Mshume Kiyate
JF-Expert Member
- Feb 27, 2011
- 6,766
- 894
Pongezi kwa wabunge wa Dar es Salaam, wabunge wengine mikoani wanatakiwa kuiga huu mfano linapotea jambo la maslahi ya Umma mnaweka pembeni ukelekweta wa vyama
Wapi makongoro mahanga kwenye list ya MPs?
Ndugu zangu,
Bunge letu limeanza kuchangamka. Ndio, nimeanza kulifuatilia Bunge kwa muda mrefu. Sasa naiona tofauti. Na jana tu, nimemwona David Kafulila akishambulia bungeni kwa kujiamini. Ni kwenye mjadala wa bajeti ya Wizara ya Usafirishaji na Uchukuzi.
Kafulila anasimama na kutamka; Wabunge wenzangu tukomae bila kujali itikadi zetu. Tukomae jamani, hawa jamaa fedha wanayo ya kuimarisha usafiri wa reli. Anasema Kafulila wa NCCR- Mageuzi.
Na hiyo ndio maana ya Bunge- wawakilishi wa wananchi kuongea kwa kutanguliza maslahi ya umma, maslahi ya nchi. Na Bunge lina maana ya kulonga kwa maana ya kuongea. Bunge halina maana ya kunongona na kulala.
Na pengine wengine hawajui, kuwa neno la Kiingereza Parliament kwa maana ya Bunge linatokana na neno la Kifaransa Parle kwa maana ya kuongea. Hivyo, Le Parleament kwa Kifaransa ina maana ya jengo ambamo waliomo wanaongea kwa niaba ya waliowakilisha.
Ndio, tunahitaji Bunge kama Kariakoo na Buguruni na si Oysterbay na Masaki. Kariakoo , Buguruni na kwingineko ndiko waliko Watanzania wengi. Wanaamka saa kumi alfajiri na wanalala usiku wa manane. Si kwa kupenda- wanahangaika na shida za dunia. Ndio, kule Kariakoo na Buguruni watu wanaongea kuanzia saa kumi alfajiri mpaka saa saba za usiku. Na wanakerwa sana wanapowaona wabunge wao wanalala bungeni, au wananongona.
Tuje kwa Wabunge wa Dar es Salaam. Wamenifurahisha sana. Hili ndio Bunge ninalotaka kuliona. Kwamba, kwenye maslahi ya taifa, wabunge wasiendekeze ushabiki wa vyama. Nina hakika Watanzania wengi wamevutiwa na hatua hii ya Wabunge wa Dar es Salaam. Kwamba bila kujali ushabiki wa vyama vyao, wameamua kwa pamoja, kama timu ile ya Barcelona kushambulia kwa pamoja kwa kuivalia njuga kashfa ya mauzo ya hisa za UDA.
Na wabunge wa Dar es Salaam wameweka wazi; wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi ule wa fedha za umma wabingirishwe mchangani. Na hawakuuma maneno, wamemtaja Idi Simba, Meya Masabuli na wengine. Kwa hatua ile ya Wabunge, bila shaka, watu wa Dar es Salaam wamefurahi sana. Lakini wanasubiri kuona hatua zinazochukuliwa kwa watuhumiwa hao wa ubadhirifu wa mali ya umma.
Na wabunge wa Dar es Salaam wakitaka waendelee kuheshimika na kuwa mfano kwa wabunge wengine, basi, katika hili la UDA na iwe Bayankata kwa kwenda mbele. Waweke ushabiki wa vyama kando. Na kama Barcelona .
Naam, tumewaona wabunge wa Dar es Salaam wakipanda kwa pamoja na kushambulia. Sasa kazi kwao ni kubaki katikati na kukomaa ' Kibayankata'- Ndio yenyewe! Na kama kuna kushuka na kujihami, basi, washuke kwa pamoja, A la Barcelona!
Maggid,
Msamvu, Morogoro
Ijumaa, Agosti 8, 2011
0754 678 252
http://mjengwa.blogspot.com
Kwa alivyo jieleza Mzee Iddi Mohamed Simba nakubaliana nae kabisa kuwa wamemlipa kama consultation fee kwani ana kampuni yake ya ushauri inayoitwa INTERFINAS (International Finance Advisory Services) na kwa wawekezaji wengi wanaifahamu kwani inajihusisha na kutoa ushauri mbalimbali wa kibiashara.
