Wabunge wa DSM. Kwa hili la UDA angalau tunawapongeza lkn hatuwasifu sana mpaka tuone mwisho wake kama ya UBT. Tunahitaji kujua ukweli wa mradi wa Maji (DAWASCO) uliofadhiliwa na ADB maarufu Mradi wa Wachina wakati ni mkopo kwetu. Tupewe ukweli kwa nini ulikabidhiwa/haujakabidhiwa wakati maeneo mengine maji hayatoki? Miundombinu ya mabomba yaliyotandazwa bila maji inayoharibika kila siku itakarabatiwa na nani. Je miradi ya kusambaza maji kwa magari ni dili za madiwani hao waliouza UDA kiharamu? Kumbukeni sasa kumekucha. Agenda hizi usafiri na barabara, maji, viwanja n.k, msipozishughulikia kwa uzalendo uliotukuka tutawazomea na kuwadhalilisha kwenye majukwaa na barabarani.