Tamko Langu

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
kwa muda wa masaa kadhaa sasa jumuiya ya wanamtandao ya watanzania imepata piga moja ambalo sio kwamba tu limeamsha hisia za kiuzalendo na kuendelea kupigania haki na usawa bali imetimiza ile ahadi yake ya kuendelea na mapambano ya kifikira kama mwanakijiji anavyosema

pigo hili ni kukamatwa kwa wanachama wawili wa moja ya forum maarufu sana katika afrika mashariki na kati < hawa ni wapiganaji wenzetu < ndugu zetu majirani zetu na wazalendo wetu wamekamatwa kwa sababu ya kuendelea na mapambano haya ya fikira .

nilipopata habari hii nilishituka sana na kuhuzunika sana nikijaribu kukumbuka hizi simu za vitisho watu wanazopata kutoka kwa watu wasioeleweka na wanapojaribu kutoa taarifa kwa vyombo husika wanashindwa kupewa msaada wa kutosha wakati mwingine hadi kitu kidogo .
pamoja na hii kamata kamata inayoendelea sisi katika sekta nzima ya ict kuna mambo inabidi tuwekane sawa na kuelimishana ili siku zijazo iweze kutengenezewa sheria au hata kama sakati hili likiishia mahakamani kijulikane kinachoongelewa ni nini .

watu waliokamatwa ni 2 inaonyesha walikamatwa wakati wakiwa sehemu moja katika office moja na inawezekana sana ni wafanyakazi wa serikali au sehemu kubwa ambapo kuna administrator anayeweza kutumia baadhi ya software kujua fulani anatembelea tovuti zipi na zipi >

kama ndio hivyo basi administrator wa sehemu hii ndio amefanikisha kukamatwa kwa vijana hawa , huyu administrator amefuata sheria gani za nchi za kuweza kufumbua siri za watu wengine au wale anaowahudumia kwa watu wengine kama hivi inavyotokea ?

je katika kampuni , shirika au sehemu husika hawana privacy policy yoyote inayoongelea mambo haya kwa ufupi au urefu ? ingawa ni kweli wizara nyingi na kampuni nyingi hazina privacy policy mtu anaweza kutoa siri huku akapeleka huku bila kuwasiliana na mtu wowote yule .

kutokana na kamata kamata hii inatupasa wapenzi , wadau na watu wote wanaohusika na suala zima la ict kuanza kupigania baadhi ya vifungu vya sheria virekebishwe na viongezwe katika katiba za nchi ili kuweza kuendana kwa wakati wa sasa na ujao .

inashangaza kwa vijana hawa kukamatwa kwa zaidi ya masaa 24 bila kupewa dhamana bila kupewa ruhusa ya kuongea chochote na mtu wowote na pia wamewekwa katika sehemu yenye mazingira mabaya kiafya na kimaadili ile sehemu sio salama hakuna mtu anayeweza kuwahakikishia usalama vijana hawa hata kidogo >

na je wamekamatwa kwa kufuata sheria zipi au vifungu vipi vya sheria vilivyomo katika katika yetu ya jamhuri ya muungano wa tanzania ama ni ubabe ule ule kama tuliouzoea ?

pamoja na kuandika hivi tunaomba wahusika wa utekaji nyara huu wawatendee haki watekwa na waache sheria zifuate mfumo wake na watuweke wazi au waje mbele ya watanzania katika vyombo vya habari watueleze kwanini wamewakamata na wanategemea nini kutoka kwa vijana hawa .

hali inatisha sana kwa hakika lakini sisi tunasema hatutachoka kupambana na mtu yeyote ambaye hatendei mema taifa hili , wala jamii yake ukitenda maovu lazima yasemwe na kupigiwa kelele sehemu zote za wenye kupenda ukweli na maendeleo

pengine Huu ndio mwanzo wa vita vitakatifu vya fikra , tunajua mwanzo ni mgUmu lakini njia tumeshaona kwahiyo tutasaidiana kwa mali na hali kuhakikisha jamii ya watanzania inafahamishwa kile inachotakiwa kupata yaani haki zao na kuhakikisha tunapigana na wahujumu wote popotE wanapopatikana au kunusa
 
Back
Top Bottom