TAMKO la UVCCM Arusha 25/5/2011 SOMA UJIONEE!

Chatanda kazini!

Hii inakuja baada ya kutishiwa juzi na maandamano ya vijana waliotaka ang'oke!
Sasa patakuwa na sinema ya kufa mtu kati ya makundi haya mawili ya UVCCM, yaani UVCCM-LOWASSA, na UVCCM-CHATANDA.
Lakini in any way, UVCCM-CHATANDA is bound to loose, na kwa nguvu ya fedha bwana Ole-Millya ataisambaratisha kwa mbali sana kambi ya CHATANDA!
Nadhani Lowasa huko aliko hatolala, na atapiga simu usiku kucha kuhakikisha wenye mdomo wanashughulikiwa!
 
Huu ni upuuzi mkubwa watu wanapiga kelele RA, EL na Chenge waondoke CCM! waondoke waende wapi? Ujinga huo! yaani mtu andoke kwenye chama chake kwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa mujibu wa itikadi ya chama chake? Unaweza kushauri Dr. Slaa, Lissu na Mbowe waondeke Chadema? huo ni upumbavu na kelele za kusumbuwa watu bila sababu.

Kama kuna mtu hapendi hizo sera na Itikadi mpya za CCM yeye ndio aondoke CCM njia ipo wazi, kelele za nini, Nape amejaribu kakiona cha moto! kaamua kutumia msemo wa 'If can't fight them join them' au la! aondoke yeye ingawa alijaribu kuondoka kupitia CCJ akashindwa.

Ni vyema watu wakaelewa kuwa hiyo ndio kazi ya CCM watambue hivyo na wakubali hivyo! kama hawapendi hayo mambo ya CCM basi waame huko watafute chama kinacho pinga sera za Ufisadi.
 
Labda haya ndio madhara ya utandawazi, some few years back, usingesikia UVCCM wanatoa matamko left right kiasi hiki. Maadili yameporomoka kwa kiasi kikubwa na sijui kama kuna uwezekano wa kupata remedy!!!!!! UVCCM taifa wao wamelala usingizi mzito na kukoroma!!!!

Tiba
 
Arafat kuna subsitance katika ulichosema, hiyo ndio ccm and thats how it is going to be, anayeona hapana ajiondoe yeye atafute chama lingine. kama kwa kasi aliyokuja nayo Nape on these three giants kaishia tu kufyata mkia hakuna nayeweza na kama hakubaliani ahame yeye chama. kwa hili nimekubaliana nawe
 
Ccm inahitaji kuwa na systerm nzuri ya kutoa info,na matamko mbalimbali.Hali hii ya kila mwanachama kujisemea anavyojua tena kwenye vyombo vya habari itakigharimu chama sana.Huyu atakuwa Chatanda kawalipa watu wawili au watatu ili wamsaidie kulinda kibarua chake.hali ni ngumu kwa chatanda na milya.
 
Mwaka huu ni :mod::mod::mod::mod::mod::mod::mod::mod::mod::mod: kizunguzungu:mod::mod::mod::mod::mod:!!! Yangu macho!
 
