa muda wa wiki 6 tu. Watani wa Episode 8 kwa wiki. So kazi ilikuwa inafanyika usiku na mchana. Sometimes Wasanii wanakuwa na dharura na wanaporudi tunakosa continuation kwa sababu za kimsingi. So hilo linakubalika japo flow ya Story bado iko vile vile.
 
Lakini pia yule mama yake carlos alikataa ghafla tu carlos asiwe na mazoea na abdul bila kuonyesha kisa nini na hapo hapo akiwa bado anajua ni mwanae mama gani anataka watoto watengane lakini..mwisho tunaona tu tony ndo anaambiwa ndugu yake carlos kajuaje na imekuaje hatujui.. Pia wakati dayana anaumwa tumbo kameza dawa hakuonekana na tumbo kubwa wakati yeye alipata mimba kabla ya sheila na sheila mimba tayari ilikua kubwa ilitakiwa tuone dayana tumbo lake..otherwise ni tamthilia nzuri sana sema kuna vimakosa vidogo sana wahusika wapo vizuri yani inaburudisha na kuelemisha kwakweli

Bi Moza alizaa na Marehemu Chief Zumo ila mtoto toka mchanga alilelewa na Zumo na hawakuonana hadi anafariki.

Kama uliangalia Episodes za nyuma Bi Moza alikwenda Ofisini kwa Carlos akamkosa lakini alibahatika kumsikia Abdul akiongea kwa Simu na Kumtaja Chief Zumo. Bi. Moza alipomuuliza Abdul maelezo yalishabihiana na Chief Zumo ambaye Bi. Moza alizaa naye. Abdul kuona siri zake zitagundulika akaamua kudanganya yeye ni Mtoto wa Zumo. Baada ya mazungumzo marefu Bi. Moza akawa ana uhakika Abdul ni Mtoto wake.

lakini Mtoto halisi wa Zumo ni Tony ambaye alibadili majina (Jina lake Ethani) makusudi ili kufanikisha upelelezi wa mali za baba yake. Tony ni mpya katika kampuni ile na alikuja kwa kazi maalumu. Baba yake alifariki katika mazingira ya kutatanisha akiwa yuko masomoni nje ya Nchi.

Tuendelee kufuatilia.
 
Tangu juzi wametuchanganya watazamaji kuhusiana na muendelezo wa tamthilia yenyewe, nadhani kuna mkanganyiko sehemu labda studio. Hata marudio huwa inakuwa saa 4.30 asubuhi lakini nimeangalia leo asubuhi na jioni saa 12.30 naona ni ileile ya asubuhi wameonesha jioni, wakati ya asubuhi huwa ni marudio ya jana yake. Siku 2 ama 3 hizi mmetuvuruga.

Apologies. Ni kweli.

EATV walirusha Episode 39 badala ya 38
So ikabidi warudie 38.

Sasa mwendelezo utarudi sawa kwa kuendelea na Episode 40.
 
Ila mama carlos baada ya kugundua kuwa Abduli si mtu mzuri aliambiwa na baba sheila... nahisi alichunguza na kujua ...wakati wa Tony anamsimulia juu ya Miradhi anayofatilia ya marehemu mzee zumo...ndipo yule mama aligundua Abdul kamdanganyaa.......

Noted.
Kuna simu huko nyuma ambayo Abdul aliongea nayo na hiyo ndo ilifanya mama ajue abdul ni Mtoto wa Zumo kumbe kamdanganya for a reason ya mali.

Tony hakujua kuwa Bi Moza ni mama yake hadi alipompeleka Hospitali na baadaye wakawa na maongezi ambayo Tony alijitambulisha kiuhalisia kuwa yeye ni Mtoto wa Zumo. Hapo ndo Bi. Moza akashtuka.
 
Instagram: @sirizafamilia

Salaam Sana

Kwa wale wanaofuatilia tamthilia ya "Siri za Familia" (Family Secrets) inayorushwa EATV hii ni thread maalumu kuhusiana na Tamthilia hiyo.

Familia nyingi zina siri ingawa zinatofautiana. Baadhi ya siri zinaweza kujulikana na familia yote au wachache au hata mwanafamilia moja. Siri zinaweza kuhusiana na miiko, ukatili, mahusiano, magonjwa, uhalifu, mauaji, ubakaji nk. Jambo lolote ambalo mtu au familia inadhani linaweza kuleta tafarani linafanywa siri ya familia.

Hata hivyo hakuna siri ya watu wengi au ya muda mrefu kwani baadhi ya siri hatimaye hufichuka na siri zingine mtu anaweza kufa nazo. Je, ni nini kinatokea pale siri za familia zinapofichuka?

Fuatitlia thread hii ya Siri hizi katika SIRI ZA FAMILIA inayorushwa EATV kila siku ya Jumatatu hadi Alhamisi kuanzia saa 12.30 jioni hadi saa 1.00 jioni na kurudiwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 4.30 asubuhi hadi saa 5 asubuhi. Marudio ya wiki nzima ni siku ya Jumapili kuanzia saa 8.

Sasa hivi tamthilia inayorushwa ni season 1 na ina episode 48. Season 2 iko katika maandalizi.

Kwa wale wapenzi tukutane hapa kwa maoni na hata wenye visa vya kweli ambavyo wangependa viwepo katika Season 2. Visa vingi vilivyopo katika Season 1 ni visa vya kweli na vinatokana na utafiti uliofanywa na visa vya kweli ambavyo wadau wanavileta.
Story za beki3
 
Wadau waasalam
Leo naileta kwenu tamthiliya ya *SIRI ZA FAMILIA* inayorushwa kupitia kituo cha luninga cha east Africa television (eatv)

Tamthiliya hii imekuja wakati ambao wapenzi na mashabiki wa michezo ya kuigiza Tanzania walikuwa wanakosa kitu wanachotaka toka kipindi cha takribani miaka kumi iliyopita ambapo michezo hii ilikuwa iking'ara vema kupitia luninga ya ITV na waliibuka watu wengi wenye uwezo

Mimi binafs nimeifatilia kwa karibu sana hakika vijana wanaitendea haki tamthiliya hii
Jina linaendana na maudhui yalyomo ndani kila muhusika anaitendea haki script yake na pengine maradufu

Hakika in mlolongo wa hadithi nzuri na tamu ambapo ukibahatika kuangalia Mara moja hutathubutu kupitwa hats Mara moja
Inagusa maisha ya kila siku ya kifamilia usaliti,mapenzi ya kweli,uaminifu,uvumilivu,siri,majonzi,magonjwa
Nichukue nafasi hii kuwapongeza wahusika waliotengeneza na waliocheza pia
Baadhi ya waliocheza humu ni mtaala Carlos,sheila,Diana,bi subira, cleop,Abdul na wengine wengi

Mi huwa sivutiw na hii michezo sana ila hii imenibamba

Hongereni kwa ubunifu ndani ya siri za familia
 
wanatukumbusha Enzi za ITV michezo ili ilikuwa ikitengenezwa na mwongozaji krisant Mhenga.

Huyu Bwana ndiye Aliye wazalisha, wakina Marehemu Stephan Kanumba. Vincent Kigosi. Dr cheni. Carlos. Swebe. Sinta. Marehemu Max na Zembwela, Bambo.

Sasa hivi tumekosa waandaaji wa zuri kama ndugu Mhenga.

Nitoe pongezi zangu za thati kabisa kwa Ndugu Super man. A.K.A Nsimbe. Kwa kutuletea mambo Ambayo alikuwa anayafanya Ndugu Krisant Mhenga.

BG UP Bro. Kazi nzuri sana.
 
Back
Top Bottom