Hii Inahitaji pongezi ya hali ya Juu SANA!! Ila kwa hao wawekezaji uchara nawaunga sana Mkono kwa nia yao Njema ya kutaka kuboresha usafiri Dar es Salaam ambao Hali ni Mbaya kupindukia!! Huwezi kabisa Kujivuni hali ya usafiri wa Public Kwa jiji la Dar es Salaam kwa Hali ya kawaida huu usafiri siku zote naufananisha na Jehadamu!! Huwezi kusema unaishi kwenye Ulimwengu wa Sayansi na Technologia halafu kuwezi hata kuplan kufika mahali fulani on Time!! Huku tukiona wanaotakiwa kufanya hizi planning wakineemesha Matumbo yao Bila kutumia akili zao KUFIKIRI!!
NAPENDEKEZA YAFANYIKE YAFUATAYO KWA WANA HISA WETU WAPYA
1: TATHMINI HALISI YA SHIRIKA IFANYIKE KWA KUSHIRIKISHA TAASISI ZINAZOHESHIMIKA NA KUJUA THAMANI HALISI YA SHIRIKA KWA SASA NA MALI ZAKE ZOTE
2:HAWA WABIA WETU UCHWARA WASHUKURIWE KWA KUONYESHA NIA YA KUWEKEZA NA KIASI CHA HELA WALICHOTOA KITAFSIRIWE KATIKA HISA NA WAPEWE PORTION YAO YA HISA HATA KAMA NI 6% NO PROBLEM ILA WATAKUWA NI SEHEMU YA WAWEKEZAJI
3:HILI SUALA LA IDDI SIMBA KUCHUKUA SEHEMU YA MALIPO NAONA LITAKUWA LA BINAFSI ZAIDI KWANI HAWA WAWEKEZAJI TUTAWATATHIMINI KUTOKANA NA KIASI WALICHOWEKEZA NDANI YA AKAUNTI YA UDA, NA KAMA HAWAJAWEKEZA CHOCHOTE TUACHANE NAO
4:NINGEWASHAURI TAKUKURU WAFUATILIE TARATIBU HUSIKA ZA MALIPO ALIYOYAPATA IDDI SIMBA KAMA YANA UHALALI WOWOTE AU NI SEHEMU YA RUSHWA NA AWEZE KUPELEKWA KUNAKO HUSIKA
5IA NDUGU ZANGU WA TRA WAJUE NDIO MUDA MUAFAKA WA KUCHUKUA KODI KWENYE MALIPO HAYA YA NDUGU SIMBA NA SIO KUFUATILIA MISHAHARA YA WATU NA HUKU KUNA WATU WANAMALIPO MAKUBWA BILA KUYALIPIA KODI!!
Wapi makongoro mahanga kwenye list ya MPs?
Mokongoro ni mjomba wake masaburi na ni wabia wa chuo cha ugavi kule chanika
Tamko hili limetolewa tarehe 4 Agosti 2011 na wabunge wafuatao wa mkoa wa Dar es salaam:
Abas Mtemvu-Mwenyekiti,
John Mnyika-Katibu,
Mussa Zungu,
Dr Faustine Ndugulile,
Philippa Mturano,
Mariam Kisangi,
Zarina Madabida,
Iddi Azzan,
Halima Mdee,
Eugine Mwaiposa,
Angellah Kairuki
Prof. Fennella Mukangara
Mokongoro ni mjomba wake masaburi na ni wabia wa chuo cha ugavi kule chanika
Conflict of interest, huwezi kuwa mwenyekiti wa bodi halafu ukajipa kazi ya consultancy. Mwenyekiti wa bodi akishakuwa mmoja wa wazabuni, hivi kweli UDA wanaweza kumnyima kazi hata kama hakushinda? Jamani tuwe na uzalendo, hata kama ana kampuni hiyo ya ushauri akafanyie pengine sio UDA ambapo yeye ni mwenyekiti wa bodi.
Kumbe kuna issues wapinzani na chama tawala mnaweza kukaa na kukubaliana? Safi
Wapi makongoro mahanga kwenye list ya MPs?