TAMKO LA VIJANA WA CCM MKOA WA ARUSHA
Tarehe 25/05/2011
Ndugu zangu waandishi wa habari leo tumeona tuwaite hapa ili tuweze kutoa maoni yetu kuhusiana na mustakabali wa chama chetu cha Mapinduzi na Jumuiya yetu ya Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha. Tumewaita hapa kwa malengo makuu Sita:-
Kuunga mkono Halimashauri kuu ya CCM Taifa kwa kuona umuhimu wa kuifanyia kazi kwa vitendo falsafa ya kujivua gamba. Tunaipongeza na kuiunga mkono Halmashauri kuu ya CCM Taifa kwa kutambua kwamba mafisadi wamechangia sana kukidhoofisha na kukipotezea mvuto chama chetu mbele ya umma wa watanzania. Kwa mantiki hiyo tunatamka kwa
kauli moja kwamba mapacha hao watatu wa kifisadi ambao ni Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge na vibaraka wao wafukuzwe mara moja kwa maslahi ya CCM na Watanzania. Pia tunasisitiza kuwa Andrew Chenge aondolewe kwenye kamati ya maadili ya CCM mara moja na wakati huohuo Edward
afukuzwe kwenye kwenye ya uwenyekiti wa Bodi ya udhamini
ya umoja wa vijana wa CCM Taifa haraka iwezekanavyo.
Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunamtaka kuwa James Millya ambaye ni kibaraka mkuu wa mafisadi mkoa wa Arusha ajiuzulu mara moja na tunatamka rasmi kumfukuza kwenye UVCCM mkoa wa Arusha ili apate fursa ya kwenda kuwa tumikia mafisadi. Tunamtaka James Millya aache kufikiria kwa kutumia tumbo na badala yake atumie kichwa. Pia tumeshaandika barua yenye kumbukumbu namba
kumb. Ars/Malalamiko/01 kwenye Chama kuelezea namna alivyo mnafiki, mfitini,mwongo na namna asivyo jali maslahi ya vijana wa UVCCM mkoa wa Arusha. Vilevile tunapenda kuujulisha umma wa Tanzania kuwa Ally Bananga anaetumiwa na Millya pamoja na mafisadi hana nafasi yoyote ndani ya Umoja wa vijana wa CCM kuanzia kwenye tawi hadi Taifa. Kwa mantiki hiyo Ally Bananga aache mara moja kuganga njaa kwa kutumia jina la UVCCM. Pia tunampa onyo kali Catherine Magige aache mara moja kutumia fedha za mafisadi kuwagawa vijana wa Arusha kabla hatujatumia haki yetu ya kikanuni ya kumsimamisha Ubunge. Tunajua kuwa amepata ubunge kwa nguvu za kifisadi kupitia UVCCM. Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunakiomba chama cha cha mapinduzi kiwafukuze mara moja makatibu wa UVCCM kutoka wilaya za Monduli, Arumeru, Longido na Karatu kwa kushiriki mandalizi ya maandamo haramu na kwa kukataa wito wa chama wa kwenda kutoa ushahidi wa malamiko yao kuhusu mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa. Kitendo hicho cha kukataa wito wa Chama ni dharau na ukosefu wa maadili. Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunatamka kwamba ili kulinda hadhi ya CCM mkoa wa Arusha tunamtaka Onesmo Nangole ajiuzulu mara moja kwa kuwa anafanya kazi ya Fisadi
Edward Lowasa na si ya CCM. Kitendo chake yeye cha kufanya kazi ya mafisadi na si ya CCM kimetupelekea kupoteza majimbo mawili kwenye uchaguzi mkuu wa 2010. Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunatamka kwamba Mhe. Mary Chatanda (MB) ambaye ni katibu wa CCM Mkoa wa Arusha ni mpiganaji na ni lulu ya CCM mkoa wa Arusha. Amefanya mengi ya maana na wa-CCM makini, wazalendo na wanaojali maslahi ya chama chetu wanatambua hilo. Pia tunawaomba CCM Taifa waendelee kumwacha hapa Arusha ili aendelee kukijenga chama na kukomesha mafisadi pamoja na dagaa wao. Sisi vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Arusha tunatamka rasmi kumtambua Ndugu. Mrisho Gambo kuwa ni mjumbe halali wa baraza kuu la UVCCM Taifa kuwakilisha mkoa wa Arusha. Tunamuunga mkono kwa ujasiri wake, umahiri wake na uzalendo wake wa kupambana na ufisadi ndani ya chama na Tanzania kwa ujumla. Na huo ndiyo msimamo
wetu kwa kuwa una tija kwa vijana wa Tanzania. Tunashauri CCM Taifa kuwaita rasmi mapacha watatu wa kifisadi (Edward Lowasa, Rostam Azizi na Andrew Chenge) kwenye kamati ya maadili ya CCM Taifa na kisha kuwafukuza mara moja kama kweli tuna nia ya kuendelea kuwa chama tawala katika nchi hii.

TUTASEMA KWELI DAIMA FITINA KWETU MWIKO
KAULI YETU: KULINDA NA KUJENGA UJAMAA
KITADUMU CHAMA CHA MAPINDUZI BILA MAFISADI
 
Jamani jamani. Hivi pamoja na kuwa magamba mnaogombana mnataka kuendelea kutawala kihivi. Nendeni shule kwanza. Upupu mtupu
 
hivi mlioandika mnadhani sisi watoto....pelekeni utoto wenuhukohuko ccm...wewe gambo tunakujua nimnafiki mkubwa tana wewe fisadi number moja natunasikia ulikua unafr.... na elisa molel hadi akakuhonga starlet.....wewe endelea kuvuruga vijana wenu naukome kutajataja cdm hatuhitaji takataka kama wewe,,,,,,,kama uliweza kuwasaliti wenzako nabado ukabaki hukohuko kwenye magamba hata kwetu hatukutaki baki magambani.........kwakifupi vijana wa ccm hamna akili msituletee upuuzi wenu huku sio mahali pake............habari zako tunazipata kazi yako kuuza habari hapo manispaa ya Arusha nakureport kwahilo gamba lingine isdori shirima,kila linaloendelea unapeleka watu wanadai hii tabia yauchoko unayo tangu tanga tech kwanza ukisoma tuu unafahamu walioandika hawana akili wakiongozwa nawewe gambo mwambie huyo riz1 boss wako anayekutumia amechemsha...............................................tumechoka ujinga wenu msituletee mambo yachuki binasfi hatutaki unafiki
 
Kweli tutaona na kusikia mengi!
Watoto wanawavua nguo Wazee tena wenye MVI nyingi!
Adabu imetoweka kwenye chama cha MAGAMBA.
 
Ccm wamezoea mipasho siku zote huwa wanakurupuka wanafanya mambo bila kujali watasomeka au la sasa hapa vita ni chitanda na mamvi .vijana wanatumika kotekote kimsingi Taifa limenajisiwa mambo yanapandiana
 
Back
Top Bottom